Matamanio Yetu (Falsafa Binafsi) | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matamanio Yetu (Falsafa Binafsi)

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by X-PASTER, Jan 25, 2011.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Jan 25, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Matamanio Yetu

  Wakati mwingine uandishi ni uwakilishi wa kweli wa mawazo yako yakiwakilisha jamii ya watu wa aina fulani, aidha kitabaka, kijinsia au hata kiimani.

  Upeo wa maisha ya wanadamu huangazwa kwa nuru ya mapenzi. Mapenzi yana taathira kubwa na ya kudumu na yamna nguvu kubwa katika maendeleo ya kimaada na kiroho ya mwandamu. Nguvu hizo huanzia kwenye mkondo wa maumbile ndani ya dhamiri ya mtu na ya maana na kumalizikia katika hazina kubwa isiyo na kikomo.

  Unapoandika jambo lolote lile kwenye haya majukwaa ya wazi, yakiwemo magazeti au mabaraza ya kwenye mitandao kama JF na mengineyo, wasomaji wako watakuwa wanaiangalia ile jamii unayo iwakilisha kwa jicho la mashaka au bashasha na kuzua maswali mengi vichwani mwao.

  Yatupasa sisi wachangiaji au waandishi wa kwenye haya mabaraza ya kwenye mitandao kuwa makini sana na kile tunacho kiwakilisha kutoka kwenye mawazo yetu na matendo yetu ya kila siku.

  Hadhira ya kwenye mitandao inaweza kutushangaa na kutuona kuwa tumedumaa kimawazo kiasi ya kwamba tunashindwa kutafakali kwenye uhalisia wa hali halisi ya maisha yetu ya kila siku... Hapa nina maana kuwa mwandishi anaweza asione hali halisi ya maisha yake kiujumla, akaangalia kile anachokipenda yeye binafsi kwa kuwa tu, jamii inayo mzunguka imemtengeneza yeye aonekane kama ni liwazo la ngono, ulamali na starehe za muda au ufisadi au imani za kidini na itikadi za kichama.

  Jamii zetu zina matatizo mengi yanayoikabili, matatizo ambayo kila kukicha yanaongezeka na kukosa utatuzi yakinifu. Maadili machafu ni machafu kama vile mwili mchafu usababisha harufu mbaya na kuwakera walio jilani nawe, hivyo hivyo tabia mbaya ukera na kuathiri jamii inayo kuzunguka.

  Mwanadamu mwenyewe ndiye mwenye kujenga heshima na utukufu wake. utakapo jiheshimu na kuzingatia maadili mema, basi utakuwa mfano mwema wa kuigwa katika jamii yako inayo kuzunguka. Siku zote kumbuka kuwa maneno yakikudondoka hayarejei tena mdomoni mwako!

  Katika ulimwengu huu uliojaa taharuki na vioja, binadamu huwa daima katika harakati na pirikapirika akiogelea katika mawimbi ya matatizo na masaibu. Maisha yake hufuatana na mashaka na matatizo, isipokuwa tu awe anachuma maua adimu katika bustani la maisha au awe anapata matumaini na matarajio yake moja baada ya moja. Madhali uzi wa uhai wa mtu haukukatwa kwa mkasi wa mauti, basi kila siku huwa na matumaini, huhangaika na hutafuta mafanikio. Taa ya matumaini ndiyo inayomwangaza mwenye matumaini, na matumaini hayohayo ndiyo yanayomgeuzia maisha yake machungu kuwa matamu.

  Mtu mmoja huwa na tamaa ya kupata utajiri mkubwa na hutumia jitahada zake zote kuweza kuupata. Mwingine hutaka cheo na umashuhuri na huhangaika sana mpaka apate matakwa yake. Mwingie uangalia nani kamtongoza nani au nani kasema nini...! Matakwa ya kila mtu yanategemea mahitaji yake ya kimwili na ukamilifu na usalama wa roho yake, lakini mawazo ya kila mtu yanatofautiana kabisa kutokana na namna ya kufikiri na kufahamu kwao kulivyo.

  Ni lazima tulizingatie hapa jambo hili la kimsingi, kwamba matakwa na matamanio huzalisha ufanisi na mafanikio wakati yanapoafikiana na mahitaji ya kiroho, yanapotimiza mahitaji ya kifikra, na yanapopandisha na kukuza kiwango cha maarifa. Vivyo hivyo, ikiwa taa inayong'ara ya mtu itaangaza maisha yake, basi atatoka kwenye giza la kutisha la masaibu na mashaka.

  Huenda mara nyingine mojawapo kati ya silika za kimwili kama vile uroho au ubarakala ikaasi na kuwa ni chanzo cha masumbuko ya mtu. Uhasidi ni mojawapo kati ya matunda ya silika za kimwili kitamaa, ambao hujidhihirisha kwa kutamani vibaya, kuitia pingu dhamiri njema na tambuzi, na kumzuia mtu kuyapata matarajio halisi ya maisha yake. Mwenye kijicho hawezi kumtazama mwenzake akistarehe au akifanikiwa; moyo wake humchoma na husononeka kila anapowaona wenzake wananeemeka.

  Roho zetu ni kama jangwa lisilo na ngome wala ukuta ambapo wezi wa furaha na mafanikio huweza kuingia kwa urahisi. Upepo mdogo kabisa huzitia wahaka na wasiwasi nyoyo zetu. Maadui wengi wa tamaa na hawaa huingia majumbani mwetu na kila mmoja hutuamrisha na hutusugua roho zetu.

  Kila mjinga hujua kwamba anapoumwa sana na kichwa inambidi aende kwa daktari kutibiwa, lakini yule mwenye kuugua uhasidi inambidi ateketee moyoni mwake!

  Kuna masuwala ambayo yameanza kujikita sana kwenye mabaraza ya mitandaoni, masuwala ambayo athari yake kama hatuta tatua sasa basi itakuwa majuto makubwa sana siku za mbeleni. Masuwala haya ni yale ya kiitikadi za Kidini na Kichama. Haya ni masuwala ambayo yemesababisha upofu wa akili na nafsi, kiasi ya kwamba hatuoni wala hatusikii lolote lile lililo nje ya itikadi zetu. Haya masuwala ambayo moto wake kama hatutoangalia basi utateketeza taifa letu na kutujengea uadui wa kweli uko mitaani.

  Jamii zilizojikita mitandaoni hivi leo, inalichukuliya suala hilo la Ubaguzi wa kidini na Kichama, kuwa ni muhimu sana kwenye bongo zao, kiasi ya kwamba kutoa uzito wa tani kadhaa za chuki ma machafuko yenye kuathiri nafsi na bongo za wasomaji. Lakini kiuhalisia na hasa wale ambao wapo ugenini haswa nchi za ulaya na Amerika. Wamekuwa wanashikana na kushirikiana kwa misingi ya maeneo walikotoka, yaani Utaifa. Hadi imefikia shughuli mbalimbali kuendeshwa kwa misingi hiyo pamoja na shughuli hata za dini ambazo mtu si wa imani ile uudhuria na kushiriki kikamilifu kabisa.

  Na vile vile tunasoma kumbi nyingi katika mitandao ambazo zimeanzishwa na watu kwa misingi ya Utaifa! Na wanachama ni wale wanatoka katika maeneo au taifa moja, bila kuangalia kama wewe ni Muislam, Mkristo au mwenye kuamini imani za jadi au kutoamini kitu kinachoitwa dini. Huwe mwenye itikadi ya chama au si mwenye itikadi za chama. Hawa wote ukubaliwa na kuwa mwanachama na hata kama katoka taifa jingine, ili mradi tu umekubaliana na sheria na kanuni za kumbi baraza.

  Ni muhimu sana kwa wale wenye kuleta udini au itikadi za kichama washiriki katika kuimarisha hali ya Utaifa! Ni jambo la kusikitisha sana kuona baadhi ya wasomi wamelinyamazia jambo hilo na hali wanaliona mbele ya macho yao na kusikia likizungumziwa na zaidi ni kuwa kuna hata kati yao wenye kushiriki katika kuihamasisha na kuikuza hali hiyo.

  Kwa hivyo, ni wajibu wa kila mmoja wetu, kuyapiga vita kwa nguvu zote kila ambapo tutaona mambo haya yanajitokeza. Na khasa kwa wale viongozi na wasomi wa kidini, kichama na wasimamizi wa haya majukwaa baraza, wahakikishe mambo haya hayapewi nafasi kwani ni adui wa nchi yetu na dunia yetu, na sio wao kuwa wa mbele kuyashabikia au kuyanyamazia.

  Basi namalizia kwa kusema kwamba, "Mapenzi ya kijamii ni sababu muhimu kabisa ya mtu kupata maendeleo na mafanikio mazuri katika maisha yake. Yule mtu anayeonyesha ustahiki wake na sifa zake njema ndiye anayeweza kutawala nchi za nyoyo zetu na kupanda ngazi ya maendeleo kwa kunufaika kwa msaada na ushirikiano wa jamii na kupata ufunguo wa mafanikio. Mtu mzuri kwa tabia na amali ni kama taa inayong'aa yenye kuongoza fikra na maendeleo ya jamii. Usafi wake wa moyo una taathira kubwa katika muundo wa maadili ya watu."

  Basi na tujirekebishe japokuwa hatupendi.
   
 2. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #2
  Jan 30, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
 3. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #3
  Feb 13, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Nimeipenda sana hii makala/angalizo lako, ni kweli na sahihi kabisa kwa ulichosema.
   
 4. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #4
  Feb 13, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Article nzuri ila niambie matakwa na matamanio hutokea wakati mmoja?
  Na ni vipi matakwa na matamanio yakazalisha ufanisi na mafaniko?
   
 5. MIAMIA.

  MIAMIA. JF-Expert Member

  #5
  Feb 14, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 216
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mh@tks x-paster
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Matakwa na matamanio yetu, yasiende kinyume na sheria na imani zetu.
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Jul 2, 2017
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,323
  Likes Received: 22,152
  Trophy Points: 280
  somo zuri sana
   
Loading...