Benchika atangaza vita dhidi ya Al Ahly

Mr Alpha

Senior Member
Jul 31, 2018
195
522
Kocha Mkuu wa Simba SC, Abdelhak Benchikha amesema vijana wake wapo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Al Ahly na wanahitaji kupata mabao mengi nyumbani, ili kujitengenezea mazingira mazuri kufuzu nusu fainali.

Akizungumza katika mkutano wa waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Benchikha amesema amekiandaa vizuri kikosi chake kuelekea katika mchezo huo.

"Kuna tofauti kubwa nilipocheza dhidi ya Al Ahly nikiwa na US Alger na mchezo ule ulikuwa tofauti na huu. Ule ulikuwa mchezo mmoja tu, lakini sasa tunaenda kucheza michezo miwili, ambayo lazima tushinde ili kufuzu," amesema Benchikha.

Amesema, Al Ahly ni timu kubwa lakini lengo lake ni kuhakikisha anaivusha Simba kwa mara ya kwanza kuelekea hatua ya nusu fainali.

"Lengo tulilojiwekea hapo mbele ni kufika nusu fainali na hatuwezi kufika bila kushinda mchezo wa robo fainali. Al Alhy ni timu kubwa, tunaiheshimu lakini lazima tutumie vizuri uwanja wetu wa nyumbani, " amesema Benchikha.
 
SISI WANASIMBA TUNAINGIA KAMA UNDERDOG
 
Hawa Al Ahly inabidi wapigwe. Kwanza kitendo cha kupost kupitia facebook nyumba zilizochoka za Keko na kuonesha eti wamedhamiria kupost uwanja wametudhalilisha sana.
Yaani picha 75% inaonesha makazi yaliyochoka na 25% kwa juu ndio inaonesha uwanja.
 
Hii comment imenifanya nikachungulie hiyo picha 😂😂
 
Hawa Al Ahly inabidi wapigwe. Kwanza kitendo cha kupost kupitia facebook nyumba zilizochoka za Keko na kuonesha eti wamedhamiria kupost uwanja wametudhalilisha sana.
Yaani picha 75% inaonesha makazi yaliyochoka na 25% kwa juu ndio inaonesha uwanja.
Kumbe ndo wamefanya udhalilishaji huo? She*#@nzy zao kabisa! Lazima tuwafundishe adabu kesho.
 
Kwani mechi ya Simba vs Al ahal ni lini?..... maana ninachojua 30/3/2024 kutakua na mechi baina ya bingwa wa Tanzania na bingwa wa South Africa.
 
Kumbe ndo wamefanya udhalilishaji huo? She*#@nzy zao kabisa! Lazima tuwafundishe adabu kesho.
Hawa watu wanadharau sana
FB_IMG_1711650778437.jpg
 
Back
Top Bottom