Siyo mihula bali alifanya kuwe na Backlog ya kujiunga na UDSM.
Mkuu
Mwita Maranya ni vyema kwa kweli tukapata habari kamili za huyu jamaa pamoja na hata picha ikiwezekana. Mtu kama huyu ambaye alikuwa maarufu wakati ule na kisha kukawa na habari kwamba alikuwa kichaa kisha aktangulia mbele za haki, basi maneno tu yanakuwa hayatoshi. Tupate ushahidi zaidi.
Mkuu
Kashishi habari za Bazigiza nazo zimekuwa kama za Matiku Matare. Kuna tetesi zilizagaa kuwa alionekana huko Ngara kisha akatangulia mbele za haki. Kama hawa jamaa wapo ni vyema wakajitokeza na kutuambia kama kweli bado wapo. Pia wanaweza hata kuandika kitabu kuhusu ule mgomo na jinsi walivyouendesha kwa ajili ya historia tu ya UDSM pamoja na nchi kwa ujumla. Ule ulikuwa mgomo mama wa migomo yote tangia UDSM ianzishwe na siamini kwa hali ya sasa kama mgomo kama ule unaweza kutokea tena. Miaka zaidi ya 30 sasa kila kitu kinaweza wekwa wazi na wanaoweza kuweka wazi kila kitu ni pamoja na Matiku, Bazigiza, jamaa mmoja akiitwa Sarungi na wengine kadhaa. Imani yangu ni kwamba mgomo ule ulikuwa ni mikono mingi na si ajabu hata wanasiasa walikuwemo.