G Sam
JF-Expert Member
- Apr 20, 2013
- 11,596
- 36,018
Mamlaka ya dawa na chalula ya taifa (TFDA) imevifungia kwa muda sasa wa miezi zaidi ya mitano viwanda vyote vya dawa vinavyosambaza dawa za binadamu bohari kuu ya dawa (MSD) kutokana na sababu mbalimbali imefahamika.
Sababu kuu ya kufungia viwanda hivyo vyote na kuifanya bohari kuu ya dawa kukosa dawa kwa kipindi kirefu ni hatua ya viwanda hivyo kushindwa kuendana na hadhi ya kimataifa ya viwanda vya kuzalisha dawa za binadamu, imeelezwa.
Hata hivyo uchunguzi unaonyesha kuwa TFDA kufungia viwanda hivyo ni kutokana na kujaa woga wa kuwajibishwa kwa watendaji wake kama ilivyo tafsiri ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na John Pombe Magufuli ambayo inaonekana kuwa na msimamo mkali. Awali viwanda hivyo vilikuwa vikifanya kazi kama kawaida chini ya tawala zote za awamu nne zilizotangulia.
Wakati hayo yakijiri MSD nayo imerudisha dawa zote kutoka mikoani ambazo zilisambazwa kwa takribani mwaka mmoja na nusu uliopita kwa kile walichooleza kuwa dawa hizo zina kasoro mbalimbali ikiwemo upungufu wa dawa katika makopo.
MSD wameirudisha dawa hizo na kuwakabidhi wazalishaji kinyume kabisa cha taratibu kutokana na madai tu ya upungufu ambapo ingewezekana kwa wadau kuketi chini na kukubaliana kufidia upungufu huo.
Madhara hayo yamesababisha dawa hizo kufikia muda wa kuharibika (expired date) na hivyo kukosa uhalali wa kutumiwa na binadamu. Hivyo basi dawa hizo zinatakiwa kuharibiwa na kuteketezwa ambapo inakadiriwa kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 11 za kitanzania.
Aidha uchunguzi wetu umebaini kuwa dawa hizo hazikuwahi kusambazwa na MSD katika mikoa mbalimbali bali bohari hiyo kuu ya dawa ilizishikilia kutokana na kile kinachoonekana madai yao kutoka serikalini kutokutimizwa. Baada ya muda kuisha ndipo MSD wakatunga mbinu kujiokoa na hili na ndipo wakayatafuta madhaifu ya viwanda ambavyo viliwasambazia dawa kwa tenda na kuwashika uchawi.
Kutokana na hatua hizo za TFDA na MSD, serikali pamoja na taifa vimepata hasara ya zaidi ya Tshs bilioni 20 pamoja na dawa kukosekana hospitali mbalimbali hivyo kugharimu maisha ya watu.