Matukio yetu kupitia nyota zetu 12.

Maalim Jumar

JF-Expert Member
Dec 28, 2010
1,246
1,250
Habari zenu.

Mtabiri: Maalim Abalhasan Jumar.

Facebook: Mtabiri wa nyota na tiba.

Youtube: MAALIM ABALHASAN

Hotline:
+255 713 351 781.

Whatsapp pia.

Email: maalimjumar@gmail.com

MATUKIO YA NYOTA ZETU.

LEO 25.09.2021 MPAKA 20.10.2021.

====☆☆☆☆====

KONDOO. (21 Machi - 20 Aprili).
Kipindi hiki unayo nafasi ya kutimiza malengo yako.
Yatatimia ikiwa huna MIKOSI.
Utagombana na watu hasa kwenye mapenzi na biashara au kazini.
Utapata msiba au taarifa za misiba ya watoto zaidi ya marafiki.
Utakimbiwa.
Utaibiwa mali au vitu vyako.
Utapata wito mbali mbali.
Wanao kudai walipwe japo kidogo kidogo.
Namba ya bahati ni 83.

NG'OMBE. ( 21 Aprili - 20 Mei).
Kipindi hiki utapoteza vitu vingi.
Mambo unayotaraji kupata hautoyapata.
Ahadi nyingi havitotimia.
Utagombana na watu wengi.
Utatengana na jamii yako.
Namba ya bahati ni 75.

MAPACHA. ( 21 Mei - 21 Juni).
Kipindi hiki utakumbushwa zaidi kuhusu madeni unayo Daiwa.
Unayo nafasi kubwa ya kusikizwa haja zako.
Utapata mipango ya safari za mbali.
Uwe makini katika ndoto za sasa ili uzifahamu maana zake.
Utapata nafasi za kuongeza maarifa ikiwa upo tayari.
Namba ya bahati ni 19.

KAA. ( 22 Juni - 22 Julai).
Ni kipindi utapata heshima.
Haja zako mbali mbali zitatekelezwa. Hasa ikiwa huna MIKOSI.
Utaandamwa na vipingamizi mbali mbali na mashauri mbali mbali ( Kesi). Shughuli zako mbali mbali ni wakati wa kuzitafuta utatuzi halisi.
Namba ya bahati ni 11.

SIMBA. ( 23 Julai - 22 Agosti).
Ni kipindi cha neema.
Utapata mialiko mingi.
Utaongeza marafiki wengi.
Utapokea misaada zaidi.
Wingi wa misaada na mafanikio itategemea usafi wa mwili ( Bahati ulio nazo). Ni wakati mzuri kwako kupangilia mafanikio itayokua nayo.
Namba ya bahati ni 12.

MASHUKE. ( 23 Agosti - 22 Sept).
Kipindi hiki Utaandamwa MIKOSI.
Utaibiwa zaidi.
Utaugua mara kwa mara.
Utaongeza wasi wasi kwa kila jambo.
Duaa zinahitaji ka mara kwa mara ili kuepusha hayo.
Namba ya bahati ni 40.

MIZANI. (23 Sept - 23 Okt )
Kipindi hiki utaepuka matatizo mbali mbali.
Hasa ikiwa huna MIKOSI.
Unayo nafasi ya kufurahia maisha.
Ni wakati wa kuangalia afya yako pia.
Mambo mengi yanayo kuhusu sasa yatajitokeza.
Jikague mwenyewe zaidi.
Mambo mengine uwe makini nayo hasa ya kipato.
Namba ya bahati ni 32.

NGE. ( 24 Okt - 22 Nov).
Kipindi hiki utapata misaada mbali mbali kuhusu mali.
Migogoro kuhusu akina mama itajitokeza zaidi kwenu akina baba.
Vitu vingi vitabadilika kwako.
Wasaidieni wote wataohitaji misaada kutoka kwako kiasi ya uwezo ulio nao.
Ni wakati wa kupata nafasi kwenye sehemu ya kazi/shughuli zako.
Namba ya bahati ni 24.

MSHALE. (23 Nov - 21 Dis).
Ni kipindi cha kuwa nao wakwe zako kwa mlio oa.
Ni wakati wa kusaidia ndugu zako kwa kiasi ya uwezo ulio nao.
Hautopata utulivu.
Uwe makini na taarifa zote utakazopewa.
Utaibiwa vitu vyako. Tamaa zitaongezeka uwe mwangalifu humo.
Namba ya bahati ni 34.

MBUZI. ( 22 Dis - 20 Jan).
Ni kipindi cha kuwasaidia wazazi kiasi ya uwezo ulio nao.
Kagua mali au vitu vyako mahali ulipo.
Siri nyingi za hitajika kusitiriwa uwezavyo.
Utaugua mara kwa mara.
Utaibiwa mali au vitu vyako Ila unayo nafasi ya kuipata.
Namba ya bahati ni 53.

NDOO. ( 21 Jan - 19 Feb).
Ni kipindi cha kupata raha.
Utapokea zawadi nyingi na taarifa nzuri nzuri.
Utaongeza harakat I za hapa na pale.
Uwe makini ni wakati wa Kusingiziwa tuhuma nzito katika mapendo yako.
Wale mliopata mirathi za wazazi wenu Muwe makini katika mali hizo.
Namba ya bahati ni 45.

SAMAKI. (20 Feb - 20 Machi).
Ni kipindi cha kuugua zaidi.
Utaibiwa na kuharibikiwa zaidi. Unakavyotaraji kupata hutovipata.
Utavyopenda kutimiza havitotimia. Utakimbia. Muwe makini na ajali zitakazojitokeza za moto ( kuunguliwa) au kubomolewa.
Namba za bahati ni 73.

÷÷÷÷☆☆☆☆÷÷÷÷

KARIBUNI WOTE.

♡Ahsanteni wote.
 

Satoh Hirosh

JF-Expert Member
Mar 30, 2021
945
1,000
Nyota yangu ni mbuzi,tarehe ya kuzaliwa 19 january,jina J

Hapo kwenye kuibiwa sasa ndy pagumu nitaanza kuingia Lindo la kukesha usiku na mchana..kuibiwa kunauma sn

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom