Matiko akiri kumiliki silaha

Matiko akiri kumiliki silaha

Makanyaga

JF-Expert Member
Joined
Sep 28, 2007
Posts
11,544
Reaction score
7,484
Matiko akiri kumiliki silaha
Najiuliza swali fikirishi kwamba ni nini cha ajabu huyu mtu kumiliki silaha, kwa hadhi yake kama mbunge?

=====
Matiko akiri kumiliki silaha
1575964753907.png

Alidai mahakamani wakati akitoa ushahidi wake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, baada ya kuhojiwa na Jamhuri dhidi ya utetezi wake.

Shahidi huyo aliongozwa na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala.

Akihojiwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Wankyo Simon, mshtakiwa huyo alidai kuwa ingawa anamiliki silaha hiyo hajawahi kuitumia wala hakumbuki kama iliwahi hata kufyatuka mahali popote.

Alidai wakati akiongozwa na Wakili wa utetezi, Kibatala kuwa katika kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge Jimbo la Kinondoni, alipewa jukumu la kufuatilia nakala za viapo na barua za utambulisho wa mawakala.

Alidai kuwa yeye ni mkazi wa Tarime Mjini, Februari 15, 2018 alipofika Dar es Salaam, aliwasiliana na mmoja wa viongozi wa kamati ndogo ya uchaguzi, Benson Kigaila kwa simu kumfahamisha kuwa amefika.

"Aliniteua mimi na Mbunge wa Viti Maalum, Susan Lyimo, kufuatilia barua za utambulisho pamoja na hati za viapo vya mawakala," alidai Matiko.

Akifafanua zaidi alidai kuwa walianza kufuatilia barua hizo Februari 16, 2018, saa nne asubuhi walikwenda kumuona Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni ambaye ndiye alikuwa msimamizi wa uchaguzi huo ili awasaidie kupata barua hizo.

Alidai kuwa walifika ofisini kwa Mkurugenzi na kuambiwa wasubiri mpaka walipoonana naye saa saba mchana, lakini aliwaambia anashughulikia jambo hilo hivyo wasubiri mpaka saa 12 jioni.

"Tulisubiri mpaka saa 12, lakini hatukufanikiwa kupata barua hizo na mkurugenzi aliwahakikishia watapata mpaka kufikia saa moja usiku wa siku hiyo," alidai na kuongeza:

"Tulipewa namba za simu za msimamizi wa uchaguzi na msaidizi wake na kuendelea kuwasiliana na msimamizi msaidizi wa uchaguzi aliyemtaja kwa jina la Victoria Charles, mpaka saa tano usiku na kwamba alionekana kutingwa na kazi ya kusambaza vifaa vya uchaguzi hivyo akashindwa kumpatia barua hizo na kumwahidi kuwa atawasiliana naye saa 11 alfajiri ya Februari 17, 2018 ambayo ndiyo ilikua siku ya uchaguzi," alidai Matiko.

Alidai kuwa mpaka kufikia saa 11 alfajiri barua na nakala za viapo hivyo zilikuwa hazijapatikana, alitoa taarifa kwa msimamizi wa uchaguzi na baadaye kwa viongozi wa kamati ndogo ya uchaguzi na jukumu lake likaishia hapo.
Mbali na Matiko, washtakiwa wengine ni Mwanyekiti wa Chadema Freeman Mbowe, Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Salum Mwalimu, Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, Mbunge wa Kibamba John Mnyika na Mbunge wa Bunda, Esther Bulaya.

Pia wamo Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk. Vincent Mashinji.



Chanzo: Nipashe
 
Hakuna kosa hapo mbona hata mimi najisiki na niko chuo mwaka wa kwanza cha msingi ni namna ulivyomilikishwa
 
silaha ya nini kwa mtoto wa kike? akivamiwa ataweza kuitumia au atapiga kelele tu? atubu dhambi za kumsaliti mumewe na kuzaa na salum mwalimu
 
Kakiri au kakubali kwamba anamiliki silaha?
Unanikumbusha salaamu za Mzee Rukhsa jana kwenye sherehe za miaka 58 ya Uhuru. Aliiambia hadhira ya wa-Tanzania waliokuwepo uwanja wa CCM Kirumba akasema NAKUPONGEZENI, SIYO KWAMBA NAWAPONGEZA, NAKUPONGEZENI! Mzee huyu jana alipelekea nikumbuke kuwa mimi ni msukuma, Kiswahili ni lugha yangu ya pili. So, is you!
 
Unanikumbusha salaamu za Mzee Rukhsa jana kwenye sherehe za miaka 58 ya Uhuru. Aliiambia hadhira ya wa-Tanzania waliokuwepo uwanja wa CCM Kirumba akasema NAKUPONGEZENI, SIYO KWAMBA NAWAPONGEZA, NAKUPONGEZENI! Mzee huyu jana alipelekea nikumbuke kuwa mimi ni msukuma, Kiswahili ni lugha yangu ya pili. So, is you!
"So is you".

Kiingereza ni lugha yako ya ngapi?
 
Hakuna kosa hapo mbona hata mimi najisiki na niko chuo mwaka wa kwanza cha msingi ni namna ulivyomilikishwa
Kumiliki silaha kisheria siyo kosa, na ni kitu cha kawaida kabisa hasa kwa viongozi wengi wa ngazi kama ya huyu mama. Tatizo liko hapa kwamba, kwa mfano wewe uko na njaa, ukaamua kwenda kwenye mgahawa kula chakula, halafu ikaja ikatokea huko mbele ya safari mtu akaja akakuuliza swali kuwa kwa nini ulikula chakula, wakati kila mtu anajua fika kabisa kuwa mtu kula chakula ni kawaida pindi unapokuwa ana njaa, sijui unanielewa? Italeta mantiki tu iwapo tu katika mazingira hayo, mtu atakuuliza kwa mfano kuwa, kwa nini ulikwenda kula mgahawa A na si mgahawa C?
 
"mwanamke ni kiumbe ambaye anaweza kufwatwa na wanaume asiowafahamu na bado asitoe taarifa polisi"..
 
Asilimia 100 unaijua ni kitu gani?
Instead of discussing the marginals, may you please stick to the topic of the thread, if at all, there are (still) any contributons from you?, Please!
 
Instead of discussing the marginals, may you please stick to the topic of the thread, if at all, there are (still) any contributons from you?, Please!
Kama hayo maswali ninayokuuliza kuhusu habari ulizoleta wewe ni marginal, nani kaleta marginals?

Mimi au wewe?
 
Kama hayo maswali ninayokuuliza kuhusu habari ulizoleta wewe ni marginal, nani kaleta marginals?

Mimi au wewe?
I would better change my phrase to,...Instead of sticking to the marginals......, .
 
Back
Top Bottom