Matokeo ya Kura za Maoni CCM yanaonyesha kuwa Viongozi wa Chini wanapingana kimtazamo na Mwenyekiti wao Taifa

Mkuu Benson Mramba karibu nyumbani chadema...tugange yajayo mkuu...ccm ina wenyewe nadhani hata magufuri amejifunza kitu kupitia hzo kura za maoni
 
Benson Mramba, naona umejionea mwenyewe Ccm inawenyewe.
Mwisho hivi vyama vinaendeshwa na Binadamu wenye mapungufu kwahiyo tuvumiliane Kiongozi.

Nazani umeona makamanda waliounga juhudi walivyofanywa na kupotezwa kwenye Ramani ya siasa.
Rudi nyumbani. Upinzani ndiyo sehemu ya Vijana kutoka kirahisi kwenye siasa.
Mbowe anamapungufu kama ilivyo kwa Magufuli na ndiyo Ubinadamu wenyewe.

Benson kapewa za uso hawezi Rudi anaogopa aibu.
Ukitaka siasa za shibe nenda ccm ukitaka siasa za uhanarakati nenda upinzani
 
Uzi mrefu, lakini hofu yako ni pale ulipoona nyie wahamiaji wa ccm hamna mtu huko ccm anawakubali. Mbona hujaongelea rushwa iliyo nje nje, huku wanaccm wakimpaka rais mafuta kwa mgongo wa chupa kuwa kadhibiti rushwa?
 
Wajumbe wameipa ccm wakati mgumu sana, hawataki mabadiriko kabisa.
 
Wajumbe wameipa ccm wakati mgumu sana, hawataki mabadiriko kabisa.
Steve Nyerere kawapaka shombo wajumbe huyu dogo adhibitiwe, hivi mtu hujui mitaa ya jimboni kwako huna makazi huna mke huna kwenu watakuaminije? Msibani hujawahi onekana watakuchaguaje haka kapumbavu Steve Nyerere mkadhibiti mapema
 
Nae spana
Safi Sana wabunge wa hovyo hovyo wanaongea utumbo tupu waliolifanya bunge likose heshima na kudharaulika wajumbe Mungu awabariki kabisa.
Ukisimama na wananchi watasimama na wewe watawala ni wapitaji.
Kuna kiherehere mmoja kazini alikuwa na tabia ya kupeleka taarifa za wenzie kwa bosi,ikafika siku akagawa kadi ya mchango anataka kuoa wafanyakazi wakazichangamikia kadi yake imefika mda wa kurejesha kadi kachezea spana Kati ya wafanyakazi 140 Hakuna aliyechanga hata mmoja japo wote wanao uwezo.
Kuna bosi mmoja akamwambia unajua kwann awajachanga hawa "wafanyakazi wenzio ndio ndugu zako mabosi ni wapitaji.
Wajumbe heko wamesimama na wananchi, wahamiaji walidhani uchaguzi mkuu ni sawa na uchaguzi wa marudio.
 
Hahahaha Hahahaha hatar fayaaa nlikuambia mapema uachane na ccm inawenyewe huku nisikia ona Sasa
Inabidi ianzishwe kampeni ya back to the root
tapatalk_1595659759521.jpeg
 
Binafsi nimeshtushwa sana na matokeo ya kura za maoni za CCM kuanzia Udiwani wa Kata hadi Ubunge. Kwa ujumla ni kuwa kila ambalo Mwenyekiti (Rais) aliloonyesha kulitaka au kulitamani Wajumbe wamelipinga kwa nguvu.

1. Wanachama wote wa vyama vya upinzani ambao hawana asili na CCM wameshindwa kura za maoni.

2. WanaCCM wengi ambao Rais amekuwa akionyesha kuwaunga mkono wameshindwa vibaya Mfano Makonda na Mwakyembe

3. WanaCCM ambao Rais ameonyesha kuwakosoa na kuwaponda hadharani wameshinda kwa kishindo mfano Mrisho Gambo na Ndugulile.

Hizi ni salamu nzito kwamba Mwenyekiti anafikiria tofauti na viongozi wa Chini na Wanachama! Angalia Kinana alivyoshangiliwa Dodoma kwenye mkutano Mkuu!

Kinana anasema hakuna Uchaguzi rahisi kwasababu kura ziko kwenye mioyo ya watu! Sasa Rais awe makini na jinsi atavyowahandle wapinzani wake kwenye uchaguzi Mkuu maana wananchi wanahasira ya kukosa Bunge Live na kuzuiliwa kwa shughuli za kisiasa.

Kesho Lissu anarudi kama ni kweli! Busara aliyoitumia Kikwete kwa Lowassa kumpa nafasi bila kutumia polisi ndio kwa mtazamo wangu inapaswa kutumika kesho.

Lissu alindwe aachwe aropoke atakavyo asaidiwe afanye kampeni zake ajibiwe kwa hoja! Nguvu yoyote inaweza kuleta matokeo mabaya sana kwa Rais. Watanzania hawapendi watu wababe kwa washindani wao!

Nyerere aliwaambia polisi msimpige mabomu Mrema msiwazuie wafuasi wake kumsukuma na gari watamsukuma ikiingia jioni wataenda lala makwao, polisi walipofata ushauri wa Mwalimu na umaarufu wa Mrema ukafa Leo kaishia kuunga juhudi.
Polisi wanafanya kazi nzuri Sana ya kuwafitinisha wananchi na ccm wanapotumika kuwaumiza wapinzani
 
Walidanganywa eti upinzani utakufa wakawahi siti matokeo yake wamekufa wao.Kutoka kutia Nia Hadi kutia huruma.Wengine wanaomba msamaha kurudi walipopakashifu na kutukana.Hapa Ina maana kuunga juhudi je pana ukomo?
 
Ngombe waliokatwa mikia
 

Attachments

  • 4B758860-6DA0-4ED8-8AFE-D49D1C40B801.jpeg
    4B758860-6DA0-4ED8-8AFE-D49D1C40B801.jpeg
    181.6 KB · Views: 1
Nachojua point number 1 ndiyo imekuuma zaidi coz upo kundi la waliokwatwa mkia 🤣🤣🤣

By the way hongera Comrade i see jinamizi limeanza kukuachia leo umeweza kufungua thread inayohusu chama chako per se.
Kama Sauli wa kwenye biblia, LABDA nae anaanza kuona mwanga, yafaa tumuombee.
 
Back
Top Bottom