covid 19
JF-Expert Member
- May 9, 2014
- 8,297
- 20,678
Inaonekana kwa sasa kuna hali isiyo ya kawaida, kana kwamba polisi wetu wanapewa posho au zawadi kubwa pindi wanapoonyesha wamempiga mfuasi wa CHADEMA. ile video inayosambaa ikionyesha mfuasi mmoja aliyefika mahakamani kufuatilia kesi ya Lissu leo akishambuliwa vibaya mno, kana kwamba alikuwa hana utu wala hadhi ya kibinadamu.
Mimi binafsi ni mwanachama wa CCM, lakini sikubaliani kabisa na vitendo hivi. Sioni sababu ya taifa letu kufika kwenye hatua ya ukatili wa namna hii. Pia, kwa hali ilivyokuwa leo mahakamani, sidhani kama kulikuwa na viashiria vyovyote vya uvunjifu wa amani.
Ni wazi kwamba askari wetu wanapaswa kupunguza hasira na kutumia hekima zaidi, kwani vitendo hivi vinatia doa kubwa kwa serikali. Polisi mnapaswa kujikita zaidi katika kutoa elimu kwa raia, kwa sababu elimu ndiyo suluhisho la msingi, na kupiga au kutumia nguvu lazima iwe hatua ya mwisho kabisa. Watanzania wengi ni waelewa, na mara nyingi heshima na maelekezo ya staha hutosha.
Kwa tukio la leo, polisi wameiingiza serikali kwenye fedheha kubwa, hasa katika kipindi hiki nyeti cha uchaguzi. Ni jambo la aibu na linapaswa kuchukuliwa hatua za haraka kurekebisha.