Mugishagwe
JF-Expert Member
- Apr 28, 2006
- 300
- 58
Jamani salaam tena na leo narudi kutaka kujifunza. Nimeona mjadala wa mgombea binafsi unapamba moto na nikaanza kujiuliza kama Mtikila ama Mzee Es anaweza naye kwenda kuomba kufata Wabunge wa Kuteuliwa ama Viti maalam.
Sasa ninavyoona ni kwamba hawana maana wakati majimbo yote ya Tanzania yana wawakilishi Bungeni na ni gharama kubwa kwa Taifa ikifika wameshaulamba ukuu.
Nchi ya Tanzania ni ya Vyama vingi na haki ya kuchagua vongozi wamepewa Watanzania kwa nini tuwe na watu wa maalum ambao ni mzigo wa walipa kodi. Wanamwakilisha nani na wana nguvu gani ukiachilia mbali kuwa ni Wabunge? Rais kuwa na wake 10 na Vyama vya upinzani kupewa kutoa Wabunge wa cheee je ni sahihi?
Mtanisamehe maana hata mwalimu aliwahi kusema Mugishagwe una kichwa kigumu kuelewa nikamuuliza kwa nini akasema huwa unangoja linatokea baada ya muda ndipo unazuka na maswali. Sasa nakuja kwenu nipeni msaada wa maoni yenu nione kama naweza kutinga Mahakamani kupingana na watu hawa ambao nadhani hawana haja kwa kuwa majimbo yote yana Wabunge wa kupigiwa kura na tena kuwapa upendeleo ni Ubaguzi kwa mujibu wa Katiba maana makundi mengine hayajawakilishwa Bungeni pia.