Matofali 10 ya ndoa bora

Matofali 10 ya ndoa bora

Void ab initio

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2015
Posts
5,723
Reaction score
5,662
Matofali 10 ya ndoa bora!

1.Lazima ujue kwamba wewe ni mke na ni wajibu wako kushuka na kumtii mumeo “enyi wake watiini waume zenu kama kutaniko linavyomtii Kristo Yesu”

2.Lazima ujue kwamba mumeo ni kiongozi wako, haijalishi uko smart kiasi gani, mume anabaki kuwa mume… hata ukiwa rais wa nchi, ukirudi nyumbani unakuwa mke wa mtu; hapo elimu, nafasi, cheo, umaarufu havifanyi kazi.
“mume ni kichwa cha mkewe… hata kama kichwa hakina akili bado ni kichwa, na unadhirisha usivyo na akili zaidi kwa kukubali kuolewa na mjinga… umeshaolewa, umegundua ni mjinga, ishi naye kwa akili na msaidie kujua nafasi yake na muache akae kwenye nafasi yake”

3.Usiwe mjinga kiasi cha kutoka nje kwenda kueleza mapungufu ya mumeo; midomo ya wanawake wengi imevunja ndoa zao… hao mashoga, marafiki, ndugu zako watakusikiliza ila hawatatatua shida zako bali watachangia kuibomoa.
“mwanamke mpumbavu huibomoa nyumba yake kwa mikono yake mwenyewe”

4.Simama kidete na umlinde mumeo anaposhambuliwa… chako ni chako hata kama kina mapungufu… mtetee mumeo mbele za watu na mkosoe mnapokuwa wawili chumbani. “naye abigaili akamwangukia daudi akamfichia mumewe aibu na kumlinda asiuawe”

5.Mumeo akitoka nje ya ndoa kutafuta nyumba ndogo, kabla ya kutafuta pepo aliyemwingia, tafuta mlango ambao huyo pepo ameutumia… inawezekana ulipokuwa single ulikuwa unajipenda, unapiga pamba mpaka basi, umeolewa unajivalia kivyovyote [shauri yako]; inawezekana ulipokuwa hujampata lugha yako ilikuwa super, lakini sasa unajibu unavyojisikia [shauri yako]; inawezekana ulipokuwa hujavaa pete ulikuwa unawapenda na kuwathamini ndugu na wazazi wake, lakini ulipoingia tu, ndio umeona karaha ya mawifi na ndugu wa mume [shauri yako]… inawezekana ni kitandani [biblia inasema mke hana umiliki juu ya mwili wake isipokuwa mumewe] usisahau hii ni ya muhimu sana, ukisema anakuchosha “kwa kukujia mara kwa mara” [shauri yako]!
“Mungu amefanya jambo jipya duniani ya kwamba mwanamke atamlinda mwanaume”

6.Usisahau kwamba ni wajibu wa mke kuamka kabla usiku haujaisha na kupiga kazi zote za muhimu ndani… biblia imesema hili, mithali 31 [biblia haisemi ni kazi ya house girl; ukimpa house girl azipige umempa nafasi ya kuwa mke badala yake, maana ni kazi za mke mwema hizi]
“mke mwema huamka kabla usiku haujaisha ili kuweka sawa mambo ya nyumbani mwake kwa siku inayoanza baada ya usiku huo”

7.Ni lazima mke awe na kitu cha kufanya… ukiwa tu golikipa, hakuna viungo wala mabeki kukulinda utafungwa magoli.
Mke ambaye ana akili nzuri lazima awe na kitu cha kuingiza kipato…afanye kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kutunza watu wa nyumbani kwake, Mithali 31 iko wazi kama unataka ndoa yako isimame, ukikwepa imekula kwako!
“mke mwema hufanya kazi kwa mikono yake mwenyewe, na kuwapa chakula watu wa nyumbani kwake”

8.Mke mwenye hekima anaulinda uhusiano na mama mkwe [hii ni zawadi ya pekee kwa mumeo], moyo wa mtoto wa kiume humpenda na kumjali mama, usisahau hii itakusaidia, ni silaha muhimu ya vita!
Soma kitabu cha Ruthu utaona Ruthu alivyocheza kete zake vizuri na kuuteka moyo wa mama mkwe. “mke mwenye busara huhakikisha anauteka moyo wa mumewe kwa kuwa kipenzi cha mama mkwe”

9.Mke mwenye busara anajua ya kwamba ni jambo moja kuwa mzazi [mwanamke aliyezaa] na ni jambo jingine kuwa mama.
Kuzaa ni kuporomosha kiumbe baada ya miezi 9 aliyoweka mungu lakini kuwa mama kunategemea malezi sahihi na bora yatakayoweka msingi mwema na bora usiofutika kwa mwanao. “mke mwema humlea mtoto wake katika njia impasayo ambayo hataiacha hata atakapokuwa mzee”

10.Mke mwenye hekima huuweka moyo wake kwa mungu: huku ndiko anakoeleza mapungufu yake, mapungufu ya mume wake, na kukabidhi ndoa yao kwenye mikono salama na makini ya Mungu. Mungu anaweza kubadili chochote ambacho wazazi, washenga au washauri wa ndoa hawawezi kugeuza au kutatua.
“mke mwema hufunga na kuomba kwa ajili ya mumewe, ndoa na familia yake… ni rafiki wa uwepo wa Mungu”
 
Mkuu unaongea na cm au unaongea na nan? Kama ndo hawa wanawake wetu wa sikuhiz umepoteza mda wako tu bure kuandika yote haya
 
Somo zuri kwa walio kwenye ndoa.
Hata wewe ambaye hujaingia kwrnye ndoa ni somo zuri sana maana linakujenga siku ukiingia tayari unajua nini cha kufanya.

pia ni somo baya kwa waliotoka na hawatarajii kurudi maana linawaumiza nahawana second chance ya kurekebisha makosa ya huko awali walikokosea.
 
Sawa mkuu.
 
Ndoa bila Mungu ni ndoano. Kuna wakati mwanandoa anatamani kutulia na familia yake lakini msukumo wa kutenda mabaya unamshinda.
Kimbilio ni kwa Mungu. Ukipata muda jifunze kitu kupitia video hii
 
Hivi ndoa ni mwanamke tu anatakiwa ku-give. Unaongelea matofali ya ndoa bila kuongelea wajibu wa mwanaume kwenye hiyo ndoa. Kama ndoa ni muunganiko wa watu wawili na ili habari yako isionekane inakandamiza au kupendelea upande mmoja ulitakiwa kuelezea wajibu wa mume na mke. Vinginevyo habari yako ni ya kiupendeleo na INAYOMGANDAMIZA mwanamke. INAYOMFANYA MWANAMKE aendelee kuteseka na kunyanyasika na hayo unayoyaita matofali ya ndoa. Na pia unakuwa si ubinadamu iwapo mwanamke ataonekana ni mtu wa kutoa tu bila kujali hisia zake
 
Basi si useme au upingane kwa hoja mkuu?!! Kama huwashauri wanawake kugive unatakaje?!!
 
Shughuli hiyo!!!
 
Mkuu unaongea na cm au unaongea na nan? Kama ndo hawa wanawake wetu wa sikuhiz umepoteza mda wako tu bure kuandika yote haya
Pole sana. Mke mwema anatoka kwa Mungu. Ampatae mke apata kitu chema.
Kama uliyempata ni kimbunga inamaana huyo sio wa kwako na huenda ulimpata pasipo kumwomba Mungu akupe.
Mpelekee huu uzi asome anaweza kubadilika na ukampenda, kama unaye mke na sio girlfriend
 
Basi si useme au upingane kwa hoja mkuu?!! Kama huwashauri wanawake kugive unatakaje?!!
Mtoa post kasema matofali ya ndoa nilikuwa namtaka aweke balance kwani ndoa ni ya watu wawili. Ngoja nitafute mistari ili nami niweke mizania .Kwa ambao wana ijua biblia vizuri nao waje hapa
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom