Elections 2010 MATOKEO ya kura za awali CCM August 1, 2010

Nasubiri matokeo kutoka Rungwe ya Prof. Mwandosya, maana nilimuonya rafiki yangu Steve Mwaka atulize boli kwanza asubiri 2015 kwa kuwa nina uhakika Prof hawezi kugombea mwaka huo iwapo atakosa chepuo la urais.

Huko uhitaji hata kusubiri. Lazima Prof. kachukua kitu. Yuko juu sana.
 
Wow..ikithibitika km ndio hivi then ni bomba coz Prof hakufaa kwemye jimbo lile...
Sio Jimboni tu hata katika nafasi yake wizarani, watu waligeuza UKIMWI na Maralia miradi ya kibiashara bwana, na yeye anacheka tu na kufaidika na tuVG cent twa miradi hiyo
 
Washindi katika baadhi ya majimbo
Mwakyembe (Kyela),Makongoro Mahanga (Ukonga?),Mary Nagu(Hanang?),Ole Medeye (Arumeru),Masha (Nyamagana),January Makamba (Bumbuli),Anthony Diallo (Mwanza?),Mathayo (Musoma),Ole Sendeka (Simanjiro),Richard Kasesera (Rungwe Mashariki),Hussein Bashe (Nzega),Ntukamazina (Ngara),Dr.Batilda (Arusha Mjini),Kimaro (Vunjo),Prof.Mwandosya (Rungwe Magh),Anne Kilango (Same),Nape Nnauye (Ubungo).

Wabunge Maarufu waliokwishapoteza ni Malecela (Mtera),Prof.Mwakyusa (Rungwe Mashariki),Lembeli,Mama Mwangunga na Selelii.
 
Halafu huko Kyela bila jina lako kuwa "Mwa"-somebody ina maana ndio usahau kabisa ubunge eeh?

Kutoka kwenye siasa kidogo nasikia Juma alienda kwenye intavyuu ya benki moja.wakati wa maongezi akawualiza majina watahiniwa wenzake wakati wanasubiri kuitwa .Wa kwanza kasema anaitwa mwaibabile, wa pili mwakasafyuka watatu akamwambia anaitwa Mwangolombe. Na yeye wakamuuliza unaitwa nani ikabidi aseme anaitwa Mwajuma
 
Nasubiri matokeo kutoka Rungwe ya Prof. Mwandosya, maana nilimuonya rafiki yangu Steve Mwaka atulize boli kwanza asubiri 2015 kwa kuwa nina uhakika Prof hawezi kugombea mwaka huo iwapo atakosa chepuo la urais.

Prof alifanya kosa kutogombea urais mwaka huu, alikuwa na nafasi nzuri ya kumpiga kidali poo Mh. JK. Mwaka 2015 sidhani kama ataweza kupamba na Dr. Asha-Rose Migiro ambaye wengine tunampa nafasi kubwa ya kuombwa na NEC ya CCM arudi agombee upresidaa
 
Washindi katika baadhi ya majimbo
Mwakyembe (Kyela),Makongoro Mahanga (Ukonga?),Mary Nagu(Hanang?),Ole Medeye (Arumeru),Masha (Nyamagana),January Makamba (Bumbuli),Anthony Diallo (Mwanza?),Mathayo (Musoma),Ole Sendeka (Simanjiro),Richard Kasesera (Rungwe Mashariki),Hussein Bashe (Nzega),Ntukamazina (Ngara),Dr.Batilda (Arusha Mjini),Kimaro (Vunjo),Prof.Mwandosya (Rungwe Magh),Anne Kilango (Same),Nape Nnauye (Ubungo).

Wabunge Maarufu waliokwishapoteza ni Malecela (Mtera),Prof.Mwakyusa (Rungwe Mashariki),Lembeli,Mama Mwangunga na Selelii.

Kigogo, siyo ushabiki. Ni halia halisi. Mwandosya aking'oka, CCM nayo inakosa urais mwaka huo. He is a foundation stone to it.
 
Prof alifanya kosa kutogombea urais mwaka huu, alikuwa na nafasi nzuri ya kumpiga kidali poo Mh. JK. Mwaka 2015 sidhani kama ataweza kupamba na Dr. Asha-Rose Migiro ambaye wengine tunampa nafasi kubwa ya kuombwa na NEC ya CCM arudi agombee upresidaa

Parameters ziko dynamic ndugu. mambo bado machanga kabisa. Unajua kuwa mpaka siku Dr. Bilal anatangazwa kuwa makamu wa Rais,, rais wa Zanzibar (karume) alikuwa bado anaamini kuwa yeye ndiyo makamu wa Rais?! Ilikuwa ni mikakati ya muda mrefu, lakini atmosphere ili-change mle mle CC na Bilal akachukua. Politics si mchezo
 
Ila ombea Mungu asihamie CHADEMA maana mpambano utakuwa mkali zaidi na Dr. Slaa akiwa na Mwakalinga.

Hatimaye sasa itakuwa rahisi kumwambia Mwakalinga ahamie CHADEMA.

Mkuu Sikonge,

Naomba Bwana Mwakalinga asifanye kosa hilo, lita-work against yeye. Anachotakiwa kufanya ni kutulia aangalie mapungufu yaliyojitokeza kwenye primaries. Yaliyo ndani ya uwezo wake ayashughulikie na kama yapo yaliyo nje ya uwezo wake (ya kichama) na hana namna ya kuyarekebisha basi hapo anaweza kuhama chama na kuanza kupanga mikakati mipya kwa malengo ya kugombea 2015 na sio mwaka huu.

Watu ambao wanaweza kuhama chama na wakashinda ni wale ambao wanaongoza kura za maoni na vikao vya chama vinawakata majina. Kama mgombea hakutumia njia chafu na aliongoza kihalali, akihamia upinzani ni rahisi sana kushinda. Mfano mzuri ni Dr. Slaa, aliongoza kura za maoni mwaka 1995, CCM kwa ujuba wao wakamkata jina akaona isiwe shida, akahamia CHADEMA na alishinda. Mpaka leo CCM huwa wanajutia sana hilo kosa, walikata jina bila kutafakari na kufanya uchunguzi wa kutosha.
 
Oooh this is real good news! fascinating! God is answering our prayers!
Mwakalinga 3? Oooh mai
mix with yours
 
Parameters ziko dynamic ndugu. mambo bado machanga kabisa. Unajua kuwa mpaka siku Dr. Bilal anatangazwa kuwa makamu wa Rais,, rais wa Zanzibar (karume) alikuwa bado anaamini kuwa yeye ndiyo makamu wa Rais?! Ilikuwa ni mikakati ya muda mrefu, lakini atmosphere ili-change mle mle CC na Bilal akachukua. Politics si mchezo
Gwa Kumitwu, nakubaliana na wewe ndio maana nadhani Mbeya na washabiki wa Mwandosya wafikirie juu ya ndoto yao kuwa Mwandosya atakuwa bado hot cake 2015 kama alivyokuwa 2005. Anaweza kuwa katika nafasi nzuri kama tu atapambanishwa na akina Bernard labda!! lakini kama Magufuli ata-keep pace yake hivi hivi, na Asha-Rose na wakapambanishwa na yeye anaweza akajikuta anashika namba 4. Lakini tukubaliane kuwa siasa is very Dynamic huwezi kutabiri ushindi au anguko, Chochote kinaweza kutokea. Nasubiri matokeo ya Makete Dr. Norman Sigalla anapambana na Dr. Binilith Mahenge
 
Keil,

Naliongelea kuhamia CHADEMA kwa sababu moja kubwa kuwa tayari atazoa baadhi ya watu wake na ahame nao CHADEMA. Chadema tayari watakuwa na wajumbe wengi ambao ni PRO Mwakalinga na si Pro CCM.

Hii zaidi ipo kama njia ya kusaidia KULINDA kura za Slaa kwenye uchaguz wa RAIS.

Kwa hali ilivyo sasa, sidhani kama atataka tena kurudi kwenye SIASA. Sintashangaa akirudi zake UK na kwenda kubeba Box za Kichina kama watamhitaji au abadili kazi kabisa. Kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Familia yake itakuwa upande fulani happy kuwa baba KARUDI.
Anyway, kwenye maisha huwa kuna kushinda MAPIGANO na kushinda VITA. Only God knows nani atakuwa mshindi wa VITA. Ndiyo maana huwa wanasema "Mchekaji, ni yule anacheka wa MWISHO."

Ngoja tusubiri matokeo ya SIKONGE sasa na DR. SLAA kivumbi kikianza.
 
Washindi katika baadhi ya majimbo
Mwakyembe (Kyela),Makongoro Mahanga (Ukonga?),Mary Nagu(Hanang?),Ole Medeye (Arumeru),Masha (Nyamagana),January Makamba (Bumbuli),Anthony Diallo (Mwanza?),Mathayo (Musoma),Ole Sendeka (Simanjiro),Richard Kasesera (Rungwe Mashariki),Hussein Bashe (Nzega),Ntukamazina (Ngara),Dr.Batilda (Arusha Mjini),Kimaro (Vunjo),Prof.Mwandosya (Rungwe Magh),Anne Kilango (Same),Nape Nnauye (Ubungo).

Wabunge Maarufu waliokwishapoteza ni Malecela (Mtera),Prof.Mwakyusa (Rungwe Mashariki),Lembeli,Mama Mwangunga na Selelii.

Mwawado muogope Mungu wako japo kidogo, bro!

Kwaheri ya kuonana!

FMES!
 
kwa habari za karibu nilizonazo Dr. Mwakyembe kashinda kwenye kura ya maoni akifuatiwa kwa mbali na Elias Mwanjala.
mwenye taarifa zaidi atupatie maana tambo za jimbo hilo zilikuwa si haba.

Mhh,

Quinine sources zako nimeziheshimu.

Wewe ni kati ya watu wa kwanza kabisa kuleta matokeo hapa JF. Very good job mpiganaji.
 
Prof alifanya kosa kutogombea urais mwaka huu, alikuwa na nafasi nzuri ya kumpiga kidali poo Mh. JK. Mwaka 2015 sidhani kama ataweza kupamba na Dr. Asha-Rose Migiro ambaye wengine tunampa nafasi kubwa ya kuombwa na NEC ya CCM arudi agombee upresidaa

Angediriki kugombea mwaka huu mtandao wangemmaliza, na sidhani kama CC ingekubaliana na hilo. Hapo angekuwa amejiweka mahali pabaya sana. Kama unakumbuka, Dr. Bilal alilaumiwa sana alipojitokeza kugombea mwaka 2005 na bado mwaka huu lilikuwa linaongelewa na baadhi ya wajumbe walitaka jina lake likatwe kabisa kwa kuwa eti alijitokeza 2005 kugombea.

Kilichompa ulaji Dr. Bilal ni mgawanyiko uliopo Zenji, kama NEC ya Zenji ndio wangepiga kura, Dr. Shein asingeona ndani. Sasa ili kuleta mshikamano ndani ya chama ndipo ikabidi jamaa apozwe kwa kupewa umakamu. Siasa za Zenji zinaongozwa na Bara na hasa linapokuja swala la kuteua mgombea urais wa Zenji.

Kwa hiyo turufu kama hiyo Mwandosya hawezi kuitumia huku bara na ndio ilibidi awe mpole. Bado Mwandosya ana nafasi ya kugombea, lakini uwezekano wa kushinda ni mdogo sana kwa kuwa yuko nje ya inner circle ya JK. Na kama angejitokeza mwaka huu ndiyo angewekwa mbali zaidi na kujiharibia kabisa. Subira huvuta heri, may be anaweza kupeperusha bendera ifikapo 2015.
 
Pia huko Mbeya mfanyabiashara mwenye mtandao wa mahotel ya Nkwenzuru kashinda kura za maoni CCM

Mkuu ndio nani huyo?Mbeya mjini upinzani ulikuwa zaidi ni kati ya Benson Mpesya na Mwang'onda.
 
Keil,

Naliongelea kuhamia CHADEMA kwa sababu moja kubwa kuwa tayari atazoa baadhi ya watu wake na ahame nao CHADEMA. Chadema tayari watakuwa na wajumbe wengi ambao ni PRO Mwakalinga na si Pro CCM.

Hii zaidi ipo kama njia ya kusaidia KULINDA kura za Slaa kwenye uchaguz wa RAIS.

Kwa hali ilivyo sasa, sidhani kama atataka tena kurudi kwenye SIASA. Sintashangaa akirudi zake UK na kwenda kubeba Box za Kichina kama watamhitaji au abadili kazi kabisa. Kila kitu kina uzuri na ubaya wake. Familia yake itakuwa upande fulani happy kuwa baba KARUDI.
Anyway, kwenye maisha huwa kuna kushinda MAPIGANO na kushinda VITA. Only God knows nani atakuwa mshindi wa VITA. Ndiyo maana huwa wanasema "Mchekaji, ni yule anacheka wa MWISHO."

Ngoja tusubiri matokeo ya SIKONGE sasa na DR. SLAA kivumbi kikianza.

Nashukuru kwa ufafanuzi, maana sikujua kama unaangalia mbali kiasi hicho. Ninakubaliana na mkakati wako wa kuongeza kura za Slaa. Pamoja na hayo Dr. Slaa ana kura nyingi sana na ndiyo maana hizi primaries zinaweza kuwasumbua sana CC na sasa hivi hawalali wanapiga hesabu za kupunguza kura za Dr. Slaa.

Yaani hata sijui ni nani ambao wanagombea Sikonge. Ni akina nani wanaogombea Sikonge kupitia CCM mwaka huu?
 
Back
Top Bottom