Benson Mramba
JF-Expert Member
- Oct 29, 2013
- 644
- 1,482
Binafsi nimeshtushwa sana na matokeo ya kura za maoni za CCM kuanzia Udiwani wa Kata hadi Ubunge. Kwa ujumla ni kuwa kila ambalo Mwenyekiti (Rais) aliloonyesha kulitaka au kulitamani Wajumbe wamelipinga kwa nguvu.
1. Wanachama wote wa vyama vya upinzani ambao hawana asili na CCM wameshindwa kura za maoni.
2. WanaCCM wengi ambao Rais amekuwa akionyesha kuwaunga mkono wameshindwa vibaya Mfano Makonda na Mwakyembe
3. WanaCCM ambao Rais ameonyesha kuwakosoa na kuwaponda hadharani wameshinda kwa kishindo mfano Mrisho Gambo na Ndugulile.
Hizi ni salamu nzito kwamba Mwenyekiti anafikiria tofauti na viongozi wa Chini na Wanachama! Angalia Kinana alivyoshangiliwa Dodoma kwenye mkutano Mkuu!
Kinana anasema hakuna Uchaguzi rahisi kwasababu kura ziko kwenye mioyo ya watu! Sasa Rais awe makini na jinsi atavyowahandle wapinzani wake kwenye uchaguzi Mkuu maana wananchi wanahasira ya kukosa Bunge Live na kuzuiliwa kwa shughuli za kisiasa.
Kesho Lissu anarudi kama ni kweli! Busara aliyoitumia Kikwete kwa Lowassa kumpa nafasi bila kutumia polisi ndio kwa mtazamo wangu inapaswa kutumika kesho.
Lissu alindwe aachwe aropoke atakavyo asaidiwe afanye kampeni zake ajibiwe kwa hoja! Nguvu yoyote inaweza kuleta matokeo mabaya sana kwa Rais. Watanzania hawapendi watu wababe kwa washindani wao!