mi sishangai hata kidogo kuona mambo kama haya yanaibuliwa pasipo ulazima wowote, tushazoea na hii inatupa sura ya pili ya ndugu zetu ingawa bado hawajataka kuwa wawazi zaidi ili jamii ya watanzania kwa ujumla wao tukajua!tatizo lililopo mezani ni juu ya matatizo yaliyotokea arusha,lengo ikiwa ni kujua chanzo ni nini na tufanye nini ili yaliyotokea yasirudie tena. kinyume na matarajio ya wengi watu wenye upeo kama hao pamoja na wanazuoni wantoa tamko kama hilo?? tokezeni mtoe dukuduku lenu,
haya yote ni mazao ya udini aliyoanzisha baba mwenye nyumba,hatutaki nchi yetu iingie katika marumbano na dhambi za kutengana sababu ya udini!tanzania ni moja, tunayo mambo mengi sana ya msingi ya kujadili na sio udini hii ni dhambi ambayo itatufikisha pabaya sana!