Mateso ya watanzania u.s.a

Kweli inauma ila kesi hadi leo hii imeshakamilika Dada huyo kashinda na anatakiwa kulipwa fedha zake zoote. Cha ajabu serikali ndo italipa deni hilo .Fuatilieni muone
 
Inasikitisha, inatisha pia inakatisha tamaa, kumbe viongozi wetu ndo wakatili kiasi hiki? mwisho wa siku mtu kama huyu na kashfa kubwa kama hii, atabidilishiwa kitengo tu, ila hatachukuliwa hatua yoyote
 
Kimsingi huyu mtu alipaswa aachishwe kazi, afunguliwe mashitaka mangine ya kuvunja haki za binadamu na afungwe. Unyama gani huu, tunalalmikia waarabu huko Saudia na U.A.E kumbe tunakwenda mbali mno, unyama tunafanyiana watanzania sisi kwa sisi...Aibu kiasi gani kwa serikali. Shame upo the whole family, shame upon the person who appointed him and all associates in this animal behavior.
 
Hivi hapa Sheria Ikoje?
What if wakisema ni uongo hawakumtendea haya?
Am just curious!!
 
Aliyemtesa huyu ndo sasa kaula kwenye kitengo cha usalama wa taifa. Si sahihi kumpa kazi yoyote mtu wa namna hii. Anastahili kukumbana na sheria.
 
Hii story inaweza kuonekana ya kuhuzunisha sana, but mnaokumbuka hii imeshatoka kwenye magazeti siku nyingi kidogo. Nimepata kuongea na diplomat mmoja na alichosema ni kuwa kwa kawaida hawa ma-housegirls wanaotolewa bongo huwa inakuwa hivi: ili apate viza lazima awe na mkataba unaoeleweka,yaani unakidhi sheria za nchi unayoenda. Sasa kwa kuwa diplomats hawezi kumudu kuajiri housegirl huko ughaibuini, anatafuta mbongo na wanamtengenezea mkataba ili viza ipatikane. Sasa the tricky part ni kuwa wako wanawake wa mataifa ya west Africa na hata kenya, ambao 'huwafumbua macho' hao ma HG wa kibongo na kuwashawishi waende kushitaki...ukitazama hakuna HG hapa Bongo anayelipwa 900USD hata wanaofanya kwenye nyumba za madiplomata masaki, Obay nk..halafu ni jambo la kawaida kwa HG hapa bongo kufanya kazi zaidi ya masaa 12, wanaamka saa 12 asubuhi na kulala saa nne usiku. Sio kawaida HG kuwa anapewa likizo na day off; hii inaonyesha kile nilichoandika hapo juu kuwa mikataba hii purpose yake ni kupata viza. Huyo mwanamke kwa kuripoti suala hilo anajua anapata faida zifuatazo 1)Amnesty, hivyo ataishi marekani kimoja 2) Chance kubwa ya kuvuna kitita cha hela ya kufa mtu!. Kwa hiyo tunapojadili nadhani hoja sio kuteswa Marekani, Ma HG wote wanateseka popote pale tanzania humu humu! Hivyo labda tmjadala uwe je hakiza wafanyakazi kama hawa iko wapi???
 
Aliyemtesa huyu ndo sasa kaula kwenye kitengo cha usalama wa taifa. Si sahihi kumpa kazi yoyote mtu wa namna hii. Anastahili kukumbana na sheria.

Haahahaaa!!
Mlangaja na wengine,
Msisahau kuwa Kitengo cha usalama ni nyeti sana ktk nchi , na nchi yetu hivi sasa iko kwenye kashfa ya ufisadi kwa viongozi wetu wa juu, hivyo mtu kama huyo/hao ni zahiri kupata nafasi katika kitengo hicho ili waweze kukitumikia kitengo hicho kwa kulipa fadhila kwa uongozi uliowateua, hivyo hutakuja sikia kitengo hicho kuigeuka serikali hata kama ni mafisadi.

Bw. Mzengi
Najua kwa kupata nafasi hiyo, umepata kinga ya kushitakiwa, hongera sana!lakini ,
"confenction is always weakness, the greave soul keep its own secrete and take its own punishment in silent". Do that.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom