Matawi ya loliondo: Sasa aja mzungu

Amina Thomas

JF-Expert Member
Mar 9, 2008
272
129
Jamani mmesikia "vijiko vitatu" vya mzungu dar? Nimesikia kwenye magazeti ya leo kua amejitokeza mzungu anaetoa dawa ya kutibu ukimwi na saratani hapa dar. Naomba kama kuna ambae ameshapata vijiko atujuze zaidi.
 
Mzungu aibua tiba nyingine Dar

Na Beatrice Shayo

10th April 2011

headline_bullet.jpg
Yeye anatoa vijiko vitatu tu

Baada ya tiba ya vikombe kushamiri mikoa mbalimbali nchini, Mhubiri wa kimataifa Gordon Dacre kutoka Marekani naye ameibuka na tiba ya vijiko vitatu kutibu magonjwa sugu ikiwemo ukimwi na saratani kwa kutumia dawa za mitishamba.

Dacre ametangaza kutibu magonjwa hayo jana jijini Dar es Salaam wakati akiongea na waandishi wa habari.

Tiba ya Mhubiri Dacre imeibuka baada ya kujitokeza kwa watu wengine watano kueleza kutibu magonjwa sugu kwa kutumia mitishamba.

Alisema dozi hiyo ni vijiko vitatu kwa siku, kwa wagonjwa wote wanaosumbuliwa na ukimwi, figo, ini, kisukari, vidonda vya tumbo na aina nyingine ya magonjwa 17.

Alisema kuwa dawa hiyo inaitwa Omega Wash ambayo imechanganywa na aina mbalimbali za mimea ikiwemo karafuu pamoja vitunguu saumu.

Dacre anasema kuwa dawa hiyo ameoteshwa na Mungu tangu miaka minne iliyopita ili aweze kuwatibu watu wote wanaoumwa na magonjwa sugu na kuwaombea kupitia katika dawa hiyo.
“Nilimuomba Mungu anisaidie kunipatia dawa ili iweze kuwafikia watu wote dunia nzima kwa lengo la kunipunguzia mzigo wa kupita kila nchi kwa ajili ya kuwaombea kila mtu mwenye magonjwa sugu,” alisema Dacre.

Hata hivyo, alisema kuwa dawa hiyo haina madhara yoyote kwa binadamu na kwamba tayari wataalamu wa tiba, madaktari na wanasayansi wameifanyia utafiti.

Alisema dawa hiyo ina chembe chembe ambazo zinasafiri kwa haraka katika mwili na kusafisha damu pamoja na kurudisha uhai wa binadamu.

Aliongezea kuwa kuna baadhi ya wagonjwa waliokuwa wakisumbuliwa na maradhi ya Ukimwi wamepona kupitia dawa hiyo na kuanza kutolea ushuhuda kwa wengine.

Dacre alisema dawa hiyo inapatikana kwa wingi katika mkoa wa Arusha na imekuwa ikiuzwa kwa Sh. 70,000 pamoja na Dar es Salaam.

Aliongeza kuwa kwa sasa wanasubiri usajili wa dawa hiyo kutoka katika Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA) baada ya kupeleka taarifa ya kutaka kusajiliwa.

Mhubiri huyu anakuwa mtu wa sita kuibuka nchini na dawa za kutibu magonjwa sugu akitanguliwa na Mchungaji mstaafu Ambilikile Masapila(Babu) wa Loliondo anayetumia mti wa Mugariga, Asha Baraka wa Tabora anayetumia majani ya mahindi, Fatma Senga wa Morogoro, Jafari Fikiri wa Mbeya na Joshua Mwantyala wa Mbozi anayetibu kwa kumnyunyizia mgonjwa maji mdomoni. Mhubiri Dacre yeye anatibu kwa dawa inayoitwa Omega Wash.

CHANZO: NIPASHE JUMAPILI
 
wachungaji hawa walikuwa wapi siku zote? Wameona Ambilikile Mwasapile anapiga bao, nao ndo wameibuka.
Huyu mzungu ana kibali kotoka mamlaka ya chakula na dawa?
 
huyu mzungu kwa nini asitibie huko kwao mpaka aje Tanzania?......tena Arusha na Dar?.......hakika siku zi ukingoni.....tutaona mengi mwaka huu na ndio kwanza tupo April mpaka August tutakuwa tumejibeba hakyanani
 
Taifa la wajinga hili? Kila majaribio yanafanyika hapa!hamna tofauti na bichwa la mwendawazimu la kujifunzia kunyoa. Tutalishwa kila kila uchafu
 
Taifa la wajinga hili? Kila majaribio yanafanyika hapa!hamna tofauti na bichwa la mwendawazimu la kujifunzia kunyoa. Tutalishwa kila kila uchafu

Si hatutaki kutumia akili ya kawaida (common sense), tunapenda kufuata mkumbo! hayo ndio matokeo yake!!
 
huyu mzungu kwa nini asitibie huko kwao mpaka aje Tanzania?......tena Arusha na Dar?.......hakika siku zi ukingoni.....tutaona mengi mwaka huu na ndio kwanza tupo April mpaka August tutakuwa tumejibeba hakyanani
Alisikia Tanzania ni nchi ya kuamini ushirikina!
 
watanzania wengi sana tumejaa matope kichwani... Bora ata ukimwi utumalize ili tupunguze ghasia duniani tuwe mbolea tuu...
 
huyu mzungu kwa nini asitibie huko kwao mpaka aje Tanzania?......tena Arusha na Dar?.......hakika siku zi ukingoni.....tutaona mengi mwaka huu na ndio kwanza tupo April mpaka August tutakuwa tumejibeba hakyanani

preta MPAKA AUGUST ;TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA
 
wachungaji hawa walikuwa wapi siku zote? Wameona Ambilikile Mwasapile anapiga bao, nao ndo wameibuka.
Huyu mzungu ana kibali kotoka mamlaka ya chakula na dawa?
je nahuyo tapeli wenu waloliöndo anakibali kutoka katika mamlaka ya chakula na dawa?
 
Back
Top Bottom