Mateja na malori ya mafuta!

leipzig

JF-Expert Member
Jan 9, 2013
2,767
1,703
Kwa muda mrefu sana mateja wamekuwa wakifungua mifuniko ya malori ya mafuta yakiwa kwenye foleni sehemu mbali mbali hapa jijini Dar.

Katika kuuliza kwangu ni kwanini polisi hawawazui mateja hao wanapofanya vitendo hivyo hatarishi nilijibiwa eti hayo malori yanakuwa yameshamwaga mafuta na pia mateja hawana chochote kitu ikiwa watakamatwa na polisi.

Naomba niwahakikishie mara zote malori hubaki na mafuta kwenye matenki na ndio maana hawa mateja hufungua mifuniko ili kukinga mafuta yaliyobaki.

Cha kushangaza hawa mateja hawana tahadhari yoyote wakati wanapofanya upuuzi huo. Ilitokea siku moja nilijaribu kumzuia teja asifungue mfuniko lakini alikaidi na kunichomolea kisu/bisibisi na ikabidi niwe mpole na yeye akaendelea. Cha kushangaza madereva tuliokuwa nao kwenye foleni waliishia kucheka na kuniona mimi ni kituko bila kujali athari ambayo ingeweza kutokea kwetu sote.

Naliomba jeshi la polisi litoe tamko rasmi kukemea uzembe huu unaoendelea katika barabara zetu. Hii itasaidia kuongeza uelewa wa raia katika kujua hatari ya moto inayoweza kutokea na kusababisha maafa makubwa.
 
Ikitokea bahat mbaya kapata ajali ndo utaskia serikali inalaumiwa
Wakat mwingine hapa dunian jihadhari ww tuu, ukafatilia na usalama wa wengine utaonekana kama mjinga, hata kama upo sahihi
 
Kuna mmoja nilimshuhudia akiwa kakaa kabisa kule nyuma na dumu lake huku gari linaenda,tena wengine huenda nayo umbali mrefu sana asee,hii nakumbuka nilikuwa natoka Dom to Dar,.achilia mbali hawa wa mijini,ni hatari wala si uongo plus na vipisi vya sigara vinavyotupwa kiholela watu wataoga moto sana tuu.
 
Subiri maafa

Watawajengea na mnara
 
Back
Top Bottom