Mkuu najiuliza kama mimi ningekuwa CCM ningefanya nini. Nisingekubali kushindwa, lazima nigefanya kila ninaloweza nisiabike hasa katika kipindi kama hiki ninapokuwa na kashfa. Na ukiangalia hesabu wa tofauti ya kura inaruhusu kucheza rafu hiyo. Kama Jeshi ni lako, polisi ni wako, usalama ni wako na above all tumeya uchaguzi ni yako, kwanini usifanye ujanja? Tujaribu kujiweka kwenye nafasi ya CCM ili tuweze kuona kwa nini wanafanya wanachofanya, kama kweli wamefanya hivyo.
Aleluya!
Ninachoona mimi CCM watangaze Utawala wa Chama Kimoja kwani hawataki kushindwa!
Kulikoni kwahadaa mataifa kuwa Tanzania kuna Democrasia ya Vyama vingi! Period!
Mungu wetu na atusaidie!
Sisi watu huru tunaomba kuuliza maswali
mtu uko kwenye computer ni kipi kimekufanya ujiridhishe kuwa ccm wamewaibia chadema kura??
Sasa kipi washindwe maana kila wakati wanapanga mikakati ya kishetani ya kuiba kuraUshabiki tu hakuna lolote
Sasa kipi washindwe maana kila wakati wanapanga mikakati ya kishetani ya kuiba kura
Yaani utawala wa Kishetani kazi yake kubwa ni kudhulumu watu hata kile kichache za maskini kama vile uchaguzi wa biharamulo vileNa sasa wameanza kuleta mambo ya kidini ili kupoteza malengo yao ya kishetwani.
Tulia............Tafakari.........Mmiliki wa Timu ni Refa, wewe unatarajia nini hapo mbona mnajifanya mnashang'aa na wakati kilichokuwa kinatokea hahitaji ukawa na degree kukiona. Na mkubali sana nyerere aliwajua watu wake nakuambia hii cheni ya ujinga Tanzania itabaki hivyo hivyo
Mpaka Yesu Aje au Mtume!
Mkuu ni kigezo gani umekitumia kuamini hivyo ,mfano hukuwepo B'mulo lakini bado unaamini umeibiwa ni stds zipi mnatumia?
Mnipe Desa mnalotumia na mimi nijifunze jinsi stds hizo zinavyotumika.
Yaani utawala wa Kishetani kazi yake kubwa ni kudhulumu watu hata kile kichache za maskini kama vile uchaguzi wa biharamulo vile
Mkuu Invisible,
Mimi naona unisaidie, hivi haya matokeo uliyokuwa unabandika ulikuwa unayatoa wapi? Una uhakika 100% kwamba yalikuwa ni matokeo ambayo yamebandikwa vituoni? isije ikawa ni matokeo ambayo unapewa na wafauasi wa vyama ambao wako tayari ku spin jambo lolote.
Ningependa kujua nini kimetokea, na je ni kweli kwa kura za kila kituo CHADEMA walishinda?
Kwenye mambo ya uchaguzi inatakiwa kuwa makini sana kabla ya radio/TV kutangaza ushindi.
Kama ni kweli CHADEMA walishinda na wameibiwa basi nawaonea huruma. Isije ikawa kama ya Iran ambayo hata watu wa West wenyewe wanaamini huyu rais ameshinda ila vijana walikuwa wanataka mabadiliko wakawa tayari kutumia kila njia ili ku take advantage of the situation.
Binafsi ningependa kweli kujifunza CCM wanatumia mbimu zipi kuiba? Hivi hakuna wana CCM hapa wanaotaka ku spill the beans? Yaani vyama vya upinzani mmeshindwa kabisa kuiba siri za CCM?
Tanzania si nchi ya amani tena,kwani sasa hivi mioyo ya watanzania haijatulia kwa sababu ya ccm,wameshindwa kusoma alama za nyakati kuwa Watanzania wa sasa si wa miaka ya 80 na 90,taratibu fundo la uchungu wa watanzania linajaa,ipo siku litafumuka na hapatakalika.Hakuna aliyezaliwa akamilikishwa amani,amani inatafutwa na inatunzwa.
Mi inaniuma sana.
Inatia huruma sana kuona chama hicho kikongwe kinajigamba kuwa wanashinda kumbe ushindi ni wa kishetani kama hivi tunavyoona kuwa ni ushindi wa nguvu za giza huku Tume ya Taifa ikibariki maovu yaoTanzania si nchi ya amani tena,kwani sasa hivi mioyo ya watanzania haijatulia kwa sababu ya ccm,wameshindwa kusoma alama za nyakati kuwa Watanzania wa sasa si wa miaka ya 80 na 90,taratibu fundo la uchungu wa watanzania linajaa,ipo siku litafumuka na hapatakalika.Hakuna aliyezaliwa akamilikishwa amani,amani inatafutwa na inatunzwa.
Mi inaniuma sana.
hivi limekaaje hili la wakurugenzi wa halmashauri/miji waajiliwa wa serikali za mitaa zilizo chini ya ofisi ya waziri mkuu kuwa wasimamizi wa uchaguzi kwenye majimbo? Je kweli tume ya Uchaguzi itakuwa huru hapo? Kuna makamishina wangapi kwenye Tume ya uchaguzi toka vyama vya upinzani?