Tangu nijiunge na JF nimekuwa nikisoma posts nyingi ambazo waandishi wake wamekuwa wakitumia, katika uandishi wao, lugha vibaya. Lugha hizo aidha ni Kiingereza au Kiswahili. Hii inaonyesha kuwa waandishi hawa wamezoea kutumia lughahivyo hata wanapoongea. Kwa vile JF ni jamvi la kufundishana, naona si vibaya kuanzishwa forum ya lugha, ambapo pindi mwandishi wa post atakapokosea kuandika kwa ufanisi sahihi, wana JF wataweza kumsahihisha. Kufanya hivyo itatuwezesha pia sote kujifunza na kueneza ufanisi wa legha zetu hizi.