Matibabu ya ceragem tanzania

Amina Thomas

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
272
129
Kuna wakorea ambao wanatibu maradhi mengi sana kwa kutumia mazoezi pamoja na mashine za umeme hapo mwenge karibu na ITV mama yangu anaenda huko kila siku.

Hua namsikiliza kwa makini sana kuhusu matibabu hayo, anaondoka saa 12 asubuhi kila siku, anarudi saa tisa u nusu kwa sababu watu ni wengi sana kiasi kwamba wengine wanaenda saa kumi alfajiri.

Wanaanza kwa mazoezi ya viungo halafu wanaenda kwenye hizo mashine za umeme, wanavaa suruali na t. shirt nyeupe tu. mashine hizo zina toa joto ambalo wanasema linatibu kisukari, busha, ugumba, u bubu, kupooza, vivimbe vya kila aina vikiwemo vya saratani, pamoja na magonjwa mengi sana mengineyo.

Kwa upande wangu naona imekaa ki loliondo maana kila siku watu kibao wanatoa ushuhuda. halafu ni buree!. hivi serikali inafahamu kuhusu hili?

Habari zenu wannajamvi..naomba kuuliza juu ya hawa wakorea wenye kituo cha seragem..je? zile mashine zao zinasaidia?. Yoyote mwenye uthibitisho wa kuona aje hapa anihakikishie..

Nina binti yangu ana 1.8 year.. alipata homa ya uti wa mgongo kwahiyo ikimsababishia celebral palsy. so mpaka sasa hawezi kukaa, shingo haijakaza, hawezi kushika kitu chochote..huwa nampeleka kwenye physiotherapy muhimbili na CCBRT. Improvement ipo kwa mbali namimi sijakata tamaa bado naamini ata improve.

Sasa nimesikia kuwa hawa seragem wana mashine nzuri zinazotibu kupitia uti wa mgongo kwa hivyo mnijuze kwa wale mliowahi kuona kwa macho kwa jirani. ndugu, jamaa, rafiki ama wewe mwenyewe..
 
Mumy..... Hujangundua eeeeh? Wanatangaza biashara hao na inawezekana kuna aliyekoserikalini anashare nao mumy amka tanzania sivyo uijuavyo
 
ni mwenge. ukifika kituo cha itv, unashuka na bara bara ya kwenda viwandani. ukienda mbele kidogo kuna njia inakata kushoto. majengo yake yana bati za bluu. hata ukiulizia ceragem unafika. ni maarufu sana.
 
Jamani, this is called Ceragem ... hata mimi baada ya kuisikia ikabidi nifanye utafiti binafsi. Kwa asilimia kubwa it works .... unajua mwili wa binadamu uko very complex na sehemu kubwa ya matatizo yetu yanatokana na failure ya tissues, cells n.k. Sasa hizi mashine zina-activate hizo cells na tissues na kisha wanasisitizia mazoezi. To me it is not Loliondo ...

You can google for Ceragem. Ulaya hii kitu inaonekana ipo sana tena wana vimashime vidogo majumbani lakini hapa kwenu kila kitu kinakuwa kigeni ..... Mungu ibariki Tanzania.
 
Nyingine imefunguliwa Ubungo, nyuma ya stand ta mkoa. Hata mie nina mashaka nayo. Ukihoji kuhusu ule umeme wanaochomewa unaambiwa ni miale ya jua na si mionzi. Nashindwa kuelewa kabisa.

Ukianza matibabu haya siku za mwanzo ni lazima uumwe sana. Unatakiwa kuchomwa kila siku mara tatu kwa mwezi mzima mfululizo, then unaweza ukawa unachomwa kila baada ya siku moja. Umeme, mashine, huduma vyote vinatolewa bureeeee!
 
Kama kawaida yetu Watz tunaingizwa mkenge na hawa Orientals. Time will tell
 
Yap mimi ni mhanga my friend alimsimulia my mum.Akaanza hayo mazoezi two months ago. Imekwenda imefika nimeamua kununua machine Tshs 2.1 Million. Mum anatumia home lakini bado analalamika, anyway ngoja nijipe 1 month nitarudi hapa kuwajuza.
 
Hii inafanya kazi, inatumia infrared radiation, inatibu 90% ya magonjwa yasiyo ya kuambukizwa kwa kufanya tissue repairing
 
Nyingine imefunguliwa Ubungo, nyuma ya stand ta mkoa. Hata mie nina mashaka nayo. Ukihoji kuhusu ule umeme wanaochomewa unaambiwa ni miale ya jua na si mionzi. Nashindwa kuelewa kabisa.

Ukianza matibabu haya siku za mwanzo ni lazima uumwe sana. Unatakiwa kuchomwa kila siku mara tatu kwa mwezi mzima mfululizo, then unaweza ukawa unachomwa kila baada ya siku moja. Umeme, mashine, huduma vyote vinatolewa bureeeee!

Mmh! Kwa nini bure? Running cost anafaidi li nani?
 
Mmh! Kwa nini bure? Running cost anafaidi li nani?
Uliwahi kuuziwa karanga na wale wachuzi wa kikapu mkononi? Yani anachota kama punje tano hivi za karanga anakuonjesha, ukishanogewa tu lazima ununue, sasa ndio modus operandi ya Ceragem ukianza matibabu ni muonjo, baadae unauziwa mashine ukajitibie mwenyewe. Sawa Koku?
 
Mwanahisa, si wangetanganza wanauza mashine? Safari za mwezi mzima kwa mtu aliyepooza ndio nini?
 
Jana nimewaona wanajitangaza tena kwenye kipindi cha wanawake LIVE wako Tabata
 
Mwanahisa, si wangetanganza wanauza mashine? Safari za mwezi mzima kwa mtu aliyepooza ndio nini?
Nafikiri wanawafanyisha watu mazoezi yakuamka asubuhi na mapema bila wao kujua kua ile nafuu wanayopata inatokana na ule mchaka mchaka wa asubuhi. Ila mashine ndio core business hizi nyingine mbwe mbwe tu.
 
Usalama wa hizo mashine je zimethibitishwa hazina madhara kwa binadamu?? Kwa utitiri huu wa bidhaa feki nachelea kuamini hii kitu

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Wamefika Mwanza na Moro wanauza vitanda ndo vinaitwa ceragem pia wanatoa huduma bure na wengine wanatakiwa kulipia
 
Back
Top Bottom