Matukio mashariki ya kati na ulofa ulioko tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matukio mashariki ya kati na ulofa ulioko tanzania

Discussion in 'International Forum' started by kamanzi, Mar 27, 2011.

 1. k

  kamanzi Member

  #1
  Mar 27, 2011
  Joined: Oct 28, 2007
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 15
  Hivi karibuni nimepata mshangao wa mwaka mara baada ya kuona matukio mawili yanayokinzana TAnzania. La kwanza ni llile ambapo Sheikh Mkuu (nimewaambia awali kuwa huyu nu chaguo la CCM) alipowaasa waislamu wote Tanzania kutoshiriki maandamano ambayo kwa mujibu wake yenye vurugu ya CHADEMA. Lakini haukupita muda, kundi la watu wanaojiita waislamu waliingia mtaani na kuandamana wakipinga "mauaji" yanayofanywa na nchi za magharibi dhidi ya "nchi ya kiislamu", Libya. MAtukio haya mawili yamenishtua kusema kweli.

  Nimeshtuka kwasababu wakati chaguo la CCM Mufti Simba anawashawishi watanzania wenye haki ya kudai maisha bora, hakusikika akipinga wananchi hao hao wakipigania maisha bora ya nchi ya Libya. Hivi kuna uzalendo kweli hapo? Lakini labda nieleze ni kwanini naona sasa watanzania tunaelekea kwenye ulofa sasa.

  Awali ya yote yanayotokea Libya hayahusikani na dini maana wapinzani na walio upande wa Ghadafi wengi wao ni waislamu. Kinachotokea ni mapigano yanayotokana na ukabila baina ya watu wa mashariki walio na makao yao makuu Tripoli na wale wa magharibi walio na makao yao makuu Benghazi. KWa maana hiyo kuuleta udini katika hili ni kuwa na ufahamu haba wa matukio ya kimataifa.

  La pili linalofanya mapigano haya yawepo na ndilo linaloniumiza zaidi kuhusu watanzania ni suala la kiuchumi. KWa wale wasiojua, sababu mojawapo iliyomfanya Ghadafi abaki madarakani kwa miaka 40 sasa ni uwezo wake wa kuwakumbuka wananchi wake japo kwa shingo upande. Kila mwezi, Ghadafi kwa kutumia pato la mafuta amekuwa akiwapa wananchi wake pato (social benefit) la dola za kimarekani 2,000 wawe wanafanya kazi au la. KWa level ya kitanzania iyo ni pesa kubwa mno. Ila kwa kifupi ni kwamba wananchi wameanza kufunguka na kutaka zaidi maana anachobaki nacho Ghadafi na familia yake achilia mbali kabila lake ni kubwa mno. Kinachoniuma hapa ni kwamba, wale wanaopewa dola 2,000 kwa mwezi hata wakiwa hawana kazi wanaandamana na kutafuta haki yao zaidi. Lakini waislamu wenzao ambao pamoja na kuwa nchi yao ina kila aina ya madini ikiwa na yale yasiyopatikana kokote kule duniani (Tanzanite), wanakatazwa kuandamana sio wakiomba pato zaidi bali wakitaka bei ya sukari ipunguzwe.

  NAjiuliza hivi watanzania ni malofa kiasi gani? Dola 2,000 wanaopewa walibya walio jobless kwetu ni mshahara wa profesa mlimani. LAkini bado watu wakilalama wanakuwa wapinzani, waharibu amanai na kadhalika. Kuna akili ipi katika haya yote tukijua ya kuwa nchi yetu ina utajiri wa kupitiliza wa mali asili? Niliwahi kuwapa takwimu hapa kwamba japo ng'ombe wote waliopo Botswana ni wachache kuliko wale walioko katika mkoa wa Shinyanga peke yake, bado pato la beef Botswana ni kubwa kuliko mapato yetu ya madini yote ukijumlisha na pato linalopatikana katika utalii. Hivi tumelogwa?

  Jk mwanzilishi wa siasa za udini Tanzania majuzi tu alimwambia Magufuli atumie "utu na ubinadamu" katika bomoa bomoa. Hivi ni utu gani alioutumia kuidhinisha mkataba wa Richmond ambao kila mtu anajua Lowasa alikuwa ni fall guy tu? Au ubinadamu gani aliutumia kupitisha mkataba wa DOWANS? Utu upi aliutumia kutaka kuharakisha malipo ya bilioni 94 ya dowans? Pengine upo utu pale ambapo katika karne ya 21 DAr es Salaam mji mkubwa kuliko yote kiuchumi TAnzania hauwezi kuwapa wakazi wake maji safi na umeme wa uhakika. Kama hayo yapo DAr, huko Nanjilinji kukoje?

  BAdo ninawaasa waislamu ambao wengine ni marafiki zangu wakubwa tukiokuwa pamoja tangu utoto na wengine tukahudhuria pamoja madrasa tukijifunza KHalifu, Bete n.k. JK na kundi lake la maharamia kama Rostam, Makamba, UVCCM na wengineo kama Mufti Simba hawana wema na nyie hata kidogo. Wangekuwa nalo lolote la msingi leo hii Tanzania ingekuwa na mahakama ya KAdhi kama Kenya nchi yenye waislamu wachache kuliko sie lakini hilo lipo kwenye katiba yao. PIa TAnzania ingeshajiunga na OIC tena muda mrefu. Umewahi kufikiria ni kwanini pamoja na safari za kila leo nje ya nchi za JK hadi leo hajapata muda wa kuwa Alhaji (kwenda hijja Mecca)? Ni kwasababu usilamu kwake sio issue. Issue ni matumbo yao na familia zao na watafanya lolote ikiwa ni pamoja na kutugawakiudini kukamilisha agenda zao.

  Waislamu wa Tunisia, Egypt, Libya, Yemen, Syria na Jordan wameshatufundisha kukataa ufisadi uliojificha kwenye udini. Tusipojifunza ushujaa wao si tu tunawaangusha watoto wetu na vizazi vijavyo bali tunageuka malofa. NAWAKILISHA!!!
   
 2. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #2
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Kamanzi,

  Hadithi ndeefu, haina kichwa wala miguu. Jee, unaweza kuandika kwa ufupi na kuelezea unachokusudia kwa kueleweka?
   
 3. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #3
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Mimi nimemuelewa. Tumia muda wako kidogo usome kila mstari. Mkuu, hujapitia misukosuko ya elimu ya juu? Unaweza kuwa na assignment kibao na test zinaendelea kutangazwa, lakini mtu unajipa muda fulani kwa siku walau kusoma something. Hii ni mistari michache sana, ungetulia usome ungeelewa.
   
 4. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #4
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  Kuuliza si ujinga, wewe uliyeelewa habu tujuze umeelewa nini?
   
 5. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #5
  Mar 27, 2011
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  1. Sheikh alipinga maandamano aliyoyaita 'yanahatarisha amani', baada ya siku chache akayapokea maandamano mengine na kuamuru watu wawashambulie wanaopinga uisilamu!
  2. Sheikh aliyapinga maandamano (ya CHADEMA) ya kupinga hali ngumu ya maisha Tanzania, lakini akaumbuliwa na wa-Libya pale
  walipoandamana kuipinga serikali yao licha ya kwamba wana nafuu ya maisha kwa mbali ukinganisha na watanzania aliotuambia
  tusiipinge serikali yetu!
  3. Sheikh anatumia kigezo cha "Magharibi kushambulia uisilamu", lakini anasahau kwamba walioandamana Tunisia, Egypt, Libya, Yemen, Syria na Jordan majority ni waisilamu
   
 6. Xuma

  Xuma JF-Expert Member

  #6
  Mar 27, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 631
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  "asiyejua maana haambiwi maana"
   
 7. FaizaFoxy

  FaizaFoxy JF-Expert Member

  #7
  Mar 27, 2011
  Joined: Apr 13, 2011
  Messages: 58,107
  Likes Received: 22,163
  Trophy Points: 280
  1) Jee, kuna ulazima wa maandamano kama unaona hayana mantiki? Au mmoja akiamuwa watu waandamane ni lazima wote waunge mkono na kuandamana? "Sheikh" ana kila haki ya kupinga maandamano yanayoamriwa na "Padiri". Hususan maandamano yakiwa ya kushinikiza na kulilia madaraka baada ya kubwagwa vibaya kwenye kura za kidemokrasia.

  Kubwagwa vibaya ni kuwa hata robo ya kura za urais, robo ya viti vya ubunge, robo ya madiwani hujapata katika chama chako, halafu eti maandamano ya "maisha bora".

  2) Hiyo juu imejibu hoja yako namba moja na mbili.

  3) Mpenda haki yoyote duniani atapinga kuvamiwa nchi yoyote na raia zake kuuliwa. Kama hamumtaki kiongozi waachieni wenye nchi wafate taratibu zao na si kuwaingilia na kushambulia na kuua kwa uongo. Uongo kama uliotumika Iraq. Jee, ulishaona silaha za maangamizi za Iraq mpaka leo. Sheikh ana kila haki ya kupinga mauaji yanayofanywa na majeshi ya kikurusedi nawe una kila haki ya kutetea ukurusedi.
   
 8. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #8
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu mada yako nimeielewa sana na ninakupa pongezi kwa kutumia
  muda wako kwa uchambuzi wa mambo ingawa nimegundua mapungufu
  ambayo yanatokana na kutojua au ni kusimamia utetezi wa fikra za kidini...
  na hii inatokana na kutojua utofauti kati ya dunia ya kwanza,pili na tatu


  Kama utapata muda wa kufanya ziara za dunia hizi zote na ukizingatia
  dunia ya tatu unaijua fika basi ungepata fursa ya kujua ni kwanini waliiweka
  dunia katika madaraja haya matatu.....kwa fikra hadi nyanja za kimaendeleo
  na usingepata muda wa kuhoji ni kwanini watanzania si kama waarabu wa
  dunia ya pili na wa magharibi,amerika na mashariki ya mbali wa dunia ya kwanza.


  Kwa kusema hivi tunaposema sisi ni dunia ya tatu na ya mwisho tuna mantiki
  ya mwisho kwa nyanja zote yaani udini,fikra,maendeleo,ujinga,uwezo,nia,tija n.k
  na tuwe tunafanya utafiti na si kuwalaumu watu wetu na hata viongozi ambao
  wamezaliwa katika dunia hii hii ya tatu na ya mwisho.

  mada yenye tija ni ile iliyofanyiwa utafiti kwani tunataka tuelimishwe.......
   
 9. S

  Societa Jesuit JF-Expert Member

  #9
  Mar 27, 2011
  Joined: Feb 1, 2011
  Messages: 200
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0

  Mkuu sinkala hongera kwa uyakinifu wa hoja na hii inaonyesha kwa jinsi gani
  unatakiwa kuwa ''the great thinker'' kwa sisi tulio katika pango la giza.......
  na haya ndiyo matatizo yanayotupata dunia ya tatu na hasa kwa kauli zetu zina-
  zojipinga utadhani ni kwamba zimetolewa na watu wawili wenye itikadi tofauti za
  kifikra hadi unashangaa je,huyu mtu anayetoa hizi kauli kama angeishi dunia ya
  kwanza asingekuwa na ''psychological problems?''

  na hii ni kwasababu hatuna utamaduni wa kupima afya ya ya akili
  ili kujua kiwango cha taahira ya akili ya sisi wengi wa dunia ya tatu....thanks man.
   
 10. KYALOSANGI

  KYALOSANGI JF-Expert Member

  #10
  Mar 28, 2011
  Joined: Jan 21, 2011
  Messages: 1,901
  Likes Received: 473
  Trophy Points: 180
  Mungu wangu kama wewe huana uelewa wa mabo ,nenda kasome udaku ,yaani page moja iankusumbua kusoma umepita shule gani wewe!
   
 11. Mjanga

  Mjanga JF-Expert Member

  #11
  Mar 28, 2011
  Joined: Feb 13, 2011
  Messages: 1,246
  Likes Received: 79
  Trophy Points: 145
  Sasa watu gani ni "malofa"?? WATANZANIA wote AU Mufti Simba na baadhi ya Waislamu waliomuunga mkono??? jenga hoja yakinifu mkuu!!!
   
 12. chitambikwa

  chitambikwa JF-Expert Member

  #12
  Mar 28, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 3,940
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 135
  Kweli umasikini wa kichwa ni mbaya kuzidi hata *******
   
 13. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #13
  Mar 28, 2011
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  nimesoma thread moja kuwa Majimshindo ni 'kibaraka' jamvini, aangalie yasije yakamkuta kama ya Hizza Tambwe aliyeishia kuwauliza waandishi maswali baada ya kuwaita!
   
 14. nsimba

  nsimba JF-Expert Member

  #14
  Mar 28, 2011
  Joined: Oct 7, 2010
  Messages: 785
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  ushabiki unakusumbua, hUna hoja. You act as not a great thinker!!!
   
 15. M

  Mafie PM JF-Expert Member

  #15
  Mar 29, 2011
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 1,318
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 135
  Bondeni school Ars!
   
Loading...