Sildenafil Citrate
JF-Expert Member
- Jan 29, 2021
- 572
- 2,553
Unaelewa nini ukiambiwa umeze dawa kutwa mara tatu?
Maduka mengi ya dawa pamoja na hospitali zetu hutumia lugha hii kimakosa pasipo kuwaelewesha vizuri wagonjwa. Kwa kiasi kikubwa, huwafanya wagonjwa wasitumie vizuri dawa wanazopewa.
Siku moja ina saa 24, kwa kuzingatia mgawanyiko sawa wa vipindi vya kumeza dawa, mgonjwa hupaswa kuzimeza kila baada ya masaa 8. Hivyo, badala ya kusema dawa imezwe kutwa mara tatu, ni vizuri ikisemwa kuwa imezwe mara tatu ndani ya saa 24, au kila baada ya masaa 8.
Vivyo hivyo kwa kutwa mara moja, au kutwa mara mbili. Mgonjwa anapaswa kuambiwa ameze mara moja tu kwa siku, au mara mbili kwa siku kila baada ya masaa 12 mtawalia.
Watoa huduma wanapaswa kuhakikisha kuwa wanatoa maelezo kwa usahihi, pia wagonjwa wanapaswa kufuata maelekezo hayo ili kuongeza ufanisi na kupunguza madhara ya dawa husika.
Neno kutwa huleta maana isiyo sahihi kimantiki, huwafanya wagonjwa wameze dozi nzima ya dawa kwa mgawanyiko wa saa 12 pekee yaani asubuhi, mchana na jioni pasipo kukumbuka kuwa siku nzima huhusisha mjumuiko wa saa 24.