Matibabu ya BP bila Dawa

BabaDesi

JF-Expert Member
Jun 30, 2007
6,032
3,944
Salamu Madakitari wa JF.

Ninaomba kujuzwa: Pamoja na kufanya Mazoezi, ni chakula gani na Tiba asili ipi ninaweza kutumia ili kupona na kuepuka BP bila kulazimika kutumia madawa makali yenye chemical yanayoweza kusababisha tatizo lingine la Figo?

Ninaomba Msaada
 
Tatizo lako n lipi hasa? High blood pressure ama low blood pressure? na itakua vyema kama ukitupa na vipimo vyako 3 vya pressure mara ya mwisho umepima. Tuanzie hapa kwanza
 
BP kuiepuka ni rahisi.. Epuka uzito mkubwa kwa kulaa vyakula visivyo na mafuta...epuka kula ovyo ovyo..achana na sigaraa na pombe iliyozidi..fanya mazoezi lakini kikubwa KATAA STRESS. ukiweza kufata haya BP haitakupata lakini kikubwa ni kuepuka msongo wa mawazo.
 
Salamu Madakitari wa JF. Ninaomba kujuzwa: Pamoja na kufanya Mazoezi, ni chakula gani na Tiba asili ipi ninaweza kutumia ili kupona na kuepuka BP bila kulazimika kutumia madawa makali yenye chemical yanayoweza kusababisha tatizo lingine la Figo?
Ninaomba Msaada
Mkuu fuata ushauri wa MR @rikiboy
Kama alivyo eleza a mimi nitaongeza kuwa kuna dawa ya asili ukivaana aka ukiwa nayo na ukifuata ushauri ulioambiwa hapo juu basi utakuw aumepona kabisa maradhi yako ya presha.

Kinga Dhidi ya Maradhi ya Presha.

Namna pekee ya kujikinga na maradhi haya ni kuhakikisha unachukua tahadhari za kuepuka shinikizo la juu la damu kwa kubadili mfumo wa maisha hasa kwa kupunguza ulaji wa vyakula vyenye mafuta na chumvi nyingi.

Kufanya mazoezi mara kwa mara na kuwa makini na uzito wa mwili pamoja na kuepuka kitambi ni nyingine ambayo itakusaidia kujiondoa kwenye uwezekano wa kupata maambukizi ya shinikizo linaloweza kuua macho yako.

Kwa wenye shinikizo la damu, inashauriwa kumuona daktari bingwa wa macho kwa ajili ya vipimo mara kwa mara. Ni vyema kufanya hivi ili kugundua tatizo mapema kabla ya kupoteza uwezo wa kuona.
 
Tatizo lako n lipi hasa?? High blood pressure ama low blood pressure??...na itakua vyema kama ukitupa na vipimo vyako 3 vya pressure mara ya mwisho umepima. Tuanzie hapa kwanza
...Ni High.. Vipimo vya Mara ya mwisho Wiki kama Tatu zilizopita ni 149/90...na imekuwa inazungukia hapo. Haipandi sana zaidi ya hapo wala haishuki sana zaidi ya hapo.
 
...Ni High.. Vipimo vya Mara ya mwisho Wiki kama Tatu zilizopita ni 149/90...na imekuwa inazungukia hapo. Haipandi sana zaidi ya hapo wala haishuki sana zaidi ya hapo.
walikuambia pressure yako inasababishwa na nini, umepima figo?
 
walikuambia pressure yako inasababishwa na nini, umepima figo?
... walisema inawezekana ni umri tu (61) ambapo ndio imeishakuwa kama ndio BP yako ya kawaida, na uzito ( 91 )....figo IPO fit maana sijapata kuona chochote ambacho kingenipa wasiwasi kuhusu huko....
 
Salamu Madakitari wa JF. Ninaomba kujuzwa: Pamoja na kufanya Mazoezi, ni chakula gani na Tiba asili ipi ninaweza kutumia ili kupona na kuepuka BP bila kulazimika kutumia madawa makali yenye chemical yanayoweza kusababisha tatizo lingine la Figo?
Ninaomba Msaada
Chanzo cha hilo tatizo la BP ni nini?

Maana tiba mujarabu sharti ilenge kiini cha tatizo
 
BP kuiepuka ni rahisi.. Epuka uzito mkubwa kwa kulaa vyakula visivyo na mafuta...epuka kula ovyo ovyo..achana na sigaraa na pombe iliyozidi..fanya mazoezi lakini kikubwa KATAA STRESS. ukiweza kufata haya BP haitakupata lakini kikubwa ni kuepuka msongo wa mawazo.

Mtu anawezaje kuepukana na msongo wa mawazo?
 
Back
Top Bottom