Jana usiku CCM wamezindua kampeni ya kuchangia kampeni kwa kutumia simu za mkononi!
Makadirio ni kwamba watakusanya taslimu 40,000,000,000/=(bilioni 40)!
Mimi nilipotazama jinsi washiriki wale walivyochangamka kutoa kwa kutuma ujumbe, nilihamasika kwamba iwapo ungeanzishwa uchangiaji wa namna hiyo kwaajili ya madawati ya shule zote nchini, hakuna mtoto ambae angekaa kwenye vumbi!
Kama jana, ziliweza kupatikana milioni 20 ndani ya dakika 5 tu za uchangiaji, je kwa miaka 5 ya uongozi wa JK, wananchi wangechanga kiasi gani, na tungekuwa wapi?
Kwanini wabongo tunapenda kufanya fund-raising za 'Disposable cash, kama hizi kampeni, tisheti na harusi, unlike kuwekeza kwenye investment za kudumu kama elimu, afya na miundombinu?
Ningekuwa mimi ndo JK, ningesubiri hela yote hiyo ichangwe, kisha natangaza ghafla kwamba hakutakuwa na kampeni, hela zote zinatumika kupeleka maji, au kujenga dispensari vijijini!
NINA HAKIKA 100% KWAMBA CHAMA CHANGU KINGECHAGULIWA BILA KUPINGWA NA RAIA YEYOTE...Unaonaje?
Waheshimiwa, jana CCM ilizindua kampeni ya uchangiaji kwa wanaachama na wakereketwa kama wanavyojiita niliangalia lakini kuna kitu hapa tuchangieni:
Mwenyekiti wa taifa CCM kwa kusisitiza uchangiaji alisema
Jamani tuichangieni CCM, tukukumbuke chama hiki kilivyoifanyia nchi hii. Je? Wanajamvi bila CCM nchi hii haingekua hapa? Au ingekua mbali zaidi? Na je ni CCM imeifanyia Nchi mambo mazuri au Inchi ndio imeifanyia CCM kua hapo?
Karibuni.
Hivi nyie tuko pamoja!!....nawaogopa brodas!
Mara nyingi nasoma post zenu wala sizijibu.....kazi yangu kusoma naju yepi hoja za msingi na yepi pumba! Katika hili sikubaliani nanyi. Suala la kukusanya fedha za kampeni kwaajili ya CCM ni jambo jema wala sioni tatizo. Leo hii CHADEMA wakichangisha fedha kwaajili ya kampeni yao na uhakika you dont comments at all badala yake mtasema chama kinajizatiti kupata ushindi! Tatizo la wana JF ni kwamba karibia WOTE ni wapinzani wa chama Tawala CCM! Sijaona hoja yoyote ya msingi katika hili na katika mengine yote yalopita isipokua ni porojo mingi za Waswahili ! Badala ya kujadili issues kama East African Federation na impacts zake mnamjadili JK akikusanya fedha kwa wapiga kura wake ili kuwezesha chama kushinda. Ninyi mngetaka achangishe wapi, kwa nani kama siyo kwa wapenzi wa chama chake? Angeanza tu kampeni bila fund-raising si mtasema kaiba? Acheni TAARAB, Maneno maneno, chokochoko na Uswahili wenye nia ya kuchafuana. Kama mnaweza nanyi changisheni hamnyimwi..lakini yote tisa CCM kitashika tena hatam na mtaongozwa na serikali yake kama kawaida. Nilishasema mimi SIYO mwanachama wa chama chochote cha siasa bali an "OBSERVER". Tafakari!!!!

Hii injulikana kabisa!...Fundraising hizi zinatumika kama smoke-screen kuwazuga watu, ili waelewe kwamba nccm walichangisha, kumbe vyanzo vyao ni vilevile vya mwaka 2005!Lakini wajanja tushawastukia!Na huyu jamaa wa Push-Mobile ni mdau nini wa filthness inayoendelea kwenye system ya sisiem nini?