Matokeo kidato cha nne yamechakachuliwa

Matokeo kidato cha nne yamechakachuliwa

Kaka ukistaajabu ya musa utazima kuona samsoni akivunja miamba.. Nilicho sikia mimi ni kwamba eti kwa kuwa shule za kata ndio hasa hufanya vibaya! Hzo ndizo zimelengwa kufanyiwa hyo adjustment ili serikali waonekane wame upgrade ktk kusimamia muamko wa elim. Ndo taifa letu jamani. Litawaliwalo na watu wazima waigizaji na ubishow
Bila kuboresha mazingira ktk Shule za kata matokeo yataendelea kushuka kitafika kipindi hata wakiweka A iishie 45 bado wanafunzi hawataipata.... Waache SIASA wapeleke vitabu, walimu, wajenge maabara na zana za kufundishia na kujifunzia
 
Wasemaji wa taifa wamezidi kuwa wengi. Watu wanatunga habari utadhani walikuwepo kwenye usahishaji. Siku zote kauli ya mwisho ni ya kiongozi husika katika masuala hayo na siyo laymen. Tusikurupuke na kutoa taarifa za uongo itawacost sana hasa katika issue za kitaifa.
 
Hizo ni taarifa za kweli na sababu hasa ni wanafunzi wa kiislamu wamefeli sana na shule za kiislam kuwa na matokeo mabaya.nchi afadhali ingeongozwa na mbwa
 
Hizo ni taarifa za kweli na sababu hasa ni wanafunzi wa kiislamu wamefeli sana na shule za kiislam kuwa na matokeo mabaya.nchi afadhali ingeongozwa na mbwa

dogo acha kutusi watu. ww ungependa uongozwe na mbwa? teh.teh....
 
serikali acheni mambo ya ajabu bwana,tumechoka kusubiri,nasikia ngoma mpaka 4rm 6 wamalize paper
 
Waziri wa elimu na katibu mkuu (waislam) wanaendekeza udini sana
 
Waziri wa elimu na katibu mkuu (waislam) wanaendekeza udini sana
 
Taarifa nilizozipata hivi punde ni kuwa bado mvutano kati ya NECTA na Serikali unaendelea.Serikali inalazimisha kutangazwa kwa matokeo 'bora' huku NECTA ikitaka kutangaza matokeo halali.Dr.Joyce Ndalichako amenihakikishia kuwa hatafyata mkia juu ya hili.Naibu Waziri wa Elimu,Phillipo Mulugo,haishi kupiga simu NECTA kuulizia maagizo ya Serikali kwa NECTA.Matokeo yalipaswa yatangazwe leo Jumatatu ya tarehe 6/2/2012.Mulugo ameyakwamisha.Mchafukoge.Wahitimu kaeni chonjo...ukweli utajulikana muda si mrefu.
 
Ukimya wangu humu jamvini ulinisogeza karibu na Wasahihishaji wa Mitihani ya Kidato cha nne.Wasahihishaji wamenidokeza kuwa kutokana na kufanya vibaya kwa wanafunzi wa kidato cha nne waliomaliza Oktoba mwaka jana kuliko hata mwaka uliotangulia 2010,Serikali iliamua kufanya 'Standardization' ya kuua rasmi elimu ya Tanzania.Habari zilizonifikia zinasema kuwa Daraja D limehesabiwa kuanzia alama 15,C-35,B-55 na A-75 badala ya 21,41,61 na 81 inavyotakiwa kuwa kwa madaraja husika.Kulitokea mvutano wa wazi katika kikao hicho cha 'kustandardize'.Serikali imelenga kutangaza kuwa Matokeo ni mazuri na ufaulu umepanda.Inajiandaa kujisifu kwa takwimu.Baraza haliko tayari kwa hilo.Mvutano.Hii ndio sababu hasa ya kuchelewa kutangazwa kwa matokeo hayo.Mwenye macho haambiwi tazama.

Huu ni uongo wa hali ya juu...(Kama hujui kitu usibwatuke) na sidhani kama kwa utaratibu huu wa kuleta habari za uongo tutafika unless tupo kisiasa zaidi....mimi nilifikiria JF ndio sehemu ambayo watu wanaweza kupata harabi za makini lkn kwa mshangao sivyo...hakuna issue ya kufeli wala issue ya standardization...ila kilichopo ni utaratibu ambao baraza imeamua kuufanya kama njia mpya ya kupata utaratibu mpya wa matokeo...kama ilivyokuwa zamani walivyoweza kubadili utaratibu wa kuwa na mtaalamu mmoja ambaye ndio alikuwa anashikilia utaratibu mzima wa utungwaji wa maswali..

Lazima tukubali kwamba serikali inajitahidi licha ya kwamba wananchi mnaona kwa uchache wake kubadili mifumo chakavu na duni kwahiyo sidhani kama ni hivyo unavyosema hapo...Wanafunzi wasubirie matokea and probably this week yanatoka.
 
Jamani kwanza wote tumeoza kwani wanafunzi hawa wako kwenye jamii iliyoyokosa maadili kwa kiwango kikubwa kwani tabia zooote mbaya walizo nazo wameiga kwetu ndio maana tunashindwa hatakuwakaripia tunaishia kusema niliona nikasikitika sana so wote tubadilike, pili hawa waalimu waliopewa jukumu lakuwalea na kuwafundisha hawa watoto wanatekeleza majukumu yao ipasvyo! kama mwalimu nilazima uhakikikshe mwanafunzi anaelewa unachomfundisha basi kama jitihada zako zimegonga mwamba lazima utumie njia mbadala hatakama nikuwatengea sehemu maalum walio wazito kuelewa ili kuwe nautaratibu maalum kwajili ya kuwasaidia ndipo tutakapofika tunakotaka Tanzania iwe. kwani wanalipwa ili wafanye kazi ya kuelimisha so kama hawajaelimika walimu waajibishwe*
 
CCM oyeeeee

Back
Top Bottom