Matibabu ya Kikwete yazua balaa Bungeni

Matibabu ya Kikwete yazua balaa Bungeni

suala hili la viongozi kutibiwa nje linawaumiza na kuwatesa watanzania,kwasababu kamwe hawatafikiria kuboresha hospitali zetu kwa kununua vifaa vya tiba vya kisasa maana wao hawahusiki na bahati mbaya hawawajali kabisa wananchi,hakika ni wanyonyaji,pesa wanazotibia nje ni kodi za wananchi,waboreshe basi hospitali zetu ili wawe wanatubiwa hapahapa,au basi wananchi wanapougua magonjwa magumu nao wapelekwe nje na serikali,setikali hii haiko fair kabisa;
ona mkuu wa kaya yeye kaenda usa huku kwetu kaacha hospitali hazina matibabu,du!maana yake ni kwamba wananchi mtajijua.
 
  1. Prostatitis - infection or inflammation of the prostate gland. Prescription drugs are the most common form treatment but the condition constantly reoccurs.
  2. Benign Prostatic Hyperplasia (BPH) - non-cancerous growth of the prostate gland. When the gland becomes too large it will require surgery.
  3. Prostate Cancer - the second most common cause of death in men. Surgery, chemotherapy and radiation are the most common methods of treatment for prostate cancer.

Let's face it, your prostate won't heal itself and if left alone, those problems CAN and WILL get a lot worse.
Wouldn't it feel great to know that you can stop the worry, frustration and discomfort of your enlarged prostate? The revolutionary all-natural formula, Everest Nutrition Prostate Plus™, can restore your prostate health and might even save your life!
Unaongelea prostate. Wao tangu juzi wanasema prostrate. Sijui wewe ndiye umekosea au kuna kitu wameamua kuficha!
 
Wapemba wa CUF ni wajinga sana SEIF akienda kutibiwa Oman na India sawa.JK ameenda marekani wanalialia.
 
Mkuu UTHUBUTU bila matendo ni wehu! Uthubutu unatakiwa uwe kwenye matendo na sio kwenye maneno.

Nakubaliana nawe.Ila kessy amejaribu kwa maneno,Mimi nawe tumebaki na ndio Mzee huku.Tukilalamika bila kuchukua hatua yoyote.Nafikiri hatujachelewa tufikiria njia bora ya kugoma kuburuzwa.
 
Ataenda kufanya nini wakati yeye ni Mtanzania? Kuna nini zanzibar cha kumpeleka wakati hata kwenye serikali ya Muungano haimo?

Ombi langu Watanzania tusirudie tena kuwa na raisi mshereheshaji kama kikwete. Miaka kumi Tz haijawa na raisi na ndiyo maana sasa watu wanaanza kujichukulia sheria mfukoni. Hivi bunge la enzi za Mwalimu, kweli wabunge wangeweza kunyanyuka kwenda kumpiga mbunge mwingine bungeni? Huu ni mzaha. Na tatizo hili lllimekomaa ccm wanapigana katika kila chaguzi zao na sasa wameanza kupiga hata wazee waasisi wa taifa.

Ccm hawafai tena. Hawana uwezo wala sifa ya kuongoza nchi hii.

Huyu jamaa asije akatia mguu huko visiwani
 
BUNGE wa Nkasi Kaskazini, Ally Kessy (CCM), kwa mara nyingine tena, jana alinusurika kichapo kutoka kwa wabunge wa Chama cha Wananchi (CUF), baada ya kuwapasha kwamba wanatibiwa nchini India, kwanini wanahoji Rais Jakaya Kikwete kutibiwa Marekani.

Kessy alizua kizaazaa hicho wakati Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai alipokuwa akijibu miongozo mbalimbali ya wabunge, ukiwemo wa Kessy.

Mbunge huyo ambaye sasa ni mara ya tatu kukwaruzana na wabunge wa CUF kutoka Zanzibar, aliomba mwongozo wa Spika na alipopata nafasi alihoji sababu ya wabunge wa Zanzibar kuhoji matibabu ya Rais Kikwete aliyefanyiwa upasuaji nchini Marekani wakati wao wamekuwa wakitibiwa India kwa gharama za Serikali.

“Mheshimiwa Spika, hawa Wazanzibar wanaohoji Rais Kikwete kutibiwa India, wanakosea sana, mbona wao wanatibiwa India, hatusemi kitu. Nawajua wabunge zaidi ya sita waolitibiwa India, kuna kosa gani Rais Kikwete kutibiwa Marekani, au mlitaka akatibiwe Zanzibar, kwendeni zenu huko,” alimalizia kwa kusema Kessy na hivyo kuibua kizaazaa.

Kauli hiyo ya Kessy iliwaibua wabunge wote wa kambi ya upinzani ambapo baadhi yao walipaza sauti kutaka atolewe bungeni, lakini wabunge wengine wa CUF, wakiongozwa na Khatibu Said Haji (Kondo), walinyanyuka kwenye viti vyao na kumfuata kwenye kiti chake.

Lakini kabla ya kufikiwa, Kessy alisimama na kuchomoka kwa kasi kutoka nje, huku askari wa Bunge wakiwazuia wabunge wa CUF waliokuwa na jazba wasimfuate.

Mbunge wa Tabora Mjini, Ismail Aden Rage (CCM), alifanya kazi kubwa kumzuia mbunge wa Kondo, Khatib ambaye alionekana dhahiri kupania kumtandika Kessy.

Kabla ya Kessy kuanzisha sarakasi hiyo, mbunge wa Viti Maalum, Rukia Kassim Ahamed (CUF), aliomba mwongozo wa Spika kutaka Bunge lisitishe kujadili Mapendekezo ya Serikali ya Mpango wa Taifa mwaka wa fedha 2015/2016 ili lipate nafasi ya kujadili deni la Serikali la zaidi ya sh bilioni 100, linalodaiwa na Bohari ya Madawa nchini (MSD), na kusababisha uhaba mkubwa wa dawa kwa wananchi nchini.

Mbunge huyo alisema hakuna sababu ya wao kuendelea kukaa bungeni na kupigwa kiyoyozi huku Rais Kikwete akienda kutibiwa Marekani wakati wananchi vijijini wakipoteza maisha kwa kukosa dawa, kauli ambayo ilimuibua Kessy na kujibu mapigo.

Hii ni mara ya tatu kwa Kessy kutibuana na wabunge wa Zanzibar na kuzua kizaazaa. Mara ya mwisho ilikuwa katika Bunge Maalum la Katiba ambapo mbunge huyo alisema Zanzibar inabebwa katika masuala la Muungano na kwamba haichangii chochote.

Kauli kama hiyo alishawahi kuitoa katika Bunge la Bajeti ambapo alisema Zanzibar inainyonya Tanganyika na kwani haichangii chochote katika masuala ya Muungano, kauli ambayo mara zote imekuwa ikimletea matatizo na wabunge kutoka Zanzibar ambao wanadai ni ya kibaguzi.

Rais Kikwete, amefanyiwa upasuaji wa tezi dume (prostate), katika Hospitali ya Johns Hopkins iliyoko Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani.

Taarifa iliyotolewa na Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu kwa vyombo vya habari juzi ilisema Rais Kikwete amefanyiwa upasuaji huo juzi alfajiri baada ya madaktari waliomfanyia uchunguzi wa afya yake kujiridhisha kuwa alikuwa anahitaji matibabu ya aina hiyo.

Inaelezwa kuwa upasuaji huo ulichukua kiasi cha saa moja unusu, umefanyika salama na kwa mafanikio makubwa na wananchi wataendelea kupewa taarifa sahihi kuhusu hali ya Rais kwa kadri zitakavyokuwa zinapatikana.

Afya ya JK yaimarika

Kwa mujibu wa taarifa ya Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu jana, hali ya Rais Kikwete inaendelea kuimarika na kuwa nzuri huku akiwa ameanza kufanya mazoezi ya kutembea tangu juzi.

“Rais Kikwete ameanza kufanya mazoezi ya kutembea siku ya pili tu baada ya kufanyiwa operesheni. Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais, Ikulu, itaendelea kuwapatia wananchi habari sahihi kuhusu maendeleo ya afya yake kadri habari hizo zitakavyokuwa zinapatikana,” ilisema taarifa hiyo.

Pia, Ikulu iliwashukuru wote ambao wamekuwa wakimwombea Rais Kikwete ili apone haraka na kurejea nyumbani kujiunga na wananchi wenzake katika ujenzi wa taifa.

Chanzo:Tanzania daima

tetrtetetete
 
Angalia wapuuzi wa Lumumba walivyorukia uzi kama vile walikuwa MSALANI sasa wamekurupushwa wametoka bila kunawa na kutuletea harufu zao za .......,yaan uzi wote unanuka kilumumbalumumba tu!!!
Watu wenye harufu ya kinyesi kama wewe hawajifichi.
Badala ya kutumia akili unatumia kiungo kisichoonyeshwa hadharani.
 
Suala hili linaegemea kwenye imani zaidi na limegawanyika katika maeneo matatu.
1.Eneo la kwanza ni la waislam ambao hawaridhishwi na utawala wa Kikwete na wamekuwa wakisoma dua mbaya misikitini.Hapa inaweza kuaminika kwamba karushiwa ule ugonjwa wa kipwani wa mamwinyi(tezi dume).Kibaya zaidi ni kuteswa na kudhalilishwa kwa masheikh kama akina Ponda na Uamsho.
2.Ni kwa upande wa Wakristu ambao wanaamini Kikwete ni mdini na wamekuwa hawakauki kwa matamko ya kuiponda serikali na kuitabiria anguko baya
3.Ni kwa makada na waumini wa kawaida toka pande zote wanaoamini kwamba ugonjwa wa Raisi ni wa kawaida kama ambavyo ingeweza kumtokea mtu mwingine yeyote na haihusiani na dua mbaya za wanadini na wasiompenda.
 
Uzima na ugonjwa yote ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Acha kupotosha watu
 
Alaumiwa mama watoto. Nikitakiwa kuleta sababu niko tayari, naachia nafasi wajumbe wenhine
 
Uzima na ugonjwa yote ni majaaliwa ya Mwenyezi Mungu. Acha kupotosha watu

lizabon ww ni msengerema,kwahyo huw unapochangia habar za lowassa kwamba ni mgonjw huw unajitoaga akili,lakin jk akiugua ni mipango ya Mungu,we farara kweli
 
tezi dume mara nyingi inasababshwa na kufanya sana ngono hasa na wanawake tofaut, nadhan tabia ya jk unaijua ktk hili
 
Hahahahahaaaaa ugonjwa wa Profesori umekua gumzo sana, Mzee wa tezi Dume!!! Kwanini juzi hawakutangaza tukameze dawa za kuzuia tezi Dume badala yake wakasema busha?
 
Akili zako kama za kuku tu ngoja siku moja uamke unaumwa ndiyo utajua mipango ya mungu ilivyo.
 
Hahahahahaaaaa ugonjwa wa Profesori umekua gumzo sana, Mzee wa tezi Dume!!! Kwanini juzi hawakutangaza tukameze dawa za kuzuia tezi Dume badala yake wakasema busha?
Mkuu akili yako inatofauti gani na huyu mtu.
 

Attachments

  • image.jpg
    image.jpg
    37 KB · Views: 130
Back
Top Bottom