Jana usiku CCM wamezindua kampeni ya kuchangia kampeni kwa kutumia simu za mkononi!
Makadirio ni kwamba watakusanya taslimu 40,000,000,000/=(bilioni 40)!
Mimi nilipotazama jinsi washiriki wale walivyochangamka kutoa kwa kutuma ujumbe, nilihamasika kwamba iwapo ungeanzishwa uchangiaji wa namna hiyo kwaajili ya madawati ya shule zote nchini, hakuna mtoto ambae angekaa kwenye vumbi!
Kama jana, ziliweza kupatikana milioni 20 ndani ya dakika 5 tu za uchangiaji, je kwa miaka 5 ya uongozi wa JK, wananchi wangechanga kiasi gani, na tungekuwa wapi?
Kwanini wabongo tunapenda kufanya fund-raising za 'Disposable cash, kama hizi kampeni, tisheti na harusi, unlike kuwekeza kwenye investment za kudumu kama elimu, afya na miundombinu?
Ningekuwa mimi ndo JK, ningesubiri hela yote hiyo ichangwe, kisha natangaza ghafla kwamba hakutakuwa na kampeni, hela zote zinatumika kupeleka maji, au kujenga dispensari vijijini!
NINA HAKIKA 100% KWAMBA CHAMA CHANGU KINGECHAGULIWA BILA KUPINGWA NA RAIA YEYOTE...Unaonaje?

They just want to justify dirty monies from somewhere.... mie naona watz tunapigwa changa la macho lakini CAG yupo atatuarifu baadaye
Shule nyingi za serikali hata vyoo hazina na kuna shule nyingi ukipita unakuta choo cha watoto kimeandikwa "choo hiki kimejengwa kwa msaada wa walipa kodi wa Japan". Unafikiri fedha za kufanya hayo hazipo? Fedha zipo; wanagawana hawa watu na vizazi vyao na marafiki zao. Fundraising kama hizo wakizifanya kwa ajili ya kujenga madarasa, kuweka madawati, kujenga vyoo vya shule, n.k. tutawauliza; na fedha za kodi mmeweka wapi?
Hapa wana kisingizio cha kusema hawaruhusiwi kuchota kwenye mifuko ya kodi. Ingawa fedha itakuwa hiyo hiyo ila itazunguka tu kwa kutumia mlango wa nyuma. Hakuna watanzania walioko tayari kuichangia CCM bilioni arobaini isipokuwa wale walio sehemu ya uozo unaofanywa na CCM. Hawa watachota huko kwa posho za mara mbili mbili, safari na semina uchwara, malipo kwa kazi hewa, n.k. halafu watazihamishia kwenye mfuko wa kampeni kwa madai kuwa wamechangia.
Halafu nani ata audit nani amechangia nini? Kuna wale ambao wakichangia wanataka wajulikane ili mkuuu wa nchi awaone kuwa wamechangia. Hawa hawawezi kutumia utaratibu huu ambao hauwapi fulsa ya kuonekana wametoa ngapi! Kwa hiyo njia pekee ya kuzipata fedha hizo ni kwa kundi lile linalokula Maposho parallel kutunga vikao na kulipana hayo maposho na hizo fedha kuzunguka na kuingia kwenye mfuko huo wa kampeni.
Lets be critical for a minute..tuache kuchonga kaa wanasiasa.
Hivi unaezaje kupinga kuchangishana hela ya kampeni wakati unakubaliana na mfumo wa siasa uliopo.
This is open contradiction to me.
Nani anaekubaliana nao?...Ni kwamba ndo uliopo...labda kwasasa tuseme kwa kifupi kabisa kuwa ni "'whether we like or not"...Of course kuna mawazo mbadala bana...kuna CCJ!
Good strategy!
Wanajua wasipochangisha hela za kampeni,mtasema wamewaibia tena kutoka benki kuu yenu.