Dah usinikumbushe Mimi na ushamba wangu nilitokea kijijini kwenda mbeya. nilikutana nao stend u nayoeleza hivyohivyo ndo walivyoniingiza mjini Mimi, nikaona nauaga umaskini kilaini niliwasindikiza hadi waliposema wanaenda kuuza hayo madini nipate mgao. wakaanza kubishana Yule mwenye mzigo akasema ananiamini Mimi tu hivyo niubebe hadi mwanjelwa wao watakuja nyuma ila niache Simu na tupesa nilitonato nikaona haina shida wanipe na Mie niingie nao mtini. nilipewa nauli ya kwenda tu ya daladala sikujali nilifurahi sana aisee, nikashuka maeneo anayoishi kaka yangu lengo kumpa akauze tukajenge Ghorofa kijijini, Ile kufungua mzigo nikakuta betri ndogo 2 zimechakaa. basi ikala kwangu