Matukio ya Derby: Kuruka ukuta uwanja wa Taifa

ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
2,113
3,485
Leo kuelekea derby ya simba na yanga, wazee wenzangu tukumbushane matukio ya uwanja wa taifa kipindi hicho cha 90's.

Nakumbuka miaka ile pesa ilikuwa ngumu kweli kweli na mapenzi ya kutazama kabumbu yalikuwa ya hali ya juu.

Basi tulikuwa tuna njia mbalimbali za kuingia uwanjani. Hapa ni ubabe wako tu. Walemavu walikuwa wanaingia free sasa wewe ni kuchonga mchongo tu kumtafuta mlemavu kisha unamsukuma na kibaskeli chake ukipita naye tu kwenye gate unaachana naye hapo umeshawin.

Hatua nyingine ni ya kuruka ukuta mzee baba ule ukuta ulikuwa mrefu sana hasa upande wa kaskazini ambako ndiko kulikua na main gate. Na muda wote huu ukuta ulikuwa ukilindwa na maaskari wenye umbwa na waliopanda farasi.

Hapo sasa ni timing tu. Unacheki noma ukiwa nje kama askari yuko mbali unaparamia ukuta, ukifika juu unacheki tena askari wa ndani wamekaaje. Ukipata mwanya unajiachia kama komando kipensi unatua chini na kutoka nduki mpaka kwenye majukwaa ambayo yalikuwa machumachuma tu unayapanda na kuyakalia kwa timing maana ukijitingisha tu utajikuta uko chini.

Same applied to uwanja wa Karume. Pale ukuta ulikuwa mfupi kwa hiyo hutumii nguvu nyingi kupanda. Kimbembe ilikuwa umbali kutoka kwenye ukuta mpaka uwanjani. Basi tulikuwa tunapanda tukiwa wengi halafu tunahesabu moja mpaka tatu.

Tunatimua mbio askari anashindwa amkamate nani. Ila atakaye nyakwa ndio askari watamalizia hasira zao zote. Atachezea rungu za ugoko mpaka hana hamu. Nimezimiss sana siku zile ambazo kijana kweli alikua strong si kama vijana wa sasa.
 
utakuwa ulikuwa lege lege ulishindwa kujituma kutafuta hela ya kiingilio?
Ukiwa legelege unasubiria mpaka dk za mwisho huko ambako kwenye magate maumbwa hufunguliwa na magate yanakuwa wazi ndio legelege wanaingia kushuhudia dakika za mwisho. Msemo huo tuliuita fungulia umbwa.
 
Back
Top Bottom