Matumaini Ya Kuiondoa CCM 2015 yanazidi Kupotea

Matumaini Ya Kuiondoa CCM 2015 yanazidi Kupotea

Mkuu wewe ulikua umejiandaa kuona ccm inatoka mwakan kwa taarifa yako ccm itasherekea miaka 100 ya kutawala
 
CCM haiwezi kutoka madarakani leo, kesho wala keshokutwa, wala hakuna sababu ya CCM kutoka madarakani.
 
Unasema CCM itarudi madarakani. Kwani ilitoka??
 
Matumaini ya kuing'oa CCM madarakani yanazidi kupungua kwakuwa CCM wamewapatia Wananchi MAISHA BORA waliyowaahidi au? Maji, Umeme, Barabara, Elimu bora vyote vimeboreshwa vinapatikana ndani ya CCM? Wafanyakazi wanalipwa mishahara minono ama hadaa inaendelea kwao? CCM wame review Mikataba ya Kifisadi waliyoingia Kwenye Madini, na sekta ya nishati? Wanyama wetu wameacha kuuawa na kusafirishwa hovyo? ... CCM wameacha mauaji kwa raia wasiokuwa na hatia kwenye maeneo yenye migodi ya dhahabu?.... Thamani ya shilling imeimarika uchumi umekua?... CCM wananini cha kuwaambia Watanzania baada ya miaka 55 ya uhuru? ... Billion 400 za Ufisadi wa IPTL? Trillions za USwiss? .... Please achene dhihaka kwa Watanzania... watu wanashida, maisha ni magumu kuliko mnavyofikiri na kujamba humu jamvini ...
Mwaka 2010 Watanzania Wengi Tulianza Kujipa Moyo Sasa Ni Muda Wa Kuondoka CCM Madarakani, Kutokana Na Mhamko Wa Wakati Huo Hasa CHADEMA NA MGOMBEA WAKE WA URAIS DR Slaa Walipotikisa Ngome Za CCM. Wengi Tuliamka Kutoka Usingizini. Lakini Sasa Matumaini Yameanza Kupotea Na Uwezokano Wa CCM Kurudi Madalakani Sasa Ni Mkubwa, Hii Ni Kutokana Na Vyama Vyetu Vya Upinzani Kwa Sasa Havieleweki. Kwangu Mimi UKAWA Sina Hakika Kama Itadumu Mpaka Mwakani Kwani Upepo Umeanza Kuonyesha Hivyo. KUTOKANA NA MAZINGIRA YANAVYOONYESHA NA HALI YA SIASA ILIVYO CCM MWAKANI LAZIMA WASHINDE KWA HILO NASIKITIKA KAMA MWANAMABADILIKO. HUO NDIO UKWELI AMBAO HATUTAKI KUUSEMA.
 
Kila kitu kinawezekana. Kuing'oa ccm madarakani inawezekana kinachohitajika ni mikakati na kukijenga chama kwa haraka hasa maeneo ya vijijini ambako ndo ngome ya ccm. Tunafahamu fika kwamba umasikini wetu ni mpango wa ccm ili tuendelee kuwachagua. Wanachokifanya ccm ni kutekelekeza ahadi nusunusu ili wakija kampeni zingine waseme mutuchague ili tumalizie ahadi zetu.

Kama wapinzani wataanda mikakati mizuri kuiondoa ccm madarakani inawezekana kabisa.
 
zikiwa serikali 3 lazima 1 ccm waachie lakini 2
upinzani wasahau ndio maana ukawa wanajitahidi
wapate angalau hata 1...
 
Matumaini ya kuing'oa CCM madarakani yanazidi kupungua kwakuwa CCM wamewapatia Wananchi MAISHA BORA waliyowaahidi au? Maji, Umeme, Barabara, Elimu bora vyote vimeboreshwa vinapatikana ndani ya CCM? Wafanyakazi wanalipwa mishahara minono ama hadaa inaendelea kwao? CCM wame review Mikataba ya Kifisadi waliyoingia Kwenye Madini, na sekta ya nishati? Wanyama wetu wameacha kuuawa na kusafirishwa hovyo? ... CCM wameacha mauaji kwa raia wasiokuwa na hatia kwenye maeneo yenye migodi ya dhahabu?.... Thamani ya shilling imeimarika uchumi umekua?... CCM wananini cha kuwaambia Watanzania baada ya miaka 55 ya uhuru? ... Billion 400 za Ufisadi wa IPTL? Trillions za USwiss? .... Please achene dhihaka kwa Watanzania... watu wanashida, maisha ni magumu kuliko mnavyofikiri na kujamba humu jamvini ...

Mkuu,usitegemee Kupata Majibu Ya Maana Kwa Hawa Mabuku 7 zaidi ya kutokwa mapovu tu!
 
mkuu acha unafiki chukua themometer au joto.read pima nguvu ya chadema kisiasa 2010 na sasa kuelekea 2015.

CDM ni imara zaidi kwa sasa kuliko wakati wowote ule,mbinu za mapambano zimebadilika na hii CDM NI MSINGI ndio kaburi la ccm
 
Back
Top Bottom