Matatizo ya ndoa yanarithishwa?

Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
280
Likes
5
Points
33
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2010
280 5 33
Ndugu wana JF nina swali na nitashukuru kama mtanipa majibu sawia maana najua wahusika watanishukuru kama nitawapa jibu sahihi maana mi nilipoelezwa na mmoja wao sikuwa na jibu. (Naomba niwe mwazi kuwa aliyenieleza ni mume kwa hiyo maelezo yako biased kiaina upande mmoja)

Nina marafiki wawili mtu na mkewe. (Mume ndo rafiki yangu sana maana tulisoma wote chuo. Mke siyo rafiki sana ila tunachat.) Wote ni wafanyakazi na wanafanya kazi nzuri tu na wanalipwa vizuri. Hawa watu wanachekesha. Kila siku hawaishi kugombana ingawa nahisi wanapendana sana.

Wanachongombania ukikisikiliza huwezi ukaamini kama ni watu wenye masters degree. Its not essential (in my opinion).

Central issue ya ugomvi wao ni fedha. Mama anataka fedha za mumewe zitumike kwenye shughuli za ndani kama kununua mboga, kitunguu, chumvi na udongo wa mkewe. Mume anagoma. Mume anasema yeye tayari anagharamia ujenzi wa nyumba kubwa ya vyumba vinne self contained, ananunua mafuta ya gari la mkewe kwenda kazini na vitu kama gesi, mchele na unga.

Mume anadai ili kuweka usawa hela ya mama itumike kununua chumvi, udongo n.k kwa kuwa mama alishakataa kuchangia kwenye miradi mikubwa kwa kisingizio mshahara wake ni mdogo na ana baba, mama na dada zake wawili (na watoto wao saba) wanaomtegemea yeye.

Mume anadai mkewe kushiriki katika kujenga familia yao ndogo japo kwa kuchangia kidogo ni muhimu ili kile kinachopatikana kiwe cha wote na mke anasema mume kukataa kununua chumvi, maziwa na mayai ni dalili ya ubahili wa kurithi.

Yeye (mke) anasema ndugu zake wakistabilise ataweza kutoa mchango mkubwa katika familia.

Hii ndiyo source ya maugomvi yao ya kitoto. (Sijui nyie mnasemaje).

Right now mke anatishia kuondoka home au kutafuta bwana wa kumuongezea kipato ili achangie home na mume naye ameweka kigingi anasema kama ndoa na iharibike lakini hatatoa hela ya kununua vitu vidogo wakati mkewe naye anapata salary.

Baada ya kuona siwaelewi wana ndugu hawa nikaona nichunguze family background zao.

Mume anatoka katika familia ya wastani lakini inajiweza. Baba na mama yake hawaishi pamoja. Mama anafanya kazi mkoa na anakuja once a month. (Story ni kuwa ugomvi wao ni namna fedha inavyotumiwa.

Mama anataka fedha itumike kwa wao kuishi kwa raha na baba anataka kuinvest kwenye assets kwa ajili ya watoto wao).

Mke anatoka kwenye family ya kawaida iliyoko mkoa. Baba na mama wanaishi pamoja kwa kuelewana. Ni wakulima. Tatizo ni dada zake mke. Wako watatu. Wote wamekimbia wanaume zao.

Wao na watoto wao saba wako pale home kwa baba yao. Hawataki kurudi kwa wanaume eti kwa sababu wanafanyishwa kazi sana na hawakuzoea hivyo.

Mzee hawezi kumudu kutunza family kubwa hiyo so inabidi mtoto wa kike msomi ndo alipie gharama za matunzo za watu 10 every month.

Maswali yangu:
 1. Je, ni sahihi kwa mume kugoma kulipia nyanya na vitunguu ili abaki na matumizi makubwa tu?
 1. Je, ni sahihi kwa mke kugharamia familia yake ya mkoa at the expense ya kujenga familia yake mwenyewe?
 2. Je, hii familia itaweza kudumu katika ndoa maana mke ameshatishia kuondoka?
 3. Je, matatizo ya kifamilia yanarithishwa kati ya kizazi na kizazi.

Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).
 
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Messages
37,832
Likes
23,171
Points
280
The Boss

The Boss

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2009
37,832 23,171 280
kwa kihasi fulani mke yuko right...
kabla mume hujaanza masuala ya ujenzi na future..
lazima ujali masuala ya kila siku ya kula na mahitaji ya ndani....

ningekuwa mimi,ningemwambia wife pesa yako wasaidie ndugu zako
pamoja na matumizi binafsi ya mke kama saloon,mavazi.vocha na kadhalika.
mume lazima ugharamie matumizi ya ndani hata kama mnajenga.
 
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined
Sep 30, 2009
Messages
11,314
Likes
111
Points
145
Fixed Point

Fixed Point

JF Bronze Member
Joined Sep 30, 2009
11,314 111 145
[/B]

Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).[/QUOTE]

Kumbe unafanya data collection? all the best
 
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined
Aug 21, 2007
Messages
11,845
Likes
86
Points
0
Gaijin

Gaijin

JF-Expert Member
Joined Aug 21, 2007
11,845 86 0
japo kuwa ni wajibu wa mume kulipia kila kitu katika familia japo kama mke hana matatizo mengine, nafikiri kibinaadamu mke pia alitakiwa kuonyesha wepesi katika kuchangia kidogo katika familia yake na mumewe pia.
ukifikiri ............atawalea dada zake mpaka lini?

sidhani kuwa matatizo ya kifamilia yanarithiwa lakini yanaweza ku influence mitazamo yao
 
N

Nanu

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2009
Messages
1,224
Likes
9
Points
135
N

Nanu

JF-Expert Member
Joined May 29, 2009
1,224 9 135
Maswali yangu:
 1. Je, ni sahihi kwa mume kugoma kulipia nyanya na vitunguu ili abaki na matumizi makubwa tu? Hapana ni sahihi mume kutunza familia yake. Lakini issue iko hivi mama anafanya kazi na anayempeleka kazini ni mume maana ananunua mafuta ya gari ya mama. Kwanini mama asijigharamie usafiri wa kwenda kazini hali analipwa mshahara?
 2. Je, ni sahihi kwa mke kugharamia familia yake ya mkoa at the expense ya kujenga familia yake mwenyewe? Ni sawa mke kuwasaidia ndugu zaka lakini sio kwa expense ya matumizi ya nyumbani kwake. Kwa maana nyingine mume wa huyu dada anailisha na kuivisha familia ya mkewe pamoja na watoto wenye baba zao na mama zao wenye nguvu tu. Anafanya hivyo kwa sababu huyu mama anafanya kazi na wala halipi nauli ya kwenda kazini (hanunui mafuta ya gari lake), hanunui chochote nyumbani na bado mzee anamgharamia kila kitu. Sasa fedha zake zote anapeleka kwao, kwa maana nyingine zile fedha ambazo amesave kwa matumizi ndiyo anapeleka kwao, hivyo hizi ni baadhi ya hela za mume.
 3. Je, hii familia itaweza kudumu katika ndoa maana mke ameshatishia kuondoka? Maadam, mama ameanza kutishia mara mbili (anataka bwana wa kumwongezea fedha ili atoe kwa familia au aende nyumbani kwao) hiyo iliyopigiwa mstari inawezekana tayari inafanya kazi lakini anataka kuhalalisha kitu ambacho mume hatakubali na hivyo ataendelea kuumia peke yake. Mume inatakiwa aache kuweka gari mafuta na asitoe fedha ya saloon maana mama anafanya kazi na hizi ajihudumie mwenyewe. Kwa kufanya hivyo anaweza kuona rangi halisi za mke wake! Akiamua kuondoka be it, kwani huyu inaonekana hajali maendeleo ya familia yake bali anajali familia za ndugu zake..toa boriti kwenye jicho lako kwanza ndipo uone la mwenzako.. you can't stretch beyond your capacity la sivyo utapasuka msamba, maana yake inabidi awasaidie ndugu zake kwa kiasi anachoweza bila kuathiri familia yake..hata katika biblia imeandikwa..uwe na upendo kiasi...
 4. Je, matatizo ya kifamilia yanarithishwa kati ya kizazi na kizazi. Wala hayarithishwi bali yanawezwa kujifunzwa. Inabidi pia wafanye maombi ya pamoja ya kukata maagano za asili ambazo zinaweza kuwa zinawanyemelea. Lakini kwa upande mwingine tabia huwa zinarithishwa kizazi hata kizazi na zile tabia mbaya unaweza kuziepuka kwa maombi ya kukata mnyororo wa maagano ya ukoo wako hasa yale yasiyo ya Kimungu
 
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
280
Likes
5
Points
33
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2010
280 5 33
Boss nakubaliana na wewe kuwa kwa kiasi fulani wote wako right na hii ndo source ya ugomvi. wote ni wasomi na wanajua position zao ziko sahihi. lakini nani wa kuwaambia kuwa hii inahitaji common sense zaidi kama siyo mimi?

Asante kwa ushauri.

kwa kihasi fulani mke yuko right...
kabla mume hujaanza masuala ya ujenzi na future..
lazima ujali masuala ya kila siku ya kula na mahitaji ya ndani....

ningekuwa mimi,ningemwambia wife pesa yako wasaidie ndugu zako
pamoja na matumizi binafsi ya mke kama saloon,mavazi.vocha na kadhalika.
mume lazima ugharamie matumizi ya ndani hata kama mnajenga.
 
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
280
Likes
5
Points
33
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2010
280 5 33
[/B]

Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).[/QUOTE]

Kumbe unafanya data collection? all the best
haahaaa!! thanks. its so fun to think the way you think.!!
 
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
280
Likes
5
Points
33
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2010
280 5 33
Nanu,
Thank you so much for this. You are a wise person and i will read and re read your message.

i find it very sensible and i will use it for sure.

Thank you again.

Maswali yangu:
 1. Je, ni sahihi kwa mume kugoma kulipia nyanya na vitunguu ili abaki na matumizi makubwa tu? Hapana ni sahihi mume kutunza familia yake. Lakini issue iko hivi mama anafanya kazi na anayempeleka kazini ni mume maana ananunua mafuta ya gari ya mama. Kwanini mama asijigharamie usafiri wa kwenda kazini hali analipwa mshahara?
 2. Je, ni sahihi kwa mke kugharamia familia yake ya mkoa at the expense ya kujenga familia yake mwenyewe? Ni sawa mke kuwasaidia ndugu zaka lakini sio kwa expense ya matumizi ya nyumbani kwake. Kwa maana nyingine mume wa huyu dada anailisha na kuivisha familia ya mkewe pamoja na watoto wenye baba zao na mama zao wenye nguvu tu. Anafanya hivyo kwa sababu huyu mama anafanya kazi na wala halipi nauli ya kwenda kazini (hanunui mafuta ya gari lake), hanunui chochote nyumbani na bado mzee anamgharamia kila kitu. Sasa fedha zake zote anapeleka kwao, kwa maana nyingine zile fedha ambazo amesave kwa matumizi ndiyo anapeleka kwao, hivyo hizi ni baadhi ya hela za mume.
 3. Je, hii familia itaweza kudumu katika ndoa maana mke ameshatishia kuondoka? Maadam, mama ameanza kutishia mara mbili (anataka bwana wa kumwongezea fedha ili atoe kwa familia au aende nyumbani kwao) hiyo iliyopigiwa mstari inawezekana tayari inafanya kazi lakini anataka kuhalalisha kitu ambacho mume hatakubali na hivyo ataendelea kuumia peke yake. Mume inatakiwa aache kuweka gari mafuta na asitoe fedha ya saloon maana mama anafanya kazi na hizi ajihudumie mwenyewe. Kwa kufanya hivyo anaweza kuona rangi halisi za mke wake! Akiamua kuondoka be it, kwani huyu inaonekana hajali maendeleo ya familia yake bali anajali familia za ndugu zake..toa boriti kwenye jicho lako kwanza ndipo uone la mwenzako.. you can't stretch beyond your capacity la sivyo utapasuka msamba, maana yake inabidi awasaidie ndugu zake kwa kiasi anachoweza bila kuathiri familia yake..hata katika biblia imeandikwa..uwe na upendo kiasi...
 4. Je, matatizo ya kifamilia yanarithishwa kati ya kizazi na kizazi. Wala hayarithishwi bali yanawezwa kujifunzwa. Inabidi pia wafanye maombi ya pamoja ya kukata maagano za asili ambazo zinaweza kuwa zinawanyemelea. Lakini kwa upande mwingine tabia huwa zinarithishwa kizazi hata kizazi na zile tabia mbaya unaweza kuziepuka kwa maombi ya kukata mnyororo wa maagano ya ukoo wako hasa yale yasiyo ya Kimungu
 
Masikini_Jeuri

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
6,803
Likes
380
Points
180
Masikini_Jeuri

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
6,803 380 180
Wote wawili wanasahau priority waliyonayo kwao wao binafisi; lila mtu no. 1 priority kwa mwenzie!

Well kuhusu matatizo kurithishwa ni kweli; Hata kitabu kitakatifu Biblia imeandikwa ....nitawapatiliza wana maovu ya baba zao! Hivyo ndugu zanguni tusifanye mambo kinyume na Mungu atakavyo; kwani kwa kufanya kinyume na Mungu tunakuwa tunajichumia laana amabazo wanetu wasipokombolewa watazirithi!
 
M

Malila

JF-Expert Member
Joined
Dec 22, 2007
Messages
4,509
Likes
963
Points
280
M

Malila

JF-Expert Member
Joined Dec 22, 2007
4,509 963 280
Ndoa nyingi zilizofanikiwa ni zile ambazo kisomo au uchumi wa mhusika si rungu la kumchapia mwenzake.
Tunapoingia ktk ndoa na vyeo vyetu/degree zetu/makampuni yetu/ nk na tukasahau wajibu wetu ndani ya ndoa zetu taabu lazima ije.
 
Masikini_Jeuri

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined
Jan 19, 2010
Messages
6,803
Likes
380
Points
180
Masikini_Jeuri

Masikini_Jeuri

JF-Expert Member
Joined Jan 19, 2010
6,803 380 180
Tunapoingia ktk ndoa na vyeo vyetu/degree zetu/makampuni yetu/ nk na tukasahau wajibu wetu ndani ya ndoa zetu taabu lazima ije.
Ukamanda wako huko huko!!!!!!!!!!! teh teh teh teh teh:D

Kweli tupu mkuu
 
FirstLady1

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined
Jul 29, 2009
Messages
16,727
Likes
802
Points
280
FirstLady1

FirstLady1

JF-Expert Member
Joined Jul 29, 2009
16,727 802 280
Huyo mwanamke anatakiwa amsaidie mmewe jamani kama jamaa yuko kwenye issue za ujenzi ,mafuta ya gari na mengine..
jamani yaani mwanamke anaona ugumu kununua hata chumvi, pilipili na vitunguuu
si haki ongea nae mwanamke ajaribu kumsaidia mmewe !
 
carmel

carmel

JF-Expert Member
Joined
Aug 24, 2009
Messages
2,840
Likes
14
Points
135
carmel

carmel

JF-Expert Member
Joined Aug 24, 2009
2,840 14 135
kwa kihasi fulani mke yuko right...
kabla mume hujaanza masuala ya ujenzi na future..
lazima ujali masuala ya kila siku ya kula na mahitaji ya ndani....

ningekuwa mimi,ningemwambia wife pesa yako wasaidie ndugu zako
pamoja na matumizi binafsi ya mke kama saloon,mavazi.vocha na kadhalika.
mume lazima ugharamie matumizi ya ndani hata kama mnajenga.
In red, It takes a very matured, and understanding person with a very loving heart to do that. Btw, why did he chose to mary a poor girl with lots of dependants/ i bet he knew it before committing to her.
In blue, na ikitokea mume hafanyi hayo yote yaani mke anajigharamia mwenyewe na bado anataka mke amsaidie na kuilisha familia inakuwaje? ni fair?
 
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined
Jun 28, 2009
Messages
3,158
Likes
11
Points
0
Tumain

Tumain

JF-Expert Member
Joined Jun 28, 2009
3,158 11 0
Mume anatakiwa kuhudumiwa familia kuanzia vitu vidogo mpaka vitu vikubwa

Hata hivyo kwa case hii ikiwa mwanamke anafanya kazi (si mama wa nyumbani) lazima asaidie kuhudumia familia "equal proportion of her income" ni wajibu na lazima angekuwa mama wa nyumbani hapo angepewa kila kitu

Huyu mwanamke ni selfish na mwanaume anatakiwa awe strong amwambie achague moja lazima ahudumie familia katika sehemu fulani

Mke wangu anayefanya kazi lazima amlipe house keeper kwa mshahara wake na alipie gharama fulani za nyumbani e.g. vyombo, na partly vyakula

Kuna haja ya kufanya "consensus" na kuangalia kipi ni priority kwenye ndoa yao...na watoto wao
 
F

Future Bishop

Member
Joined
Dec 4, 2009
Messages
75
Likes
4
Points
0
F

Future Bishop

Member
Joined Dec 4, 2009
75 4 0
Kwa uzoefu mdogo nilionao najua kuwa suala la fedha ndani ya nyumba huwa ni chanzo kingine cha ugomvi na kutoolewana kati ya mme na mke. Ni mapato kiasi gani kila mmoja anapata na yanatumikaje, ni moja ya changamoto kubwa ukiacha ile ya uaminifu wa kutomegwa/kumega nje ya ndoa.

Mimi nitasaidia kwa kueleza ninavyofanya;

Mimi na mke wangu wote tunafanya kazi na tuna akaunti ya pamoja(Joint bank account) japo mshahara wangu ndo unapitia kwenye hii akaunti. Yeye analipwa kwa cheque kwa hiyo akipata cheque analeta nyumbani cash au anaingiza kwenye hiyo akaunti.

Kila mwaka kuna mipango ya maendeleo tunayokubaliana kuiweka na kujadiri mapato ya kuwezesha kukamilisha mipango hiyo. Kwa hiyo kila mwezi tunakubaliana matumizi/bajeti na tunaangalia jumla ya mapato yetu katika mwezi huo. Kwa hiyo hakuna cha kusema ni hela ya fulani(mme/mke) ndo imenunua nyanya, imenunua mafuta ya gari, immeenda kwa ndugu wa mke/mme au imejenga nyumba bali ni fedha yetu.

Kitu kingine ambacho tunamshukuru Mungu kuwa anatusaidia sasa ni kuwa kama ni fedha ya kuwasaidia ndugu zangu nampa yeye anawapa ili ndugu zangu wajue kuwa siyo mimi ninayewapa ila ni sisi tumeamua kwa pamoja kuwasaidia. Na kama ni ndugu zake na mke wangu ni mimi ndo ninawapa.

Kwa hiyo nashauri hao wapendwa wachanganye mapato yao na wakubaliane matumizi kila mwezi naamini ugomvi utaisha.
 
Mmmh huu ni ushauri bora sana. I hope utawasaidia wawili hawa. Natarajia kukutana nao ndani ya hizi siku mbili na nafikiri nimepata pa kuanzia.
 
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
280
Likes
5
Points
33
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2010
280 5 33
Dada Carmel,
i quite agree with u. in marriage you need a very matured and understanding person with a vely loving heart. But you are also married and i guess you know our African men are not like that (in generalisations). Hata uwaonyeshe upendo vipi they will still want to pressure you to do more. I guess ni kwa sababu wanaume wengi wasomi wanajua women are more clever than men and hence they feel the should play a more active role.

But siwezi kusemea why she chose her. I saw them while at UDSM and you could tell that they love each other. Hata sasa walipo kwenye ugomvi you can never tell maana wanajua kufake. Kama unakumbuka nilisema ugomvi wao mainly ni wa kitoto and on matters of principle and not on love.

They are a good couple (i wish you knew them)!! usingependa waachane au hata kuwa na affair na watu wa pembeni.

na ikitokea mume hafanyi hayo yote yaani mke anajigharamia mwenyewe na bado anataka mke amsaidie na kuilisha familia inakuwaje? ni fair?

I dont think kwenye hii ni fair kwa mwanaume kudai matumizi baada ya mke kujigharamia. Mwanaume wa aina hii anahitaji kuambiwa kwa upendo kuwa hiyo si sawa.In red, It takes a very matured, and understanding person with a very loving heart to do that. Btw, why did he chose to mary a poor girl with lots of dependants/ i bet he knew it before committing to her.
In blue, na ikitokea mume hafanyi hayo yote yaani mke anajigharamia mwenyewe na bado anataka mke amsaidie na kuilisha familia inakuwaje? ni fair?
 
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2010
Messages
280
Likes
5
Points
33
Caren

Caren

JF-Expert Member
Joined Feb 12, 2010
280 5 33
Sidhani kama mdada ni selfish. Maybe na yeye anataka kuprove point yake. Unajua tena wanawake wasomi hawapendi kuendeshwa.Ila ya mwanaume kuwa strong ndo imepelekea kuwa katika situation waliyopo. Mke akiamua kubaki na stand yake na mume na ya kwake lazima watachokana.

Nakubaliana na mengine yote.

Mume anatakiwa kuhudumiwa familia kuanzia vitu vidogo mpaka vitu vikubwa

Hata hivyo kwa case hii ikiwa mwanamke anafanya kazi (si mama wa nyumbani) lazima asaidie kuhudumia familia "equal proportion of her income" ni wajibu na lazima angekuwa mama wa nyumbani hapo angepewa kila kitu

Huyu mwanamke ni selfish na mwanaume anatakiwa awe strong amwambie achague moja lazima ahudumie familia katika sehemu fulani

Mke wangu anayefanya kazi lazima amlipe house keeper kwa mshahara wake na alipie gharama fulani za nyumbani e.g. vyombo, na partly vyakula

Kuna haja ya kufanya "consensus" na kuangalia kipi ni priority kwenye ndoa yao...na watoto wao
 
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2008
Messages
5,465
Likes
90
Points
0
WomanOfSubstance

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
Joined May 30, 2008
5,465 90 0
[/B]

Central issue ya ugomvi wao ni fedha. Mama anataka fedha za mumewe zitumike kwenye shughuli za ndani kama kununua mboga, kitunguu, chumvi na udongo wa mkewe. Mume anagoma. Mume anasema yeye tayari anagharamia ujenzi wa nyumba kubwa ya vyumba vinne self contained, ananunua mafuta ya gari la mkewe kwenda kazini na vitu kama gesi, mchele na unga. Mume anadai ili kuweka usawa hela ya mama itumike kununua chumvi, udongo n.k kwa kuwa mama alishakataa kuchangia kwenye miradi mikubwa kwa kisingizio mshahara wake ni mdogo na ana baba, mama na dada zake wawili (na watoto wao saba) wanaomtegemea yeye.

Yeye (mke) anasema ndugu zake wakistabilise ataweza kutoa mchango mkubwa katika familia.

Hii ndiyo source ya maugomvi yao ya kitoto. (Sijui nyie mnasemaje).

Right now mke anatishia kuondoka home au kutafuta bwana wa kumuongezea kipato ili achangie home na mume naye ameweka kigingi anasema kama ndoa na iharibike lakini hatatoa hela ya kununua vitu vidogo wakati mkewe naye anapata salary.

Baada ya kuona siwaelewi wana ndugu hawa nikaona nichunguze family background zao.

Mume anatoka katika familia ya wastani lakini inajiweza. Baba na mama yake hawaishi pamoja. Mama anafanya kazi mkoa na anakuja once a month. (Story ni kuwa ugomvi wao ni namna fedha inavyotumiwa. Mama anataka fedha itumike kwa wao kuishi kwa raha na baba anataka kuinvest kwenye assets kwa ajili ya watoto wao).

Mke anatoka kwenye family ya kawaida iliyoko mkoa. Baba na mama wanaishi pamoja kwa kuelewana. Ni wakulima. Tatizo ni dada zake mke. Wako watatu. Wote wamekimbia wanaume zao. Wao na watoto wao saba wako pale hom kwa baba yao. Hawataki kurudi kwa wanaume eti kwa sababu wanafanyishwa kazi sana na hawakuzoea hivyo. Mzee hawezi kumudu kutunza family kubwa hiyo so inabidi mtoto wa kike msomi ndo alipie gharama za matunzo za watu 10 every month.

Maswali yangu:
 1. Je, ni sahihi kwa mume kugoma kulipia nyanya na vitunguu ili abaki na matumizi makubwa tu?

 1. Je, ni sahihi kwa mke kugharamia familia yake ya mkoa at the expense ya kujenga familia yake mwenyewe?
 2. Je, hii familia itaweza kudumu katika ndoa maana mke ameshatishia kuondoka?
 3. Je, matatizo ya kifamilia yanarithishwa kati ya kizazi na kizazi.

Nikipata majibu hapa nitakuwa na wasaa mzuri wa kuokoa ndoa hii. (Nahisi nikimaliza kusuluhisha nitaisubmit hii family kama case study kwa ajili ya Thesis yangu ya Masters of Social Work).
Nitajaribu kutoa mchango wangu kiujumla bila kujibu maswali kwa mpangilio uliouweka hapo juu kama ifuatavyo:
1. Ndoa ni enterprise/(institution) na haipaswi kuivamia kwa kukurupuka bila kujua haswa unaingiaje na kwa mtizamo upi a mipango ipi ya muda mfupi na mrefu.Tatizo hili ni typical kwa waafrika wengi.Mtu hukutana na mtu na kuamua kuoana.Kumbe walipaswa kujadili mambo kadhaa na kukubaliana hasa kama mnatoka backgrounds tofauti kiasi hicho. Ukiangalia mke huyu kutokana na background yake naweza kum summarise kama ifuatavyo:

 • Aliishi maisha very basic - subsistance- kwa maana wazazi wake wakulima hawakuwa na makuu na kwa msingi huu hawakuwa na ugomvi au mipangilio ya matumizi ya fedha.Uchumi wao uliwatosholeza kula.Hakukuwa na surplus ya kuweka akiba au kuwekeza.Si ajabu kusoma kwa huyu mdada was by default tu na ndio maana ni yeye tu ndio alibahatika kusoma na hao dada zake hawakupata elimu ya kutosha.Subsistance economy ya familia iliwafanya waswe aggressive kuchuma surplus na inelezea uvivu wa hao wadada unaowafanya wawakimbie waume zao kisa ati wanafanyizwa kazi.Huyu mwana dada baada ya kupata exposure ya elimu, amezinduka na kutaka kuboresha hali ya huko kwao na kwa vile hakuwahi kuona mama yake akichacharika kuchangia cha ziada nyumbani, haoni ni kwanini amsaidie mume majukumu kama kununua hata vitu vidogovidogo.Kwa msingi huu, mume atakuwa anapoteza nguvu bure kumlazimisha kuchangia.Ni concept ngeni sana kwake!
 • Kwa upande wa mume,huyu naweza kusema kuwa katoka kwenye familia enterprising, iliyoishi zaidi ya subsistence level.Lakini inaonekana hata familia anayotoka siyo yenye wazazi wenye kupanga mipango ya familia pamoja katika namna ya kufikia muafaka.Hivyo pia naye anakosa skills katika ushawishi kwa vile inaonekana wazazi wake nao kila mmoja analazimisha lake ndio litawale na inaelezea jinsi wazazi wanavyoishi kila mmoja kwake na wanaona kwa vipindi.
Ninachoweza kuhitimisha ni kuwa:
1. huyu mume anatoka kwenye dysfunctional family hata kama ina uwezo.Hawezi kumudu uongozi wa familia yake. Angeweza kumshawishi mkewe na kumfanya aone sense ya kuwekeza zaidi kwenye famili yake mwenyewe na kutoa misaada kwao lakini kwa uwezo walio nao.
2. Hii familia ina safari fupi sana kama hawatakuwa waangalifu. Kila mmoja ni mjuaji.
3. Washauri kuwa ndoa ni maelewano, usihirikishwaji na uwajibikaji.Mke asidhani kuwa kazi ya mume ni kumbeba yeye na matatizo ya familia yake.Akumbuke kuwa huyo mume naye katoka kwao hakudondoka toka mtini.Uchungu wa ndugu unauma kwa wote na siyo kwake tu.Mshauri mke kuwa ndoa inakuwa tamu kama watashirikishana kwenye maswala ya msingi hasa matumizi ya fedha.Suala la fedha husambaratisha familia nyinngi hasa pale inapoonekana mmoja anataka kulalia mwingine kama afanyavyo huyu dada.Utu wa mwanamke aliyeolewa ni pamoja na kumsaidia mumewe hapo ndio heshima huongezeka. Wanawake wengi hudai usawa lakini inapokuja swala la uwajibikaji hurudi nyuma kwa kasi ya radi! HII si sawa hata kidogo!Ukitaka haki kumbuka kuna wajibu.Ukitaka kubebwa kwa kila kitu hadi ununuliwe udongo ujue unajinyima haki ya kusema na kutoa maamuzi.

Ninayo mengi zaidi ila kwa sasa niishie hapa.
 
Forum statistics

Threads 1,251,546
Members 481,767
Posts 29,775,740