Matendo bila dira ni kupoteza muda, dira bila matendo ni sawa na ndoto za mchana"

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Maneno hayo kwenye kichwa cha mada yangu yaliwahi kutamkwa na kiongozi mkubwa na mwenye heshima hapa Afrika na ulimwenguni, Ndg Nelson Mandela kama sijakosea.

Watu wengi wakiwemo wahenga wetu wamekuwa wakihusisha ndoto za mchana na mambo yasiyoweza kutimia! ki ukweli mimi huwa sielewi kwanini ndoto za mchana!? Je, ni kweli kila ndoto iotwayo usiku hutimia!? Kama si zote hutimia sasa kwanini ndoto za mchana zinaonewa!? Hiyo kwangu sina majibu!

Turudi kwenye mada. Dira kwa tafsiri isiyo rasimi sana ni mwongozo wa wapi unataka kufika au nini unataka kufikia! Kila mwenye malengo ya kufika mahali fulani lazima awe na dira ya namna ya kufikia malengo hayo aliyojiwekea.

Sasa kama dira ni mwongozo wa kufika au kufikia lengo fulani, kuwa na dira tu hakutakuwezesha kufikia hayo malengo yako. Ni lazima kuwe na kitu kitakachofuatana na hiyo dira. Kwa lugha rahisi sana hiyo DIRA ili ikufikishe uendoko ni lazima uitafsiri katika matendo. Mfano, mtoto mdogo anaye tamani siku moja aje kuwa Dactari wa magonjwa ya binadamu hana budi kujifunza kwa ukaribu sana namna gani watu hufikia kuwa madaktari. Kusema tu "nataka"kuwa daktari hakutamfanya awe daktari pasipo kusoma masomo yanayopelekea mtu kuwa daktari.

Vivyo hivyo kwa upande mwingine watu wanaofanya vitendo vingi pasipo kuwa na 'DIRA' yaani pasipokufahamu wapi wanataka kufika na namna nzuri ya kufika, mara nyingi hujikuta wanatumia muda mwingi sana na kupoteza nguvu pamoja na rasimali nyingi na mafanikio wanayo yatamani huishia kuyaona kwa wengine. Sababu kubwa ni kwamba wamekimbilia jambo hilo pasipo kujiwekea malengo ya wapi wafike na wafikeje huko wanakotaka kufika.

Mtu anayefanya kitu bila malengo wala dira ya kufika huko anakotaka kufika, hujikuta kila mara anabadili mtindo wa maisha. Na mara nyingi watu waliomzunguka wanaweza kushindwa kumshauri kwa kuhofu kumvurugia mpangilio wake huku wakiamini huenda ndo njia sahihi alizojichagulia kumbe masikini huenda hana habari.

Kila mwenye kutaka maendeleo kamwe hawezi kuwa na DIRA akaacha kuiweka katika matendo, na hawezi kufanya matendo akasahau kuyawekea DIRA! Dira na Matendo havitengani na vinapotengana ni vigumu sana kufikia mafanikio.

Kama unataka nyumbani kwako waache kuvaa mitumba ya ulaya, ni lazima uone umuhimu wa kuwafanya waache na namna gani uwaachishe jambo hilo. Ukisema, 'kuanzia wiki ijayo sitaki kuona mnanunua mitumba" kauli hiyo isiwe imelenga kusubiri mitumba iliyoko sokoni iishe halafu uwazuie waagizaji wasiagize tena! HAPANA! Kauli yako itafsiri katika matendo kwa kutengeneza nguo zitakazoitoa hiyo mitumba sokoni vinginevyo watoto wako watatembea uchi!
Vivyo hivyo katika sukari, Maji, barabara, Elimu, Viwanda n.k.

Hivi karibuni viongozi wetu wamekuwa wakitupa matumaini ya kuijenga Tanzania mpya! Tanzania yenye viwanda, Tanzania isiyotegemea sana misaada ya nje, Tanzania yenye Elimu bora, Tanzania yenye huduma za Afya nzuri, Tanzania yenye maji safi na salama hadi vijijini na mengine mengi sana. Lakini cha ajabu, mmoja akifanya hivi mwingine kesho anakuja kubatilisha kivingine kana kwamba kuna serikali mbili ambazo kuwasiliana kuhusu namna bora ya kutufikisha huko tupatamanipo ni kosa la jinai.

Ni vizuri kwa vile tayari wanamaono ya kutaka kutengeneza Tanzania mpya na kuzika ile ya zamani basi wawe na DIRA YA PAMOJA na WATENDE kwa PAMOJA. Mmoja akiamka na lake kisha mwingine mchana akaja na lake na mwingine usiku akaje na lake, ni dhahiri tutasema wanatenda pasipokuwa na DIRA na ni vigumu kufika wanapotwambia kuwa tutafika zaidi zaidi tutaishia kupafananisha tu huku kila siku tukiendelea kujiuliza eti "tunakosea wapi!?!"​
 
Back
Top Bottom