Matokeo ya UBAGUZI

daniel_mollel

Member
Sep 30, 2011
67
16
Mwalimu Nyerere alipata kusema nanukuu "dhambi ya ubaguzi itawatafuna, ukimbagua mtu wa kwenu kwa sababu ya ulevi tu, ulevi wa madaraka, ukasema sisi ni sisi na wao ni wao, sisi, na wao!!, hamtabaki salama, kwa sababu mtagundua kwamba hata sisi siyo wamoja" akaendelea kusema, "ukishaanza kubagua watu wa kwenu, hautaacha ni sawa na kula nyama ya mtu" mwisho wa kunukuu;

Ubaguzi wa zamani hauzai matunda/watoto zamani, huchukua muda kutunga mimba, kuilea vyema na baadaye sana kuzaa katoto, kachanga katakachoonekana mbele ya watu wenye fikra changa kama kamezaliwa katoto kabla ya muda (premature), lakini kadiri kanavyokua watu hubaini kumbe hakakuwa katoto, ni jitu! watasema kale katoto kamekuwa jitu!! hivi ndivyo ilivyo kila mahali watu wanapobaguana kwa misingi ya haki na sheria matokeo yake ubaguzi ule huzaa jitu katili linaloitwa chuki mwana wa kiburi ambalo likimea vema hasababisha mkwamo na hatari kubwa kwa ustawi wa watu

Daniel E. Mollel
 
Back
Top Bottom