Matawi ya vijana na wanawake ya vyama vya siasa ni kiashiria cha mabadiliko haba?

Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
37,620
46,260
Katika nchi ambazo zimeshuhudia mabadiliko finyu ya kisiasa baada ya uhuru wao mabaraza ya vijana na wanawake ndio yamekuwa mstari wa mbele zaidi kutetea maslahi ya vyama vyao.

Kwa upande wa mabaraza ya vijana

Kule Africa Kusini ANC Youth League bado ipo na ina karata kubwa katika siasa za nchi.

Zimbabwe ZANU PF Youth League bado ipo na imekuwa mwiba mkali kwa upinzani wa nchi hiyo.

Hapa Tanzania chama tawala na vyama vyote vikubwa vina mabaraza kama hayo. Wapo UVCCM, BAVICHA, Ngome ya ACT.

Nchi nyingine ambazo mabaraza hayo bado yana ushawashi ni Angola, Uganda na Botswana.

Ukiangalia siasa za hizi nchi zote kwa kiasi kikubwa ni kama zimebaki kwenye mawazo ya siasa za uhuru na agenda ya kudumisha maslahi na heshima za wapigania uhuru. Zimekuwa na mabadiliko haba sana ya kisiasa yaliyopatikana ukilinganisha na sehemu nyingine za Africa.

Nchi nyingi baada ya kupata mabadiliko makubwa ya kisiasa haya mabaraza ni kama yalipotea, kufanywa kamati tu za vyama au kupoteza ushawashi. BAVICHA, UVCCM na Ngome ACT nanyi jiandaeni.
 
Mabadiliko huanza kwa vijana kwa kupata mawazo na maarifa sahihi toka kwa watu wenye hekima na busara , ila Kuna vijana walipata nafasi ila matendo yao yalivunja tumaini la watu wengi juu ya matendo yao.
 
Back
Top Bottom