Matibabu kupitia bima ya afya bado kuna usumbufu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matibabu kupitia bima ya afya bado kuna usumbufu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by mmaroroi, Feb 14, 2009.

 1. m

  mmaroroi JF-Expert Member

  #1
  Feb 14, 2009
  Joined: May 8, 2008
  Messages: 2,536
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Wachangiaji wa Bima ya Afya hawapati matibabu sahihi katika vituo vinavyotoa huduma hiyo.Kuna Vituo viwili Kigamboni yaani Navy Dispensary na Kituo cha Afya Kigamboni vimekuwa na usumbufu katika kutoa huduma ya bima ya afya.Bado inaonekana kwamba wanaopata tiba kupitia bima ya afya ni kutibiwa bure,hivyo ni vema wahusika wawaelimishe ili waweze kutoa tiba sahihi kwa wahusika.Kuna watu wengine wamekuwa wakijilipia matibabu ili kuepuka usumbufu wakati wanakatwa fedha kwenye mishahara yao kwa ajili ya bima ya afya sasa hii si ni malipo mara mbili.Bima ya afya iondoe tatizo hili kwa kusimamia vituo vyake na kusikiliza ushauri,maoni na malalamiko ya wadau wa bima ya afya.Wana JF muonyeshe mnavyokerwa na suala hili.
   
 2. bm21

  bm21 JF-Expert Member

  #2
  Feb 15, 2009
  Joined: May 12, 2008
  Messages: 774
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  ............hiyo kitu inayo itwa bima ya afya mimi sitaki hata kuisikia kabisaaaaaaa. Kwanza mtu mwenye bima akienda hospital anaonekana kama bvile anapewa msaada na kwamba anatibiwa bure, kitu ambacho si kweli. Ukweli ni kwamba mtu anaelipa inadvance ili kupata huduma fulani alitakiwa aheshimike na ahudumiwe kwa upendo mkuwa kwani ni mteja ambaye mtoa huduma anaweza kujivunia na kuwana mipango mahususi juu yake. Lakini hili linaonekana ni kama vile msaada. Inafikia wakati unaona bora uende sehemu nyingine ukalipie kuliko kusubiri bima. Maboresho yanahitajika juu ya swala hili.
   
Loading...