Matatizo ya wabunge wa kuteuliwa!

Kwakweli nimeguswa na issue ua Bwana Makamba,hakika tunaoshangazwa na mzee huyu ni wengi, na sasa tunajua kuwa hakuwa lolote si chochote maana hata wao ndani ya CCM wanamlalamikia kuwa mla rushwa mkubwa kwa kutumia huo ukatibu mkuu.

Nnadhani ninashawishika kuwa rais alizitumia vibaya nafasi zake za ubunge wa kuteuliwa kama alivyosema muungwana kwa kutoa ahsante mpaka inatia kinyaa.

Wapo wengi walioteuliwa ambao hata kuulza swali hawajawahi bungeni mifano ni mingi, ukiacha makamba, kuna Tom Mwang'onda nk.

Ipo haja ya kutathimini mchango wa wabunge wa kuteuliwa maana hawa wa majimbo wapo wananchi waliowateua watawatathimini lakini hawa wa kupewa na rais tuwaangalie sisi.
 
Mzee Kingunge alipewa Ubunge wa kuteuliwa ili apewe Uwaziri. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Zakia Meghji. Sasa wote si Mawaziri tena, wamebaki kuwa wabunge wa kuteuliwa. Wanatusaidia nini bungeni sasa? Wanamwakilisha nani? Je Rais anazo nguvu za Kikatiba za kutengua uteuzi wao?

Kwa mtazamo wangu, lengo la kuweka nafasi 10 za wabunge wa kuteuliwa na Rais lilikuwa zuri sana. Hii ni kwa sababu Rais anaweza kuona kuna watu wanaofaa sana katika baraza lake la Mawaziri ambao sio wabunge, akawateua na kisha kuwafanya Mawaziri.

Kwa bahati mbaya sana, naona kama vile inatumika vibaya kwa kuteua watu wa minaajili ya kuwalipa fadhila badala ya kuteua watu kutokana na ubora wa utendaji wao wa kazi. Kuna wasomi wengi wanaoweza kuongeza Wizara nyeti za serikali yetu lakini hawataki kugombea ubunge kwa sababu zinazofahamika, rushwa, majungu na kadhalika. Hao ndio walistahili hizo nafasi ili wamsaidie Rais.

Masaki:

Hapana, isiwe sababu ya kumteua mtu ubunge ili apewe uwaziri.

Ndio kabisa: Rais atumie nafasi za kuteua mtu kuwa mbunge kwa kuangalia uwezo wa mtu huyo katika kuchangia mawazo na kusimamia shughuli za kimaendeleo katika sekta mahususi zilizolengwa.

Ninakubali kuwa utaratibu anaoutumia rais sasa hivi kuwateua watu ni kama kutoa zawadi tu kwa wateuliwa. Mtindo huu hautuletei tija.
 
kwa kadiri ninavyomfahamu mzee huyo sikumbuki kama amewahi kudaiwa kuwa mla rushwa. Na ninamfahamu kwa karibu sana; hivyo madai kuwa ni "mla rushwa mkubwa" ni madai mazito. Kuna mahali popote ambapo amedaiwa kula rushwa au kupata mapato nje ya taratibu za kisheria, maana najua madaraka yanaweza kumfanya mtakatifu awe mwenye dhambi. Haya tupeni somo wengine.
 
Makamba akiwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, alionyesha uwezo mkubwa ktk kutoa mawazo na kusimamia shughuli za maendeleo. Labda hakuna haja ya nafasi hizi, kumbuka ni nafasi 10. Ukipiga mahesabu ya posho, mshahara na marupurupu mengine kama Mbunge ni pesa nyingi.
 
kwa kadiri ninavyomfahamu mzee huyo sikumbuki kama amewahi kudaiwa kuwa mla rushwa. Na ninamfahamu kwa karibu sana; hivyo madai kuwa ni "mla rushwa mkubwa" ni madai mazito. Kuna mahali popote ambapo amedaiwa kula rushwa au kupata mapato nje ya taratibu za kisheria, maana najua madaraka yanaweza kumfanya mtakatifu awe mwenye dhambi. Haya tupeni somo wengine.

Hadi ameandika kitabu kuhusu hilo.
Hapana, hata mimi madai hayo nayapinga na siyakubali bila ya ushahidi usiopingika. Mimi pia namfahamu kwa ukaribu zaidi, na sina mfano wa kumhusisha na ufisadi.
 
kwa kadiri ninavyomfahamu mzee huyo sikumbuki kama amewahi kudaiwa kuwa mla rushwa. Na ninamfahamu kwa karibu sana; hivyo madai kuwa ni "mla rushwa mkubwa" ni madai mazito. Kuna mahali popote ambapo amedaiwa kula rushwa au kupata mapato nje ya taratibu za kisheria, maana najua madaraka yanaweza kumfanya mtakatifu awe mwenye dhambi. Haya tupeni somo wengine.

Aliishawahi kuhusishwa na JF hapa kuwa ni mla rushwa mzuri tu toka kwa Manji na mara kwa mara huonekama katika ofisi za Jeetu Patel na inasemekana amejengewa hata nyumba lol!
 
Mzee Kingunge alipewa Ubunge wa kuteuliwa ili apewe Uwaziri. Na ndivyo ilivyokuwa kwa Zakia Meghji. Sasa wote si Mawaziri tena, wamebaki kuwa wabunge wa kuteuliwa. Wanatusaidia nini bungeni sasa? Wanamwakilisha nani? Je Rais anazo nguvu za Kikatiba za kutengua uteuzi wao?

Kwa mtazamo wangu, lengo la kuweka nafasi 10 za wabunge wa kuteuliwa na Rais lilikuwa zuri sana. Hii ni kwa sababu Rais anaweza kuona kuna watu wanaofaa sana katika baraza lake la Mawaziri ambao sio wabunge, akawateua na kisha kuwafanya Mawaziri.

Kwa bahati mbaya sana, naona kama vile inatumika vibaya kwa kuteua watu wa minaajili ya kuwalipa fadhila badala ya kuteua watu kutokana na ubora wa utendaji wao wa kazi. Kuna wasomi wengi wanaoweza kuongeza Wizara nyeti za serikali yetu lakini hawataki kugombea ubunge kwa sababu zinazofahamika, rushwa, majungu na kadhalika. Hao ndio walistahili hizo nafasi ili wamsaidie Rais.

Rais anaweza kuwaacha watu kumi na kupeleka muswada wa kuwapata mawaziri wasio Wabunge ili waweze kukaliwa vyema kooni.Hili ni jambo muhimu sana kama tunataka kuchapa kazi na kulijenga Taifa .Mie nalia sana na hizi za rais zina kasoro kubwa hata kama lengo ni zuri lakini sasa anaweka washikaji nakulipa fadhila.
 
Mimi nataka nijue kuwa hawa jamaa wanatugharimu kiasi gani;

Mshahara = .............................

Sitting Allowance = .............................

Car Allowance = .............................

Office Maintenance Allowance = .............................

Travelling Allowance = .............................

Housing Allowance = ..............................

Medical Insuarance = ..............................

Others = ..............................

TOTAL = .............................

Grand Total (Total x 12months x 5yrs = ......................

Naomba tusaidiane kujaza ili tujue wanachotutafuna wanapokuwa hawana la kufanya bungeni.
 
kwa kadiri ninavyomfahamu mzee huyo sikumbuki kama amewahi kudaiwa kuwa mla rushwa. Na ninamfahamu kwa karibu sana; hivyo madai kuwa ni "mla rushwa mkubwa" ni madai mazito. Kuna mahali popote ambapo amedaiwa kula rushwa au kupata mapato nje ya taratibu za kisheria, maana najua madaraka yanaweza kumfanya mtakatifu awe mwenye dhambi. Haya tupeni somo wengine.

Sidhani kama huyu bwana ni mla rushwa, lakini hana uwezo katika utendaji wa kazi na hili limethibitishwa alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar na pia cheo chake cha sasa hivi kama SC wa CCM. Anabebwabebwa tu lakini ufanisi wake ni zero hata ndani ya CCM sehemu nyingi wanamlalamikia.
 
Aliishawahi kuhusishwa na JF hapa kuwa ni mla rushwa mzuri tu toka kwa Manji na mara kwa mara huonekama katika ofisi za Jeetu Patel na inasemekana amejengewa hata nyumba lol!

Kumbe naye yumo! Nilikuwa silijui hili. Yeyote anayeonekana kwa Jeetu Patel au Yusuf Manji basi huwa ameenda huko kuchukua mshiko na si mshiko mdogo.
 
Yule Mhindi majuzi alichangisha pesa na mkewe JK ndipo Makamba anashinda kulamba pesa za wizi .Kuna mtu aliwahi kuleta madai haya nabaadaye watu tumeyaona haya .Mhindi yule anamjengea JK hekalu na si Jeetu .
 
Sidhani kama huyu bwana ni mla rushwa, lakini hana uwezo katika utendaji wa kazi na hili limethibitishwa alipokuwa mkuu wa mkoa wa Dar na pia cheo chake cha sasa hivi kama SC wa CCM. Anabebwabebwa tu lakini ufanisi wake ni zero hata ndani ya CCM sehemu nyingi wanamlalamikia.

mzee yeye ukisema atakuonesha Tunduru na Kiteto... na tutake tusitake ana mvuto kwa watu wengi wa kijijini na sitoshangaa endapo Dr. Slaa atavuliwa Ubunge Karatu, basi Mgosi wa Kaya atahamia huko kuhakikisha jimbo hilo linarudi CCM.
 
Mimi ninaonelea kuwa hii ya raisi kuchagua wabunge 10 si sawa. Kwa mtazamo binafsi ingekuwa sawa kama haya mawili yangefualiliwa kwa kwa makini:
(1) Kama president anafikiri/kujiridhisha kuwa kuna Mwananchi anayeweza kushika nafasi ya uwaziri ambaye sio mbunge na "kama ni lazima waziri awe mbuge" ambayo sioni mantiki ya hilo na basi achague mbunge ambaye ni lazima atamteuwa kuwa waziri to justify in the basket ya wabunge wa kuchaguliwa there is non to fit that position.
(2) Waziri ambaye ni mbunge wa kuteuliwa "pindi" anapokosa sifa ya kuwa waziri by any means anakosa pia sifa ya kuwa mbunge. Hii ni muhimu kwa kuwa itamhakikishia raisi hizi "nafasi 10 za uwaziri" based on competense at any time.
 
Jamani nashukuru kulileta hili suala hapa katika jambo forum.
CCM ni wajanja kwani kwa makamba kuwa Katibu Mkuu wa Chama anatakiwa kulipwa mshahara na ukiunganisha hizi post atakuwa analipwa mshahara kama mbunge lakini kazi anafanya CCM na bunge limalizapo mhula naye analipwa marupurupu yake.
Janja ya CCM hiyo Tanzania lazma tuamke
 
kwa kadiri ninavyomfahamu mzee huyo sikumbuki kama amewahi kudaiwa kuwa mla rushwa. Na ninamfahamu kwa karibu sana; hivyo madai kuwa ni "mla rushwa mkubwa" ni madai mazito. Kuna mahali popote ambapo amedaiwa kula rushwa au kupata mapato nje ya taratibu za kisheria, maana najua madaraka yanaweza kumfanya mtakatifu awe mwenye dhambi. Haya tupeni somo wengine.

katika wato corrupt nchi hii makamba yumo....mfano mmoja..akiwa mkuu wa mkoa alimpapatikia manji na kuanza kuwa mpiga kampeni wake kigamboni hadi kumuita mbunge....hata kabla ya uchaguzi..pia alimsaidia manji huyo huyo KUPORA KIWANJA CHA WAISLAMU KILICHOKO JIRANI NA SHULE YA KIBASILA,TEMEKE....mifano ni mingi tu ..uliza wanaomfahamu vema.
 
Mimi nataka nijue kuwa hawa jamaa wanatugharimu kiasi gani;

Mshahara = .............................

Sitting Allowance = .............................

Car Allowance = .............................

Office Maintenance Allowance = .............................

Travelling Allowance = .............................

Housing Allowance = ..............................

Medical Insuarance = ..............................

Others = ..............................

TOTAL = .............................

Grand Total (Total x 12months x 5yrs = ......................

Naomba tusaidiane kujaza ili tujue wanachotutafuna wanapokuwa hawana la kufanya bungeni.

Ukisearch humu kwenye forum utapata majibu, Mh. Zitto alishawahi kuweka mshahara wake na akauibreakdown.
 
Kimsingi nafasi kumi alizonazo Rais zilikuwa kwa ajili ya makundi maalum katika jamii ambayo hayawezi kuingia moja kwa moja katika siasa na kugombea ubunge kupitia vyama vya siasa. Kwa mfano makundi ya walemavu, viongozi wa dini na mengine ambayo kwa kupewa mwakilishi kupitia uteuzi wa Rais yangeweza kuwakilishwa moja kwa moja ndani ya bunge. Kwa mfano kwa sasa tunatatizo la mauaji ya albino, tatizo la ukimwi. Pengine nafsi hizo kumi zingepewa kwa makundi hayo wangeweza kuchangia na kuwakilisha matatizo yao moja kwa moja kwenye chombo cha kutunga sheria kuliko kumpa mtu kama Makamba ambaye sina hakika kama amewahi kuchangia chochote.
 
makamba ni mbunge wa kuteuliwa na chama ccm na si mbunge wa kuteuliwa na wananchi. kwa hiyo akifika kule yeye anawakilisha chama na sio wananchi!! na kama chama hakihitaji yeye kusema lolote bungeni, basi yeye hana kosa, anatekeleza sera ya chama tu.

ndo tutafika hivi!!!
 
makamba ni mbunge wa kuteuliwa na chama ccm na si mbunge wa kuteuliwa na wananchi. kwa hiyo akifika kule yeye anawakilisha chama na sio wananchi!! na kama chama hakihitaji yeye kusema lolote bungeni, basi yeye hana kosa, anatekeleza sera ya chama tu. ndo tutafika hivi!!!

Kazi kweli kweli hapo!
 
Kwakweli nimeguswa na issue ua Bwana Makamba,hakika tunaoshangazwa na mzee huyu ni wengi,nasasa tunajua kuwa hakuwa lolote si chochote maana hata wao ndani ya CCM wanamlalamikia kuwa mla rushwa mkubwa kwa kutumia huo ukatibu mkuu. Nnadhani ninashawishika kuwa rais alizitumia vibaya nafasi zake za ubunge wa kuteuliwa kama alivyosema muungwana kwa kutoa ahsante mpaka inatia kinyaa.Wapo wengi walioteuliwa ambao hata kuulza swali hawajawahi bungeni mifano ni mingi,ukiacha makamba,kuna Tom Mwang'onda nk.Ipo haja ya kutathimini mchango wa wabunge wa kuteuliwa maana hawa wa majimbo wapo wananchi waliowateua watawatathimini lakini hawa wa kupewa na rais tuwaangalie sisi.

Mimi Binafasi naweza kusema kuna mengi tu tunaendelea kuya-abuse, sio nafasi hizo kumi za ubunge wa kuteuliwa. Lakini still naona kuwa bunge lingeomba hizo nafasi zipelekwe majimboni, na sio kuwapa watu nyadhifa za dezo (Mama Meghji) halafu anavuruga mambo na kuanza kulalamika. Lakini hata hivyo naomba nipingane na Bw Achebe, kuwa muongeaji au kuwa muulizaji mzuri wa maswali hakuna maana kuwa wewe ni mtendaji mzuri!
 
Back
Top Bottom