NasDaz,Kama ndivyo ilivyotokea bado naendelea kushikiria msimamo wangu kwamba kuna ulazima viwango vya zamani vitumike......it's wasn't fair at all! Mitihani imefanyika somewhere around October - November huku wahusika wakuu (wanafunzi wakiwa wanafahamu wazi kwamba grading ipo hivi!! Mitihani wameshafanya, wametulia nyumbani wanasubiria matokeo; huku nyuma wapuuzi wachache wanakaa na kuweka viwango vipya....NO, UNACCEPTABLE! Narudia, wengi wetu tunatamani kila wakati tupate sababu ya kuilaumu serikali; hapa wasilaumiwe kwa kurudisha viwango vipya bali walaumiwe kwa kutumia viwango vipya kinyemela (bila wahusika waathirika wakuu) kufahamu! Tuache ubinfasi wa kujiona tumeshavuka mto! Hapa JF nafahamu kuna wanafunzi wengi wa vyuo vikuu! Assume, tangu unaingia First Year unafahamu (say) C inaanzii 50-64; na umefanya paper unafahamu hivyo ndivyo viwango! Hatimae unarudishiwa paper yako, unakuta umepata 52; unapumua kidogo coz' unafahamu umepata C. Matokeo yanawekwa notice board, unakuta somo husika umewekewa D; unakuja kuhoji unaambiwa mara baada ya mitihani kwisha; board ilikaa na kuweka viwango vipya ambavyo C inaanzia 55-69! Let's be honest here...hivi kweli huko vyuoni kungekalika?! Yaani from nowhere, muambiwe viwango vibadilishwa tena kimya kimya! HAPANA, HILI HALIKUBALIKI! Hao wote waliokaa na kupitisha maamuzi sio waathirika wa moja kwa moja, waathirika wa moja kwa moja ni wanafunzi waliohusika na wazazi/walezi wao!
cc JokaKuu
JokaKuu,NasDaz,
..lakini NECTA ni chombo cha serikali pia.
..umesahau kwamba mtendaji mkuu wa necta anateuliwa na raisi??
..binafsi nadhani students were not supposed to fail that much hata kama grading scheme[madaraja]imebadilishwa.
..naamini wanafunzi wameathirika kiasi kile kwasababu wengi wao wanafaulu at borderline.
cc: Kichuguu, Kitila Mkumbo, @Kubwajinga, Nyani Ngabu
JokaKuu,
You're right, NECTA ni chombo cha serikali! Lakini kuwa chombo cha serikali hakuhalalishi wao kufanya mambo ya hovyo hovyo yakaachwa yapite kwavile tu mambo hayo yamefanywa na mamlaka inayotambulika na kwa baraka za serikali! Na kimsingi hoja yangu haisimami kwavile tu wanafunzi wamefeli; ninachosimamia mimi ni kwamba kilichofanyika hakikuwa right! Inawezekana kabisa katika kubadilisha Grading NECTA hawalazimiki kuutaarifu umma au inawezekana kabisa kwamba NECTA wana mamlaka ya kubadilisha GRADING hata siku rasmi ya kuanza kusahihisha mitihani yenyewe; lakini hata kama wana mamlaka hayo, bado si sahihi kufanya jambo linaloakisi maisha ya watu kihuni huni namna hiyo!
Suala la grading ni sensitive issue ambayo wahusika ni lazima walifahamu in advance na ndio maana hata kwenye University Prospectus unakuta Grading zimewekwa mle! Mtu unaanza First Year, unafahamu kabisa kwamba nikipata marks fulani; hiyo ni A or B or anything like that! Sasa kama kitu ni sensitive kiasi hicho, watu wachache hamuwezi kuamka na kuanza grading mpya bila wadau kufahamu! Kwa mfano, taarifa ya Mwananchi wanasema makubaliano ya kubadilisha grading yalifanyika December.....what does it mean? Yaani wakati mitihani imeshaanza kusahishwa, tena wakati hata wasahishaji wanafahamu kwamba grading zipo hivi na hivi; huku nyuma, waheshimiwa wachache wanaamua vinginevyo! No, sio sahihi kabisa!
Ikiwa tuta-entertain suala la NECTA kupandisha viwango kinyemela na kuona wapo right; sijui tutakuwa na mamlaka gani ya kuwasimanga siku wakiamua tena kushusha viwango kinyemela!!
Nakubaliana na hoja yako kwako kwamba " students were not supposed to fail that much hata kama grading scheme[madaraja]imebadilishwa", lakini kama nilivyosema hapo awali, iwe wamefeli sana au wamefaulu sana; bado haikuwa sahihi!
Mkuu wangu,Chifu,
Unataka kumaanisha kwamba grading system mpya ndiyo chanzo cha kufeli vibaya kwa kidato cha nne 2012?!?
Sasa ikiwa maamuzi ya kubadili grading yalifanyika December 2012; hao wanafunzi wangepata saa ngapi taarifa hizo wakati wahusika (watahiniwa 2012) walikuwa wameshafanya mitihani na kuwa majumbani kwao!!? Inawezekana mashuleni taarifa zilifika lakini zilifika wakati grading mpya zimeshatumika! Katika hali ya hali kawaida, nilitarajia suala la new grading lingefanyika na kutangazwa kwa wadau/wanafunzi angalu miezi kabla ya mitihani!NasDaz,
..mimi nadhani wananchi tunapaswa kuambiwa ukweli about who knew what and when.
..imeelezwa kwamba vikao vya maamuzi ya kubadili grading system vinahusisha watendaji wa necta na wizara.
..sasa ktk mazingira hayo kwanini taarifa hizo hazikufika mashuleni na kwa wanafunzi?
..mimi panahitajika kufanyika mabadiliko makubwa necta na wizarani. hivi tutakuwa taifa la aina gani huko mbele ya safari?
NasDaz,Sasa ikiwa maamuzi ya kubadili grading yalifanyika December 2012; hao wanafunzi wangepata saa ngapi taarifa hizo wakati wahusika (watahiniwa 2012) walikuwa wameshafanya mitihani na kuwa majumbani kwao!!? Inawezekana mashuleni taarifa zilifika lakini zilifika wakati grading mpya zimeshatumika! Katika hali ya hali kawaida, nilitarajia suala la new grading lingefanyika na kutangazwa kwa wadau/wanafunzi angalu miezi kabla ya mitihani!
Suala la kufanya mabadiliko makubwa wizarani na NECTA, naunga mkono kwani inavyoelekea mambo yanaendeshwa "Biz as usual!"
@JokaKuu,NasDaz,
..kama ni hivyo wahusika wizarani na necta wanapaswa kuchukuliwa hatua.
..uamuzi sensitive kama huo unafanyika na hakuna mtu serikalini anachukua hatua za kuusitisha??
..hii nchi iko inajiendesha yenyewe kwa kweli. we dont have a government.
Bro hoja ya ina mantiki kwa mambo mawili.Kikao cha kupitisha Viwango Vipya vya Ufaulu vilivyotumika kwa Kidato cha Nne kilihusisha Wizara ya Elimu na Ufundi,NECTA na TCU. Nyaraka za kikao hicho kilichofanyika Disemba mwaka jana,zinaonesha kuwa kikao husika kilikuwa chini ya Uenyekiti wa Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi,Dr.Shukuru Kawambwa na Katibu wa Kikao alikuwa Naibu wake Bwana Phillipo Mulugo.
Kwa upande wa NECTA,waliwasilishwa na Mwenyekiti wake Prof.Rwekaza Mukandala na Katibu Mtendaji wa Baraza hilo,Dr.Joyce Ndalichako.Pia alikuwepo Mjumbe kutoka Mamlaka ya Vyuo Vikuu nchini-TCU ambaye alikuwa ni Prof. Sifuni Ernest Mchome (ambaye baadaye akawa Mwenyekiti wa Tume ya Kuchunguza Ufaulu wa Kidato cha Nne!)
Kikao hicho kiliidhinisha kutumika kwa viwango hivyo vipyakwa kidato cha nne na cha sita. Wajumbe wote wa Mkutano walikubaliana na viwango vipya na matumizi yake kwa kidato cha nne 2012.
Habari zaidi zimeripotiwa katika Mwananchi la leo
Je, kuchunguza na kutaka kubadili matokeo haya si dharau zilizopitiliza kwa watanzania? Je, ni halali kwa Prof.Mchome kuhudhuria kikao na halafu kuongoza Tume ya Kuchunguza? Watanzania tumedharauliwa,sasa tuchukue hatua gani? Nani mtanzania muungwana atawaamini watu hawa kwasasa?
Kwa hiyo Mchome naye ni Profesa?
NasDaz,
..nimesoma gazeti la mwananchi.
..Prof.Mchome, mwenyekiti wa tume ya kuchunguza matokeo, alikuwepo kwenye kikao cha wizarani kuzungumzia mfumo mpya wa madaraja!!