MATOKEO ya Kidato cha Nne a mjadala wa kuboresha Kufaulu

mfano shule ipi ya vipaji maalum iliingia kumi bora miaka ya karibuni?
shule ipi ya mchanganyiko?
shule ipi ya kata?
shule ipi mtu binafsi? (sio FBO)?

na kati ya 50 za mwisho je?
 
Matokeo yanapatikana vizuri kabisa kwenye website ya wizara ya elimu:

http://www.moe.go.tz


thats true but lets not divert from the main complaint of the thread.. je unakubaliana na wizara ya elimu kutumia kampuni ya simu binafsi na kuwapa exclusive tender ya kutangaza sensitive issue kwa jamii kama majibu ya mitihani? na wasio na line voda je?
 
Yanapatikana lakini kwa voda pia unaktwa HELA ili upate. Tigo na Airtell sasatel zantel hawamo. RA ndo voda bwana. wakweka wengine (makampuni) ICC itakaa movenpick kuwahukumu
 
Mkuu website ya necta was down jana na leo earlier on ! na hii issue ya voda tangazo ilikuwa linapita hapo hapo kwenye website ya necta ...hamna hadithi hapa.

Nimekusoma mkuu! Issue hapa kumbe ni website kuwa down na sio kuwa matokeo yamenyofolewa. Website kuwa down ni kawaida nadhani ni kwa sababu watu wengi wanataka kuaccess hiyo website kwa wakati mmoja na ndio maana wamejaribu kuweka na kwenye website ya wizara. Nakumbuka na TCU walipotoa selection zao kulikuwa na tatizo kama hilo kwenye website yao!
 
Hawa jamaa huwa wanalalamika sana badala ya kufanya kazi. Shuleni sio dini tu bali kupiga msuli pia, ili ufaulu sii lele mama. Wao wanaanda kongamano Caremjee la kulalamika na kupinga kauli ya Maaskofu badala ya kuchunguza tatizo kubwa ni nini? Mfano Kilimanjaro, shule za kata zilikua miaka ya 90,Wakatoliki wao wanasisitiza sana elimu
 
thats true but lets not divert from the main complaint of the thread.. je unakubaliana na wizara ya elimu kutumia kampuni ya simu binafsi na kuwapa exclusive tender ya kutangaza sensitive issue kwa jamii kama majibu ya mitihani? na wasio na line voda je?

Hapo kwenye red mkuu nadhani umeteleza kidogo! Mie naona magazeti yote ya leo yametenga kurasa kadhaa kwa ajili ya kutangaza matokeo. Na ili uweze kuyaona itakubidi ununue gazeti so sio sahihi kusema Vodacom wamepewa exclusive tender ya kutangaza matokeo. Au ni kwa vile tu ina uhusiano na RA! Watu bwana!
 
Wakuu, Mi niefuatilia matokeo ya Form four yanatiusha sana, kiwango kimeshuka sana mwaka huu. Ila kuna mambo mengi sana yanachangia

•Kumjaribu mtu kwa masaa 2-3 ni uonevu mkubwa. Inawezekana mwanafunzi akawa anfanya vizuri sana darasani laniki siku ya mtihani akawa hajisikii vizuri. Cha kufanya ni kwamba, NECTA ingeanzisha utaratibu mpya wa kutahini wanafunzi kwa awamu mbili. Moja kuchukua wastani wa miaka yote mine na uwe na uzito wa alama 30%, then mtihani wa mwisho uwe na uzito wa alama 70%. Hata vyuo wanafanya hivi pia. Waanade form za kujazwa ambazo pia mkurugenzi wa elimu wilaya na kanda atazikagua ili kupunguza degree ya kuchakachua. Hii itasaidia pia wanafunzi kusoma kwa bidii.
•Serikali kuangalia upya utitiri wa mashule yanayofunguliwa yasiyo na ubora wala walimu wa kudumu.
•Kuwe na Library ya kujisomea shuleni, shule nyingi za kata hazina library.
•Kupiga marufuku Tuition zote na kupitisha sheria kufanya kitendo hiki kua kosa la jinai.
•Kufanya elimu ya form Six kua ya lazima.
•Kubadilisha mitaala shule ili kumwezesha mwanafunzi pindi amalizapo form four angalau awe na ujuzi wowote kama userimala, ufundi, upishi, ufugaji wa kuku, kitimoto n.k
•Shule ambazo azifaulishe zipewe adhabu kali kwani wanakula ada tu za wanafunzi bila kutoa elimu bora.
 
Kama watanzania wengi wenye ndugu ambao wamemaliza form 4. Kitu kimoja kimenishangaza sana kwanini taasisi ya serikali inaweka tangazo kwamba kama mwanafunzi anataka kuona majibu kwa njia ya simu ni lazma awe na line ya VODACOM ilI apate majibu hayo! Serikali kuweni makini hio kitu haina manufaa kwa jamii husika kwasabau mnajua kabisa kwamba watu wanatumia line tofauti.


Over and out

WAFANYAKAZI SERIKALINI KUWENI MAKINI NA MIKATABA YA KIJINGA MNAYOINGIA AMBAYO HAINA MANUFAA KWA WALENGWA.

where is fair competition commission, where is PPRA na wanaharakati wapo wapi?
 
awali ya yote ningependa kuwapongeza wanafunzi waliokuwa kwenye seminari za kikristo kwa kufanya vizuri, hii sio kwamba waliosoma kwenye shule hizo ni wakristo peke yao humo kuna waislam, wahindu na wabudha pia , so mafanikio ni ya taasisi na wanafunzi bila kujali dini zao
ni ukweli usiopingika kuwa ili mwanafunzi aweze kufanya vizuri kuna mazingira yanayohitajika ili aweze kufaulu kama vile, uwepo wa walimu wa kutosha na wenye ubora na walio na morali ya kazi, uwepo wa vitendea kazi/zana za elimu k.v vitabu vya ziada,kiada na rejea,uwepo wa maktaba, uwepo wa maabara, mazingira rafiki ya elimu, standi za kufundishia, na kadhalika wa kadhalika

kitu kimoja kizuri kwenye shule za kikristo ni mfumo wao wa kutoa elimu kwani bahati nzuri nyingi ya shule hizi huwa wana karibu vitu vyote vilivyotajwa hapo juu, maana aidha shule hizi huanzishwa na makanisa yenye sadaka kubwa, misaada toka nje ya nchi au huwa wanatoza ada kubwa kwa ajili ya kumudu gharama za uendeshaji na pia idadi ya wanafunzi katika shule hizi huwa haizidi 100 kwa kidato aghalabu 50 hivi. bahati mbaya kwa shule za kiislamu huendeshwa kwa shida zikikabiliwa na changamoto nyingi za uendeshaji na ukosefu wa fedha,lakini hili hutokea zaidi kwa kuwa shule hizi zinatoza ada ambayo ni kidogo sana ukilinganisha na shule za kikristo maana zinafahamu hali ya maisha ya watanzania na kwa kuwa ada huwa ndogo hupelekea wanafunzi kuwa wengi kwenye shule hizi kitu ambacho hukompromise ubora wake
pamoja na hayo tujiulize mbona kuna seminari au shule zenye majina ya 'watakatifu' wa kikiristo na bado zafanya vibaya?zingine zipo dar hapohapo na zingine zipo huko mikoani? mtu aangalie shule mfano ST PAUL'S LIULI, DAR ES SALAAM CHRISTIAN SEMINARY, DAR ES SALAAM BAPTIST SECONDARY, BANGALA LUTHERAN JUNIOR SEMINARY, ANGALIA SHULE KAMA HII

S0983 TUMAINI LUTHERAN SEMINARY <H3>DIV-I = 0 DIV-II = 3 DIV-III = 3 DIV-IV = 44 FLD = 30

SASA tatizo hapa ni nini? ni ubora wa wanafunzi au kukosekana kwa mazingira bora ya kielimu? maana hii pia ni shule ya kanisa

binafsi watanzania tuache kulumbana na kujisifu kwamba eti shule ya dini/dhehebu fulani ni nzuri kuliko ya dini/dhehebu jingine ilhali wanaosoma kwenye shule hizo wengi wao ni watoto wa watanzania wenye kipato cha kati na sio watanzania wenye kipato cha chini, hivi tujiulize mwanafunzi kutoka kule interior kabisa nkasi, nachingwea, kibondo, ludewa, ikunguluyabashashi, kilolo, kieto huko zoisa banyibanyi, kilosa kule ureling'ombe au tanganganyika masagati ifakara je anaweza mudu shule hizo mnazojisifia nazo? ndio maana serikali imekuwa ikiwaomba wamiliki wa shule wapunguze ada. kumbukeni wanaosoma shule hizi ni watanzania na wanaofeli ni watanzania wote pasi na kujali dini zao kwani wakristo kwa waislamu

lakini swali langu dogo ni kuwa kwanini seminari siku zote hazishiki namba kwenye mitihani ya kidato cha sita??? sikuzote kumi bora zimekuwa zikitawaliwa zaidi na shule za serikali kama vile ilboru, kibaha, mzumbe, kilakala, dakawa, msalato and the like?? kwa nini hawa wanaseminari huongoza kidato cha nne na hushindwa kidato cha sita? na mbona wanaseminari hawa pindi wajapo huku kwenye shule zetu za serikali huwa tunawaburuza mbaya kwenye performance darasani kama wao ni vichwa ile mbaya?
kwa hiyo mazingira rafiki huwasaidia wanafunzi wa seminari lakini haithibitishi kwamba wao ni bora sana kuliko wanafunzi walioko kwenye shule za kawaida


</H3>
 
halafu mnasema CCM wana udini, udini uko hapa kwenu wenye blogu, msifurahie hawa watoto kufeli, wala kuwashindanisha, mtakapokuwa wazee hawa ndio watakuwa madaktari feki,
hapa kuna shule za aina nyingi,
zenye wanafunzi zaidi ya 40 au pungufu,
za mchanganyiko wa sex au kutofautisha,
za serikali au binafsi
za serikali vipaji maalum au za kata
za dei au boarding
zenye A level pia au O level tu
za mijini au vijijini
zenye zaidi ya miaka kadhaa au mpya,
za binafsi za dini au binafsi wasio dini, au seminari
nk
nk


hebu tuchanganue kote huko tuangalie tatizo liko wapi


Haika,
Huo ndio uzalendo. Keep it up.
Ni vizuri tukaangalia vijana wamefelije kwenye shule zote bila kujali inamilikiwa na nani kwasababu mwisho wa siku, hao waliofeli watakuwa bado ni watanzania wenzetu na tutahitaji walete maendeleo kwa nchi bila kujali wanaamini dini gani.

Great thinkers, naomba tuachane na ushabiki wa kidini, hauna tija as usual mbali na kuleta maumivu tu kwenye roho zetu.
 
Waalimu wa seminary za kislamu ni maaustaadhi flani hivi....wao hawajasoma, watafundisha kweli? muda mwingi unatumika kukariri kuruani, na kwa kwa kuwa ni kiarabu basi inakula muda kweli. Kwa kifupi wahazingatii kabisa ellimu dunia..wao ni ya akhera ndo muhimu.
 
Ngoja niwape experience yangu huko Uganda. Kule wanazo shule za ki-islam kama kwetu Bongo na zinafanya vizuri sana kama shule nyingine. Tofauti kati ya Uganda na hapa ni kwamba kule kwenye elimu hakuna itikadi. Shule za ki-islaam zinatafuta walimu wazuri bila kujali kabila, dini, jinsia au rangi. Bila wenzetu kubadilika na kuacha ubaguzi wa kijinga hali itabaki kuwa hivi na kuishia kulalamika. Unategemea nini katika best students 80% ni wakristu? Lazima uwiano huko mbele litakuwa tatizo. Au kuna ubaya gani kumpata mwalimu mzuri wa Hisibati hata kama sio muislam akafundisha watoto hisibati kwa ufasaha? Upuuzi mtupu!!
 
Wakuu, Mi niefuatilia matokeo ya Form four yanatiusha sana, kiwango kimeshuka sana mwaka huu. Ila kuna mambo mengi sana yanachangia

&#8226;Kumjaribu mtu kwa masaa 2-3 ni uonevu mkubwa. Inawezekana mwanafunzi akawa anfanya vizuri sana darasani laniki siku ya mtihani akawa hajisikii vizuri. Cha kufanya ni kwamba, NECTA ingeanzisha utaratibu mpya wa kutahini wanafunzi kwa awamu mbili. Moja kuchukua wastani wa miaka yote mine na uwe na uzito wa alama 30%, then mtihani wa mwisho uwe na uzito wa alama 70%. Hata vyuo wanafanya hivi pia. Waanade form za kujazwa ambazo pia mkurugenzi wa elimu wilaya na kanda atazikagua ili kupunguza degree ya kuchakachua. Hii itasaidia pia wanafunzi kusoma kwa bidii.
&#8226;Serikali kuangalia upya utitiri wa mashule yanayofunguliwa yasiyo na ubora wala walimu wa kudumu.
&#8226;Kuwe na Library ya kujisomea shuleni, shule nyingi za kata hazina library.
&#8226;Kupiga marufuku Tuition zote na kupitisha sheria kufanya kitendo hiki kua kosa la jinai.
&#8226;1.Kufanya elimu ya form Six kua ya lazima.
&#8226;Kubadilisha mitaala shule ili kumwezesha mwanafunzi pindi amalizapo form four angalau awe na ujuzi wowote kama userimala, ufundi, upishi, ufugaji wa kuku, kitimoto n.k
&#8226;2.Shule ambazo azifaulishe zipewe adhabu kali kwani wanakula ada tu za wanafunzi bila kutoa elimu bora.

1. Wajameni, hili nalo litasaidiaje watoto kufaulu kidato cha nne?
2. Shule kama haitoi elimu bora, usimpeleke mwanao. Sasa mwanao kashindwa interview kwenye shule nzuri (nyingi za Katoliki) inabidi umpeleke popote; na matunda yake ndiyo hayo. Lingine ni kwamba shule nzuri gharama yake ni kubwa, hivyo ukichagua gharama ndogo si budi hukubali matokeo.
 
Wadau inakuwaje hawa watoto wamechemsha kiasi hicho, kwenye hizo paper za form four? nani alaumiwe, wazazi, wanafunzi au serikali? Mimi nina kigugumizi
 

Attachments

  • cartoon Elimu.jpg
    cartoon Elimu.jpg
    40.3 KB · Views: 149
1. Wajameni, hili nalo litasaidiaje watoto kufaulu kidato cha nne?
2. Shule kama haitoi elimu bora, usimpeleke mwanao. Sasa mwanao kashindwa interview kwenye shule nzuri (nyingi za Katoliki) inabidi umpeleke popote; na matunda yake ndiyo hayo. Lingine ni kwamba shule nzuri gharama yake ni kubwa, hivyo ukichagua gharama ndogo si budi hukubali matokeo.
Hilo ndio suluhisho pekee!!!
 
Hapo kwenye red mkuu nadhani umeteleza kidogo! Mie naona magazeti yote ya leo yametenga kurasa kadhaa kwa ajili ya kutangaza matokeo. Na ili uweze kuyaona itakubidi ununue gazeti so sio sahihi kusema Vodacom wamepewa exclusive tender ya kutangaza matokeo. Au ni kwa vile tu ina uhusiano na RA! Watu bwana!

Mkuu naona unajaribu saana ku divert issue..hamna mtu anayelalamika majibu kutopatikana kwa wananchi..issue ni kwamba iweje wizara iwatumie voda peke yake?? na pili kwanini voda icharge watu wakati wizara ina budget maalum ya kutangazia wanafunzi kama wanavyofanya kwenye magazeti? Unachoshindwa kuelewa wewe ni nini ??
 
Back
Top Bottom