Ligi ya Tanzania ipo Tano bora. Je, tunakosea wapi Kimataifa?

Dabil

JF-Expert Member
Sep 30, 2021
5,885
13,263
Wakuu sasa ni mwaka wa 3 kama sikosei ligi ya Tanzania kuwepo kwenye rank ya ligi bora Africa, lakini timu zetu zinakosea wapi?

Tukiweka ushabiki msimu uliopita Yanga walifika fainali ya shirikisho, Simba nayo imeingia robo fainali club bingwa na kurudi hapo.

Yanga waliweka malengo kufika makundi mwaka huu ingawa wametimiza malengo yao lakini bado inajitafuta.

Simba malengo yake kila mwaka ni kufika nusu ila hatuyatimizi na hapa hakuna kuchekana maana pia kwa Yanga kufika fainali ya shirikisho halafu kuishia makundi ni malengo madogo sana.

Simba kila mwaka malengo ni nusu fainali, cha kushangaza wachezaji karibia wote wame-flop.

Ligi ya 5 kwa ubora Africa ila hata robo mwaka huu ni ngumu.

Je tunafeli wapi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wanaoitia vionjo ligi yetu ni wachezaji wa nje, chama, pakou, mayele, okwi, kagere, kina varane etc.. Ni wageni na katika timu yetu ya taifa wanapata namba moja kwa moja.

Hiyo sababu ya kwanza. Ubora wao kwa ngazi ya klabu lazima watishe kwa ligi zetu za afrika, wangekuwa ni watz wangeongeza ubora wa kuwatishia timu kadhaa za afrika ila si zile bora kabisa japo tungesumbuana nao kimtindo.

Wenzetu ngazi ya timu ya taifa wana professionals wengi wanacheza ligi za nje huko.

Algeria, morroco, nigeria etc wana wachezaji wakunwa wanacheza ligi za ulaya, nasi tutengeneze vipaji vingi viende nje.
 
Wanaoitia vionjo ligi yetu ni wachezaji wa nje, chama, pakou, mayele, okwi, kagere, kina varane etc.. Ni wageni na katika timu yetu ya taifa wanapata namba moja kwa moja. Hiyo sababu ya kwanza. Ubora wao kwa ngazi ya klabu lazima watishe kwa ligi zetu za afrika, wangekuwa ni watz wangeongeza ubora wa kuwatishia timu kadhaa za afrika ila si zile bora kabisa japo tungesumbuana nao kimtindo.

Wenzetu ngazi ya timu ya taifa wana professionals wengi wanacheza ligi za nje huko.
Algeria, morroco, nigeria etc wana wachezaji wakunwa wanacheza ligi za ulaya, nasi tutengeneze vipaji vingi viende nje.
Nahisi umeingia CHAKA mkuu.. huyu jamaa alimaanisha kwann timu (klabu) za Tanzania hazifanyi vizuri kwenye michuano ya kimataifa ..

Kwa mfano mwaka huu tulikua na nafasi nne kimataifa mbili za Shirikisho na mbili za klabu bingwa... Lakini mambo yamekua magumu Sana ambapo

Azam alitolewa hatua ya awali kabisa na vibonde vya kihabeshi

Singida big stars nazo walifia hatua ya kwanza baada ya kuvuka Ile ya awali Kwa kuwatoa wazenji.. lakini walipigwa na wamisiri wakashindwa kufuzu makundi

Simba na Yanga hali ni tete huko kwenye makundi wanaburuza mkia... Tena aibu ni kua wao pekee ndo hawajashinda mechi hata moja Katika makundi yote
 
Changamoto ligi ina timu tatu tu! Zenye ushindani wa kweli wengine waliobaki ni wasindikizaji kazi yao ni kugawa point tu kwa vigogo
 
Mimi ninachofahamu ni kwamba Afrika kiwango cha mpira kimeshuka sana na Tanzania vilevile.

Huwezi ukalinganisha kiwango cha mpira cha hii Al Ahli ya sasa na ile ya miaka ya themanini au tisini, utakuta kwamba hii Al Ahli ya leo ina wachezaji wa kawaida sana na wala hawana vipaji vya asili kama waliokuwa nao hawa hapa chini 👇

Angalia hii Zamalek "nyambole" ya sasa na hii ya miaka ya themanini:👇

Angalia Raja Casablanca ya sasa na ile ya miaka ya tisini ni tofauti kama usiku na mchana:👇

Uko sahihi kwa kiasi fulani ila si kwa Afrika tu, duniani kote mpira umebadilika sana, umekuwa mpira wa kimbinu kitimu zaidi na siyo vipaji binafsi ambavyo havipo sana sasa hivi. Ni nadra sana sasa hivi kumuona mchezaji anayestand out kwa uwezo wake binafsi. Na kwenye hilo unakuta gape limepungua kati ya nchi na nchi au timu na timu maana mbinu za darasani wanazotumia timu zote ni zile zile tu.
 
Kuwa tano bora kunasaidia nini?Tuangalie mbele zaidi

Taifa litambue kuwa mpira siyo burudani tena .football is an industry.tukifika hapo kifikra tutafanya yafuatayo
1.Tuwe na sera ya michezo inayoendana na mazingira ya sasa

2.Michezo mashuleni na vyuoni ni lazima na kuwepo na walimu waliobobea katika michezo

2 Umiseta na umitashumita irudi kama zamani

3 Vyuo vya soka kama vile soccer academies vijengwe

4 Viwanja vya wazi angalau viwili kila kijiji

5.Tujenge viwanja vyenye ubora.yaani stadiums

6.Tupambane na usimba na uyanga kiintelijensia bila wao kujua.hii ni sumu
7.Serikali isiingilie mpira wa miguu na kuleta siasa za ajabu ajabu.mpira wa miguu kwa kuwa ni industry una uwezo wa kujiendesha

8.uchumi wa nchi una mahusiano na football.umadkini tulionao unatisha
9.Watu waovu wanaotaka kutumia football kwa naslahi yao wabainiwe na wafutiliwe mbali.

10.kuwepo na standards maalumu kitaifa kwa wadau wote wa michezo zikiwemo vilabu.yaani tuwe na vilabu bora tu
Vilabu viwe na sifa kadhaa ambazo visipokidhi visiruhusiwe kusajiliwa na kushirili kwenye ligi zote zilizo chini ya TFF

Mfano unaweza kuweka sharti kuwa lazima kila klabu iwe na academy,uwanja waje na uwanja wa mazoezi na vitega uchumi kadhaa ili kuifanya klabu ijiendeshe
11.Tupambane na rushwa michezoni nk
Wengi wetu tunajidanganya kuwa soka letu liko mbali.huu ni uongo.class yetu ni ya chini sana.

Soka la Afrika nalo limetawaliwa na rushwa.

Kwanini tunafunga timu kubwa kwenye makundi tu na tukiwa nyumbani?

Bado sana
 
Changamoto ligi ina timu tatu tu! Zenye ushindani wa kweli wengine waliobaki ni wasindikizaji kazi yao ni kugawa point tu kwa vigogo
Hiyo ni system ya ligi karibia zote duniani Kwa uzoefu wangu...
Nenda Laliga, ligi ya misri, south Africa, Rudi DRC hata Huko Morocco timu Bora ni mbili au tatu walau EPL ndo kidogo kuna upinzani lakini Mabingwa hua n walewale...
 
Epl man city anacheza na Wolverhampton jasho linamtoka kweli kweli kupata point tatu

Ukirudi bongo yanga simba na azam point tatu wanapata kilaini mno hawatoki jasho jingi kushinda mechi zao

Ukijumlisha na viwanja vibovu, maslahi duni kwa wachezaji marefa wabovu ndio kabisa ligi yetu inakuwa haina ubora kushindana na ligi imara zaidi africa
 
Back
Top Bottom