Matokeo jumla ya uwakilishi Zanzibar

Matokeo jumla ya uwakilishi Zanzibar

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,585
Reaction score
11,260
Wakuu heshima kwenu!
Tangu Jana nimetafuta Sana matokeo haya lakini sijabahatika kupata. Ningependa kujua visiwani Pemba CCM wana majimbo mangapi na vyama vingine pia hali kadharika unguja. Au yapo jikoni bado??my take
Huenda baraza la wawakilishi likawa la chama kimoja!!!!!!
 
lol!!!! Nimesikia wamechukua majimbo yooote na kata (wadi) zooote
kuna mbunge pemba kaibukia ushindi wa kura 90!!!!!
 
lol!!!! Nimesikia wamechukua majimbo yooote na kata (wadi) zooote
kuna mbunge pemba kaibukia ushindi wa kura 90!!!!!

Walichokifanya kwenye urais nadhani walisahau kwenye ubunge, kwa hiyo hawana amani wakiweka matokeo ya ubunge wazi kwa wote watu tutalinganisha uraisi na ubunge.
 
Sanaa za zanzibar ni za kuchekesha sana..!
Hiki ni kivutio kingine cha utalii hapa nchini kuna umuhimu wa kukitangaza tupate fedha za kigeni..!
 
kwa kweli hawakukosea walivyooiiita serikali ya mapinduz Zanzibar. halafu wanakasalam chao ka kipuuz ''mapinduz daima"
 
Hivi hakuna namna Zanzibar nzima ikawa museum ya Tanzania? Kwamba kila kilichoko kule kuanzia binadamu, nyumba, mimea na kila ktu viwe kwa ajili ya kumbukumbu na maonyesho tu? Ila tuhakikishe kwamba watu wanazalisha kama jeshini kwa matumizi yao, wanahudumiwa wanapohitaji msaada, wanalindwa na kutibiwa na kutunzwa kama sehemu yoyote ya kumbukumbu za maonyesho inavyohifandhiwa?

Sioni kama kuna la zaidi kwa sasa.
 
Kuna Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi kule Pemba kapata kura 06 na kawa Muwakilishi....Yaani sijui Tanzania ilirogwa na nani mamaaeee
 
Halafu mkweree eti anakwenda kusuluhisha Libya!!! What a waste of resources!!
 
Walichokifanya kwenye urais nadhani walisahau kwenye ubunge, kwa hiyo hawana amani wakiweka matokeo ya ubunge wazi kwa wote watu tutalinganisha uraisi na ubunge.
Gazeti la nipashe la leo lina matokeo ya uwalikilishi
 
22nd March 2016

Chama Cha Mapinduzi (CCM) Matokeo ya majimbo mbalimbali yameanza kutolewa visiwani hapa huku Chama Cha Mapinduzi (CCM), kikiongoza kwa kupata majimbo mengi ya Wawakilishi.

Matokeo kamili ni kama ifuatavyo:-

JIMBO LA MWERA:
CCM kura 3,478, CUF (81),

Bububu CCM imepata kura 6,581, CUF (2,010), ADC (2,018),

Mtopepo
CCM (6,606), CUF (195), Tadea (226)

Mfenesini
CCM (5,743), CUF (130) na ADC kura 186.

WELEZO:
CCM (4,707), (CUF 75) na Chauma (107)

MTONI:
CCM (8,089), ADC (322), Chauma (119) na CUF (198).

PAJE:
CCM 8,194, ACT 100 na CUF 82

MAKUNDUCHI:
CCM 10,718, ADC 167, CUF 71 na Chauma 56

KIJITOUPELE:
CCM kura 6,968, CUF 110 na SAU 111.

FUONI:
CCM 1426 na CUF 44.

CHUKANI:
CCM kura 5,931, CUF 176, ADC 158 na Demokrasia Makini 23.

KIEMBESAMAKI:
CCM 6,931, CUF 156, Demokrasia Makini 110 na NRA 79.

MWANAKWEREKE:
CCM kura 5,399, CUF 161.

PANGAWE:
CCM 5,369 na CUF 161.

CHONGA:
CCM 3,555, ADC 173, ACT 93 na CUF 66.

WAWI:
CCM 4,239, ADC 997, CUF 89, ACT 74 na Chauma32.

CHAKECHAKE:
CCM 4,455, ADC 274, CUF 128 na ACT 37.

OLE: CCM 3,769, ADC 98, CUF 48 na NRA 0.

ZIWANI:
CCM 2,789, CUF 153, ADC 381 na UPDP 221.

MTAMBILE:
CCM 3,154, ADC 273 na CUF 68.

CHAMBANI:
CCM 2,971 na ADC 593

KIWANI:
CCM 4,031, ADC 376 na CUF 47.

MKOANI:
CCM 6,331, ADC 140, CUF 138, ACT 57 na Tadea 45.

WETE:
CCM 3,665 na CUF 96.

MGOGONI:
CCM 3,380, CUF 43 na ADC 14.

MTAMBWE:
CCM 1,685, ADC 97, CUF 34, UPDP 25 na ACT 17.

KOJANI:
CCM 3,874, NRA 247, ADC 240, CUF 112, AFP 85 na ACT 39.

GANDO:

CCM 2,965, CUF 135 na CUF kura 73.
 
Matokeo yenyewe ni kura 58000 sasa watagawajegawaje
 
Hivi hakuna namna Zanzibar nzima ikawa museum ya Tanzania? Kwamba kila kilichoko kule kuanzia binadamu, nyumba, mimea na kila ktu viwe kwa ajili ya kumbukumbu na maonyesho tu? Ila tuhakikishe kwamba watu wanazalisha kama jeshini kwa matumizi yao, wanahudumiwa wanapohitaji msaada, wanalindwa na kutibiwa na kutunzwa kama sehemu yoyote ya kumbukumbu za maonyesho inavyohifandhiwa?

Sioni kama kuna la zaidi kwa sasa.
Naona unataka kugirwa tu hamna jengine unalotafuta
 
Back
Top Bottom