AG.6851
Member
- Jul 31, 2013
- 97
- 87
Habaar wana JF
Kwa muda wa iaka mitatu Tofauti Na Katika Maeneo Tofauti, Tanga Na Mbeya, Kuna Watu Nimekutana Nao Wakiwa Na Style Na Mazungumzo Yanayofanana.Jana ndiyo nimetambua kumbe ni wezi/matapeli.
Story Yenyewe Ni Kama Hii
Siku moja katika pitapita zangu maeneo ya Tanga na Mbeya kuna watu walijitokeza mbele yangu na kuonyesha sura ya huzuni na kuchoka na kuniuliza "unaifahamu Hospitali ya Mission ilipo, kwani kuna ajali imetokea ikihusisha Wazungu na sisi tulifanikiwa kuokota kitu flani kwenye eneo la tukio (Akaonesha bahasha ndogo yenye kitu ndani yake)"
Nilimuuliza jina la Hospitali akadai yeye anaijua kwa jina hilo la Hospitali ya Mission, nikamhoji nini lengo lako kama utaipata hiyo Hospital?akajibu "Nimeambiwa nipeleke kitu hiki halafu nitapewa Tsh. milioni moja (1000,000,000/=).
Baada ya kujibu siijui, anatokea jamaa mwingine kama mpita njia alivyotupita huyo jamaa akasema " labda tumuulize huyu anayepita huenda anajua."akamwita na kumuuliza na akauliza "hicho kitu kiko wapi?" akasema "hiki hapa lakini naomba msije kuninyang'anya" alipofungua bahasha ilikuwa na maandishi "Dhahabu hii ni mali ya kaampuni ....... na thamani yake ni Tsh. 100,000,000,000/="
Huyo mpita njia akashangaa kwa mstuko na kuniambia chinichini "Tumnyang'anye unaona dili hili" binafsi sikujua kinachoendelea na nilizidi kumhoji maswali huyo mwenye bahasha alipoona maswali yamezidi na Mungu ameniongoza bila kujua ni wezi walichukuana wawili na kudai wanaenda kuuza.
Kwa style hiyohiyo jana kuna jamaa kalizwa simu sababu eti walibadilishana kwa kuambiwa lata simu yako ma wewe ushike madini haya halafu tunakuja, wakatikomea bila kurudi.
Swali: Wewe walikukuta wapi na kwa style ipi?hata kama walikuliza funguka tu ili iwe funzo kwa wengine.