Matatizo ya usingizi

ndege JOHN

JF-Expert Member
Aug 5, 2015
19,573
44,804
Mwaka wa 2002, zaidi ya madaktari 600 na zaidi ya wagonjwa 11,000 walihusishwa katika uchunguzi mkubwa zaidi kuhusu matatizo ya usingizi kuwahi kufanywa nchini Italia. Uchunguzi huo umefunua kwamba zaidi ya Waitaliano milioni 12 wana matatizo ya usingizi.

Asilimia 65 ya waliochunguzwa husinzia asubuhi, asilimia 80 husinzia wakati wa mchana, na asilimia 46 hushindwa kukaza fikira kazini. Gazeti hilo linasema: “Kwa kuwa asilimia 22 ya misiba ya barabarani husababishwa na kusinzia, wale wanaoendesha magari wanakabili hatari kubwa.”

Uchunguzi huo pia ulionyesha kwamba asilimia 67 ya watu wenye matatizo ya usingizi hawajamweleza daktari kuhusu tatizo hilo. “angalau asilimia 20 ya watu hao hasa wanasumbuliwa na matatizo ya usingizi, na hawajui sababu.” Hata hivyo, uchunguzi wa kitiba unaweza kuonyesha tatizo lingine linalosababisha hali hiyo.

Visababishi vingine vya matatizo ya usingizi vinatia ndani wasiwasi (asilimia 24), mambo yenye kufadhaisha (asilimia 23), na kushuka moyo (asilimia 6).
 
Back
Top Bottom