Matokeo ya mtihani kidato cfha nne [csee] yanatisha... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matokeo ya mtihani kidato cfha nne [csee] yanatisha...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bakari Maligwa, Jan 28, 2011.

 1. Bakari Maligwa

  Bakari Maligwa Member

  #1
  Jan 28, 2011
  Joined: Aug 18, 2010
  Messages: 65
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ...Nadhani ipo haja sasa kwa wapanga-sera na au wataalamu wa kada ya elimu na taaluma kuketi na kufanya uamuzi mgumu juu ya sera ya elimu Tanzania. Elimu ya Tanzania inakwenda segemnege na shelabela huku waliyesoma zamani wakibaki wakiduwaa! Matokeo ya kidato cha nne 2010 ni kielelezo tosha kwa jinsi sera na au mipango mibovu ilivyozaa asilmia 49.6 ya wanafunzi waliyofeli..na hata kufanya asilmia 80 ya watahiniwa wa 2010 kupata daraja la IV na SIFURI (0). Uchunguzi wangu wa haraka unaonesha kwamba sababu kubwa za kufeli kwa watahainiwa wengi ni:
  1. Ukosefu wa umadhubuti wa sera na mipango mikakati ya elimu ya Tanzania;
  2. Ukosefu wa wataalamu (walimu) wa kutosha kufundisha masomo maalumu na ya ziada;
  3. Ukosefu wa weledi kwa baadhi ya walimu wanaoajiriwa sasa (hususan wa vodafasta);
  4. Kukosekana kwa ari na moya wa kujitolea kwa walimu na wafanyakazi wengine katika sekta ya elimu nchini;
  5. Ukosefu wa dhana za kufundishia na au vifaa vya kujifunzia;
  6. Ukosefu na au upungufu wa vitabu vya kiada na au ziada kwa shule nyingi za serikali;
  7. Ukosefu wa maabara na vifaa vya sayansi (kemia, elimu ya viumbe na fizikia) kwa shule nyingi za serikali;
  8. Shule za kata kuendeshwa kisiasa badala ya utaalam na ualimu;
  9. Wanafunzi kukosa juhudi, nmaarifa na nidhamu ya kujifunza na kufundishika;
  10. Mahusiano mabovu baina ya ushirikiano pande-tatu (waalimu + wazazi + wanafunzi); na
  11. Serikali kushindwa kuwekeza kwenye rasilimali watu wa kutosha wenye tija na maslahi mazuri ya mishahara na mazingira mazuri ya kufundishia.
  Mambo kumi na moja yaliyoorodheshwa hapo juu yanaufanya MCHAKATO WA UTOWAJI WA ELIMU kwenye shule nyingi za serikali (kata - za wananchi na zile maalumu) kuwa wa zimamoto na kupelekea kukosekana kwa mujtamaa murua wa maendeleo ya sekta ya elimu.

  USHAURI:
  • serikali iache siasa kwenye taaluma
  • serikali ichukue hatua za makusudi kurekebisha hali hii kinyume chake miaka ijayo, yaani, 2011 hadi 2015 tutashuhudia wimbi kubwa la wahitimu kufeli mitihani ya kidato cha nne na hata cha sita na vyuo kadhalika
  • serikali ichukue hatua za makusudi kuanzisha mfumo mpya wa kuchuja wanafunzi wanaotakiwa kuingia sekondari na kuachana na mfumo wa sasa wa kila mwanafunzi lazima asome sekondari
  • serikali iboreshe maslahi ya waalim na ijenge mazingira mazuri ya kufundishia
  • wanafunzi wajengewe misingi ya maarifa, ari na nidhamu juu ya mchakato wa elimu
  Pamoja kuna mengi yanayotakiwa kufanya na serikali umefika wakati sasa kwa wananchi (wazazi na walezi) kuchukuwa dhima yao kama washiriki muhimu katika ushirikiano pembe-tatu ili kuboresha mazingira ya ufundishaji na kujifunza.

  TAHADHARI: TUSIPOZIBA UFA TUTAJENGA UKUTA!
   
 2. k

  kikule Senior Member

  #2
  Jan 28, 2011
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 184
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  MKUBWA UMENENA LAKINI HUJATAJA MGOMO BARIDI WA WALIMU AMBAO HAUWEZI KUISHA UNLESS WALIMU WANALIPWA MADAI YAO KABLA HAIJALIPWA DOWANS.INASHANGAZA KUWA SERIKALI INATHAMINI DOWANS KULIKO WALIMU AU MPAKA TUPELEKE MADAI YETU ICC?:twitch:
   
 3. Seto

  Seto JF-Expert Member

  #3
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 961
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  ASANTE KWA LOWASA NA JK KWA SHULE ZAO VIVULI, MAANA ZIMETUZALISHIA ZERO ZA KUTOSHA,,,,:clap2: FOR THEM..
   
 4. N

  Ngonini JF-Expert Member

  #4
  Jan 28, 2011
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 2,024
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Na bado vilaza wa chuo kikuu cha kata mtaanza kuwaona maofisini na mitaani! Tangu lini mkwere akajua umuhimu wa elimu!
   
 5. KiJo

  KiJo Member

  #5
  Jan 28, 2011
  Joined: Jan 19, 2011
  Messages: 46
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  • Viongozi wetu wanalipuzia hili swala sana wakijua watanzania wakipata elimu wanaweza kujiendesha wenyewe na kuiba itakua shughuli meaning watafunguka macho na ndio maana wanakula wakijua watanzania bado ni wajinga hawajajielewa, hili linanawezekana kua pia ni shindikizo la nchi za nje wakitoa misaada ili kujinufaisha na rasilimali zetu.
  • Most of the Tanzanians hatujui wht education means kwa kweli, kinachoeleweka ni kuingia darasani kusoma ili kufaulu mitihani lakini maana yake halisi bado ni kitendawili for most of us, ndio maana mtu anaweza akawa na masters mpk phd but he can't solve a simple problem that requires a normal thinking like an educated person mostly viongozi wetu thus y tunajikuta tunaingia kwenye matatizo na mikataba mibovu kutokana na mamuzi yakishenzi.... Albert Einsten alidefine education as "Education is what remains after one has forgotten everything he learned in school."
   
 6. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #6
  Jan 28, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Hapa bongo as long as watoto wa hao watunga sera hawatumii hizi shule bado shule zetu zitakuwa na tija ndogo kwa vijana wetu wakati watoto wao wakisoma kwenye academy zenye kila huduma muhimu kwa mwanafunzi kusoma no matter how good hizo sera zilivyo.
   
 7. G

  George Jinasa JF-Expert Member

  #7
  Feb 5, 2011
  Joined: Sep 14, 2010
  Messages: 393
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Tatizo kubwa naloliona mimi ni mgogoro kati ya mabadiliko na maandalizi. Kwa muda mrefu hapa Tanzania, toka enzi za mkoloni, elimu yetu ilichukua umbo la paramidi. Idadi ya wanafunzi waliokuwa wanaanza elimu ya chini kabisa (msingi) ilikuwa ni kubwa, ilipungua sana katika kiwango cha sekondari na ikapungua isivyoelezeka katika kiwango cha elimu ya juu. Kwa mfano, kama watu laki mbili waliaanza shule ya msingi, sekondari wangeweza kwenda 20,000 ambao ni asilimia 10 na chuo kikuu wangeenda 2,000 ambao ni asilimia mbili. Hali hiyo ilibaki kwa muda mrefu hata baada ya uhuru. Serikali ilichofanya zaidi ni kuongeza idadi ya wanafunzi wanaopata elimu ya msingi na kuifanya elimu hiyo kuwa ya lazima kwa wote.

  Wakati mikakati ya kufanya elimu ya msingi kuwa ya wote mgogoro kati ya mabadiliko na maandalizi tulikumbana nayo. Utakumbuka kwamba kutokana na idadi ya waalimu kuwa wachache sana ukilinganisha na wanafunzi, serikali, katika miaka ya sabini na themanini ilianzisha utaratibu wa kuwatumia wanafunzi waliomaliza darasa la saba kufundisha shule ya msingi katika mtindo unaofanana na huu wa vodafasta. Lengo lilikuwa ni kuwaendeleza waalimu hawa wa upe (vodafasta) ili pamoja na wanafunzi wengine waliokuwa katika vyuo vya ualimu waongeze idadi ya walimu na hatimaye kukabiliana na uhaba wa walimu. Tatizo la matokea mabaya katika shule za msingi katika kipindi cha mwanzo lilikuwa kubwa japo taarifu za kiuchambuzi wa matokeo zilikuwa duni wakati huo,

  Mpaka miaka ya mwanzo ya 90 wakati tunaingia mfumo wa ubepari na vyama vingi, shule za sekondari zilikuwa chache sana na wanafunzi waliokuwa wanapata nafasi ya kuingia sekondari walikuwa wachache sana tena wenye akili zaidi ya za kufundishwa shule. Utaona kwamba asilimia chache ya watu waliofaulu mtihani wa darasa la saba walipata nafasi ya kuingia sekondari. Vyuo Vikuu wakati huo vilikuwa viwili tu Tanzania nzima: Chuo Kikuu cha DSM ambacho kilikuwa karibu na fani zote mhimu na Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine ambacho kilichikita katika fani za kilimo. Nafasi za wanafunzi katika vyuo hivi zilikuwa chache sana. Fani kama sheria, udakitari, injinia na biashara kwa mfano hazikuweza kusajili wanafunzi zaidi ya mia moja kwa mwaka. Wanafunzi kama hao ambao walikuwa wanachujwa kama chai usingetegemea sana kuwa na idadi kubwa ya wanao feli. Kama mwanafunzi mwenye kiwango cha chini kabisa katika kitivo cha sheria ilikuwa daraja la kwanza points 7, unatarajia wangapi watashindwa kufaulu vizuri mitihani yao?

  Hivi karibuni serikali imekuwa katika mchaka mchaka kuongeza idadi ya wasomi katika hatua za elimu ya sekondari na vyuo vya juu. Mashule ya kata yamejengwa kwa wingi bila kuwa na uwiano wa walimu na nyenzo za kufundishia. Vyuo Vikuu vingi vya binafsi na umma vimejengwa kwa mtindo huo huo. Wakati yote hayo yanafanyika hamna maandalizi ya kutosha yaliyofanyika kwa upande wa idadi ya walimu na vitendea kazi pamoja na namna ya kudhibiti matokeo. Tatizo kama hili lililojitokeza katika matokeo ya kidato cha nne linaweza kuwa kubwa katika vyuo vikuu, ila linajificha kutokana na ukweli kwamba matokeo ya vyuo vikuu yanatolewa na vyuo vyenyewe. Sasa kwa vyuo vikuu vya binafsi vinavyotoa huduma na kufanya biashara vinaweza kuanika mapungufu yao kiurahisi namna hiyo?

  Mimi naona ipo haja kuangalia uwiano kati ya mabadiliko na maandalizi vinginevyo tunaweza kujikuta tunarudi nyuma badala ya kwenda mbele. Kwa upande wa elimu ya sekondari yafutayo yafanyike mara moja

  1. Utaratibu wa kutathimini uwezo wa wanafunzi kuingia kidato cha tatu urudishwe. Mwanafunzi anayeshindwa kupata alama ya D katika mtihani wa kidato cha pili itakuwa ni miujiza kufaulu mitihani ya kidato cha nne.

  2. Serikali iboreshe zaidi mishahara ya walimu katika shule za serikali na kuwekeza katika nyenzo za kufundishia.

  3. Serikali iwekeze zaidi katika vyuo vya ufundi wa vitendo na biashara ili wale wasio na vipaji vya kusoma lakini wana vipaji vya ufundi na mambo mengine wasipoteze muda wao katika masekondari ya kawaida bali wajiendeleze zaidi katika ufundi.

  4. Suala la elimu lisipewe sura ya kisiasa bali lichukuliwe kama suala la kitaalamu na liendeshwe kwa kitaaluma.

  5. Wasomi wa Tanzania tuache kuvaa sura ya kulaumu tu bali tujione tunajukumu la kuchangia maendeleo ya elimu kama waliotutangulia walivyochangia. Utakuta DR au Pr wa Chuo Kukuu kila siku yuko kwenye vyombo vya habari anakejeli matokeo ya sekondari wakati yeye mwenyewe hajawahi kuandika hata kitabu kimoja cha chuo au sekondari. Lawama zake bila kutoa ushauri wa tiba ni kushabikia matatizo.

  6. Taratibu zifanyike kubadilisha mitaala ya elimu na mbinu za kutaini. Elimu yetu bado ina sura ya elimu ya mkoloni. Tunasoma kwaajili ya kuajiliwa (kuunza nguvu na ujuzi) na sio kujitegemea. Ndio maana Prof wa elimu akiachishwa kazi katika taasisi ya elimu anakuwa kama samaki aliyetolewa baharini. Tukiwa na mfumo mzuri wa elimu ya kujitegemea wasomi wetu watakuwa ni vyanzo vya ajira kwa wengine na sio vyanzo vya ushindani wa ajira katika soko la ajira.

  7. Mashule ya binafsi yadhibitiwe katika ada. Kuwa na shule za ada ya 3,000,000 na zingine 5,000 kunaweka matabaka makubwa kwa wanafunzi na walimu. Huyu anayelipa 3,000,000 atakuwa na huduma kumzidi huyu wa 5,000 kwa zaidi ya asilimia 1000. Wakati huo huo wote wanafanya mtihani mmoja. Huu unaweza kuwa ni ubaguzi wa aina fulani.
   
 8. A

  Alisule New Member

  #8
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Matokeo ya kidato cha nne yanatoka lini
   
 9. Mchaga 25

  Mchaga 25 JF-Expert Member

  #9
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 29, 2011
  Messages: 463
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  yameenda kuchapishwa sweden akirudi atakuja nayo
   
 10. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #10
  Jan 25, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Haahaahaaa! Huyu jamaa anafaa akachimbe kokoto! Huu uzi sijui kauchimbua wapi! Maana heading yake nimekuja spidi na hasira mbaya... kumbe ni ya mchakachuo wa mwaka juzi.
   
 11. P

  Petu Hapa JF-Expert Member

  #11
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 2, 2008
  Messages: 714
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Kuanze kuwa na kautaratibu ya kutoa mokeo kwa jumla jumla. Atokee mdau, akusanye matokeo ya vyuo na aanza kuyalinganisha.

  VETA zipo lakini ziimarishwe zaidi - na hata uwekezaji binafsi unaweza kuwekwa kwenye maaeneo haya! Nimeona imeanza kwenye masekritari - na magereji, mafundi cherehani, wanafanya kazi za kufundishwa. Lakini sasa wakue zaidi


  Hili ni gumu kidogo. Labda ubadilishe mfumo mzima wa elimu, uondeke katika biashara. Kwa sasa elimu inanunuliwa
   
 12. k

  kastarehe JF-Expert Member

  #12
  Jan 25, 2012
  Joined: Jan 20, 2012
  Messages: 231
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umesahau usiache zile degree za KICHINA zilizoanzwa kuzalishwa na vyuo vyenye heshima UDSM, SUA, SAUT, etc. Degree za kichina zamani zilikuwa nadra na kama zilikuwepo zilikuwa marks chache za CHU@%%i kwa kinasister. Lakini siku hizi pochi, $%&chi vinanunua degree!!!!
   
 13. M

  Mnyakatari JF-Expert Member

  #13
  Jan 25, 2012
  Joined: Oct 25, 2010
  Messages: 1,557
  Likes Received: 488
  Trophy Points: 180
  Albert Einsten alidefine education as "Education is what remains after one has forgotten everything he learned in school."
  [/LIST][/QUOTE]
  Correction:Einstein alizungumzia knowledge sio education kama ulivyoquote.Knowledge differs greatly to knowledge.
   
Loading...