Hongera sana CDM kwa ushindi wa arumeru, udiwani mbeya na mwanza. Kwa mtizamo wangu juu ya hii thread uko tofauti na wanaofikiri kuwa EL ndiyo sababu ya kushindwa kwa Ccm.
Sasa hivi watz wameuchoka utawala wa ccm ambao haujakidhi matakwa yao kwa muda mrefu. Hali ya maisha imekuwa mbaya siku hadi siku, na hakuna dalili zozote zinazoonesha yatakuwa bora siku za karibunim
Kibaya zaidi ni kuwa walioaminiwa kupewa dhamana ya raslimali zetu wamekuwa wakitoa majibu mepesi kwa maswali magumu ya namna ya kumfanya mTZ ajivunie utaifa wake na kufaidi raslimali zao.
Wanye nchi wameamka sasa, wanachotaka kuona ni changes na si kulalamika tena ndiyo maana kila nafasi sana ccm out! Watawala nao, (ccm) bado wana imani kuwa dola inaweza kuwasaidia ( polisi, usalama wa taifa nk) lakini nguvu ya umma ni kiboko! Ona yaliyotokea arumeru, watu wote influential walikuwa kule lakini nguvu ya umma ikawabwaga!
Hii ni salamu tosha kuwa 2015 wajiandae kuwa chama cha upinzani