Matatizo ya mwanamke mwenye wivu sana

Matatizo ya mwanamke mwenye wivu sana

nyaggad

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2014
Posts
1,160
Reaction score
694
Habari wana Jamii forums natumaini mko poa sana.

Leo nipo tena hapa kupeana maarifa,ningependa kutoa udhoefu wangu,juu ya matatizo ya wanawake wenye wivu mkubwa,kwani ninavyojua "wivu"ni moja wapo ya kipimo cha Upendo kwenye mahusiano ya kimapenzi,lakini wivu huohuo ukizidi inakuwa ni tatizo,wazungu hupenda kusema" too much is harmful ".

Wanawake wenye wivu mkubwa huwa wanamatatizo sana,ningependa wanaume wenzagu waelewe mwanamke mwenye wivu mkubwa huwa hakuonei wivu tu,anapokukuta na wanawake wengine mnaongea ama mnezoana,Bali mwanamke mwenye wivu mkubwa hukuonea wivu hadi na vitu unavyovipenda.

Kwa mfano, mwanaume ukiwa unapenda sana kuangalia mpira kama yeye mwanamke hapendi mpira atakuwa hapendi wwe uangalie mpira iwe nyumbani ama unapenda kuangalia sehemu nyingine.

Jambo jingine kwa mfano mwanaume akiwa anampenda sana labda mama yake ama ndugu yeyote au rafiki mwanamke mwenye wivu mkubwa lazima awachukie watu wote unaowapenda sana cause mwanamke mwenye wivu mkubwa huwa anapenda umpende yeyetu.

Zaidi sio kitu chochote,na jambo jingine baya zaidi mwanamke mwenye wivu mkubwa huwa anahasira sana na Mara nyingi huwa ni mtu wa visasi ukimfanyia kosa lazima alipize kwa mfano ukichepuka nayeye akijua lazima achepuke.

Kuna jambo jingine la muhimu la kuelewa sio kila mwanamke mwenye wivu mkubwa anakupenda sana hapana wengine ni roho mbaya tu na wengine huwa ni wachepukaji wakubwa na huwa wanahisi pengine na wwe unachepuka kama wao,si unajua "mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu",yangu ni hayo tu mengine mtaongezea wenyewe.

Note:hakuna binadamu aliyekamilika kama ukikutana na mwanamke mwenye wivu mkubwa na umempenda jiandae tu kisaikojia kuishi nae na kuvumilia kero zake na pengine kumbadilisha.
 
Huwa sipendi mwanaume anayependa mpira masaa yote au 24/7 ni sisa. Inachosha....
 
nina wivu balaa nimeamua kuishi mwenyewe milele i cant stand wanaume hahaha sijui ni mazingira niliyokulia ama nini lakini nina wivu na siamini mwanaume hata mmoja so sina mahusiano yale serious na wanaume wala siwapendi naona wanagegeda tu hawana mapenzi

Ila nipo karibu na wanaume yaani naishi nao kama mi mwanaume ,mwenzao sina marafiki wa kike lakin mapenzi hapana wapite hiviii
 
Kila kitu kiwe moderate....wa aina hii huwa wanashindwa hata kufanya majukumu yao nyumbani

Ok hakuna kitu kipo 24hrs akitoka job atapitia baa kucheki mechi mpk saa tano kisha anarudi. Na mechi zenyewe sio kila siku
 
Ok hakuna kitu kipo 24hrs akitoka job atapitia baa kucheki mechi mpk saa tano kisha anarudi. Na mechi zenyewe sio kila siku
Time hiyo utajua matatizo gani yanaendelea nyumbani na watoto
 
flora msoffe

Pole mkuu flora msoffe unadhani huwapendi wanaume!? La hasha! Ulichonacho ni tatizo la kisaikolojia lililotokana na madhira uliyowahi kupata kutoka kwa wanaume au kushuhudia kutoka kwa mtu wako wa karibu kabisa akitendewa ukatili na mwanaume. Ghafla,ukajikuta unawahukumu wanaume wote na kujenga msimamo akilini.

Mimi nataka kukutia moyo,si kweli kwamba wanaume wote wapo hivyo,ukiondoa kichwani huo msimamo ipo siku utapata mtu ambae utakuwa unajiuliza km ametokea sayari hii hii!! Kuthibitisha hilo,km upo nyumbani au ofisini sasa hivi,toka nje uanze kuwaangalia wanaume nguo zao walizovaa,ni wazi utaona kila mtu kavaa kivyake,wapo utakaowaona wamevaa kawaida sana,

Waliopendeza sana na ambao utawaona kituko. Tofauti hizo utakazoziona ktk mavazi,ndo hizo hizo zipo ktk kila kitu kwa mwanadamu. Binadamu tulivyoumbwa kila mmoja anaamini mawazo yake ni mitizamo yake ndo maana wapo watu miongoni mwetu wanaamini ili afanikiwe,inabidi apate kiungo cha albino. Kuwa huru Dada yangu,ipo siku utampata mtu utarudi hapa kurudia kusoma comment yangu.
 
Last edited by a moderator:
Huwa sipendi mwanaume anayependa mpira masaa yote au 24/7 ni sisa. Inachosha....

Mkuu mpira ni burudani kama zingine2,kwa nni humpendi mwanaume anayependa mpira au na wwe una wivu mkubwa?
 
Back
Top Bottom