Matukio yaliyoniacha mbavu zikiuma Mgodini Bulyanhulu

Ng'wanapagi

JF-Expert Member
Sep 18, 2013
9,125
8,644
Naamu kila binadamu unapokuwa umetulia na kukumbuka maisha uliyopitia basi lazima utakumbuka matukio yakufurahisha na muda mwingine ya kuhuzunisha. Leo nawaletea matukio mawili ya kweli na yaliyonichekesha na kunifanya binadamu niwe makini nao kwa kudaganya.
TUKIO LA KWANZA
Hili lilihusu mfanyakazi mwezetu kukutwa amelala, moja ya makosa makubwa ya kukufukuzisha kazi mgodini ni kukutwa umelala. Jamaa yetu huyu akiwa amepangiwa kazi ya ku scrape blasted materials (ores) alikuta mashine imeharibika (Srusher machine) akatoa ripoti na baada ya kusubiri mafundi waje kwa masaa kadhaa akaamua kulala, mara kaburu mmoja akiwa ameongozana na wasaidizi wake (Watanzania) yeye akashuka kuelekea eneo la mashine kama ilivyoripotiwa. Kufika akamkuta jamaa anakoroma, bahati mbaya Kaburu hakuwa na camera ambazo huzitumia kama ushahidi. Jamaa alipostuka akainuka na kukutana uso kwa uso na Kaburu. Ili kujiokoa na kufukuzwa akaanza kupiga yowe..... ananibakaaa ananibakaaa!!! Kaburu akarudi kwetu kuuliza anasemaje!? Tukamwambia anasema ..You wanted to rape him,kumbuka raia wa nje akituhumiwa kosa kubwa huwa wanapewa masaa 24 kuwa nje na mipaka ya Tanzania. Basi kaburu aliomba asamehewe (japo hakufanya hivyo) na akamsihi yaishie huko huko chini (underground). Alipoondoka huku alituacha mbavu hatuna.

TUKIO LA PILI
Ni night shift nyingine wakati tunasubiri kuletewa vifaa vya ku support blasted area (eneo lililolipuliwa) jamaa yetu akaingia chocho na kukaa sehemu akalala. Mara baada ya muda tukaona mwanga wa tochi ukielekea upande wetu, kutokana na aina ya mavazi wanayovaa ma miner (yana reflector) akamuona jamaa yetu akiwa amekaa na kujiinamia kwa usingizi. Mara Mzungu akageuza kuelekea kule alipo kamanda!! Jamaa nayeye akagutuka na kufahamu kuwa huyo si mgeni salama hasa alipoona gari imepaki upande wetu. Jamaa akainuka taratibu na kupiga magoti akifanya ishara ya msalaba kama vile alikuwa anasali . Mzungu akaishia kusema, Oooohh sorry you can go on.
 
Hahahhahaaaaa...dah huyu wa kwanza na mbinu zake za kubakwa ni kiboko

Nkoi Ngw'ana'paagi otale ole'South?
 
Hahahhahaaaaa...dah huyu wa kwanza na mbinu zake za kubakwa ni kiboko

Nkoi Ngw'ana'paagi otale ole'South?
Kaburu alichanganyikiwa na hakika jamaa kama angekomaa lazima angefukuzwa nchini. Sheria za mgodini hazinaga rushwa wala kupindishwa
 
Ukichukua video na simu watajuaje?
Huwezi kupita nayo getini kutokana na mashine za ku detect walizofunga. Pia kuna baadhi tu ya watu wenye ruhusa ya kuingia na simu. NB: Sielewi kwa sasa kama wanaruhusu maana nishaacha hiyo kazi miaka kadhaa iliyopita
Pia picha nyingi unazoona ma miner wamepiga (nazungumzia mgodi wa Bulyanhulu) huwa wanaomba kupigwa na ma SAFETY OFFICER ambao hushuka chini na camera kupiga picha muhimu za sehemu wanayotaka kuifanyia kazi, kwa ajili ya kufundishia, pia kama ushahidi wa makosa ya wafanyakazi chini
 
Aahaaaaaaa...nimecheka sana, aiseee una kipaji pia cha kuchekesha ,kifanyie kazi mkuu.
Anyway asante lkn ni true story pia ni kweli ukikaa na mimi huwezi kujutia siku yako. Napenda ucheshi, story za maisha,ushauri na kukumbuka nilikotoka
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom