Matajiri CCM wazidi kubanwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Matajiri CCM wazidi kubanwa

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by BAK, Nov 11, 2008.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Nov 11, 2008
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,910
  Likes Received: 83,368
  Trophy Points: 280
  Date::11/11/2008
  Matajiri CCM wazidi kubanwa
  Na Ramadhan Semtawa, Dodoma
  Mwananchi

  KAULI ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete kutaka wanachama wachague siasa au biashara ifikapo mwaka 2010, imezidi kudhihirika baada ya wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya chama hicho kuitaka serikali iharakishe muswada wa kudhibiti fedha katika kampeni za uchaguzi.

  Shinikizo la wajumbe hao lililotolewa katika kikao cha NEC kilichomalizika juzi mjini Dodoma, lilithibitishwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi, Kapten John Chiligati aliyesema lengo la kutaka muswada huo haraka ni kuzuia mchezo mchafu katika kampeni ambao hufanywa na baadhi ya watu wenye fedha.

  Iwapo muswada huo wa sheria utapelekwa na kisha kupita na kutiwa saini na Rais kuwa sheria, pamoja na kubana vyama vingine utawabana zaidi baadhi ya mafisadi ndani ya CCM, ambao wamekuwa wakijipanga kuelekea Uchaguzi Mkuu wa 2010.

  Kepten Chiligati alifahamisha kuwa baada ya wajumbe kutoa msimamo huo, kikao kiliafiki na kuitaka serikali ifanye hivyo ili kuweka uwanja sawa wa kidemokrasi katika kampeni kuanzia ndani ya chama hicho.

  Alifafanua kwamba, uamuzi huo unatokana na kuwepo malalamiko kutoka kwa baadhi ya wagombea wasio na fedha kwamba wamekuwa wakichezewa mchezo mchafu na baadhi ya wagombea wenye fedha.

  "Ni kweli wajumbe wameitaka serikali iharakishe kuandaa muswada wa sheria hiyo ambayo itadhibiti matumizi ya fedha katika kampeni ili kuondoa malalamiko ya kuwepo mchezo mchafu," alifafanua kepten Chiligati.

  Alisema pamoja na mambo mengine, muswada huo utapaswa kuangalia fedha za kampeni zinakotokea, zimepatikana kwa njia ipi na lazima pia kuwe na kikomo cha fedha za kampeni.

  "Nchi za wenzetu wana utaratibu wa kudhibiti fedha za kampeni, sisi hapa kwetu siku zote mambo yamekuwa yakienda kiholela tu, sasa tunataka kuwepo sheria ambayo itaonyesha mtu amepata wapi fedha za kampeni na kiwango cha juu kiwe kipi," aliongeza.

  Suala la fedha katika kampeni za uchaguzi nchini hasa ndani ya CCM limekuwa likilalamikiwa na baadhi ya wagombea wenye uwezo mdogo kifedha ambao hukosa nafasi licha ya kuwa na uwezo wa kuongoza, wekikosa kutokana na chama hicho kuvamiwa na wafanyabiashar wenye fedha ambao huzitumia katika kampeni kuanzia ngazi ya kura za maoni.

  Wakati mafisadi wakibamnwa kwa kutumia mlango huo, mlango mwingine wa nyuma pia unaonmyesha kuwabana kwani chama hicho pia kimeazimia kuaandaa utaratibu ambao unakirejesha katika enzi za TANU na CCM ya akina Mwalimu Nyerere, ambayo wagombea ubunge, udiwani watapaswa kupatikana kuanzia ngazi za mashina.

  Duru za ndani kutoka katika kikao zilisema ajenda hiyo ilijadiliwa kwa mapana.

  Akizungumzia ajenda hiyo inahusu namna ya kupata viongozi bora wa chama katika dola, Chiligati alisema utaratibu huo ambao unaendelea kufanyiwa kazi unalenga kuhakikisha kuwa kiongozi anayechaguliwa anakubalika katika ngazi zote kuanzia ya chini kwa kupigiwa kura na kila mwanachama.

  "Kwa hiyo sasa hivi tunaangalia namna ya kuhakikisha tunapata viongozi bora wa dola, tunaangalia namna ambavyo kila mwanachama wa CCM atakuwa akishiriki kumchagua diwani diwani ndani ya chama," alisema Chiligati.

  Alisema lengo kumudu gharama za usafiri ambazo zitakuwa ni kuzunguuka matawi yote kwa sababu kila mwanachama hadi katika shina lazima apigie kura.

  Aliongeza kwamba, kwa kufanya hivyo kutasaidia chama kupata viongozi bora wa dola ambao wanakubalika na kufahamika vema na wanachama kuanzia katika mashina.

  Akisisitiza namna ya kupata viongozi bora, alisema wagombea watapaswa kujaza fomu maalumu ambazo zitaonyesha historia zao halisi, vipato vyao na taarifa zote muhimu kwani baadhi yao ndiyo wanaokuwa mawaziri.

  Kwa msisitizo alisema: "Katika hili tutahakikisha tunashirikiana pia na vyombo vya dola kuhakikisha wanaojaza fomu zao wanakuwa ni watu wenye kutoa taarifa za kweli na si uongo, maana lazima tuwaangalie kwani baadhi yao ndiyo huwa mawaziri. "
   
 2. u

  usheh Member

  #2
  Jan 14, 2010
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tumebakiwa na miezi tisa tu ili Uchaguzi Mkuu uanze hapo Mwezi wa Oktoba2010,je sheria hii itapishwa kweli au ni maneneo ya kisiasa ya hapa nyumbani?
   
 3. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Changa la macho hilo.. yeye kafikaje hapo kama sio hao akina RA, Zadock, Balhabou, Manji na hao wanaotuibia?
   
Loading...