Mataifa ya Ulaya kuendelea kutoa chanjo

Mataifa ya Ulaya kuendelea kutoa chanjo

Analogia Malenga

Platinum Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,292
Reaction score
10,842
Mataifa makubwa barani Ulaya yamesema yataanzisha upya matumizi ya chanjo ya AstraZeneca baada ya chombo cha udhibiti wa kitabibu cha Ulaya kusema chanjo hiyo ni salama na inafanya kazi vizuri.

Mataifa makubwa barani Ulaya yamesema yataanzisha upya matumizi ya chanjo ya AstraZeneca baada ya chombo cha udhibiti wa kitabibu cha Ulaya kusema chanjo hiyo ni salama na inafanya kazi vizuri.

Na wala haina uhusiano na athari za kuganda kwa damu baada ya matumizi yake. Kauli hiyo inafuatia ile ya shirika la afya duniani WHO na lile la uangalizi wa afya la Uingereza kwa pamoja kusema chanjo hiyo ni salama.

Muda mfupi baada ya Shirika la Uangalizi wa Madawa la Ulaya (EMA) kutangaza usalama wa AstraZeneca mataifa ya Ulaya yaliotangaza kuendelea na chanjo hiyo ni pamoja na Ujerumani, Ufaransa, Uhispania, Italia, Uholanzi, Ureno, Lithuania, Latvia, Slovenia na Bulgaria.

Pia soma:
Orodha ya nchi zilizositisha utoaji wa chanjo ya Astrazeneca
Thailand yasitisha matumizi ya AstraZeneca kupisha tathmini zaidi
 
Mabeberu hawana nia mbaya katika huu ulimwengu,wanaumiza kichwa kutatua tatizo la corona maana hata wao linawasumbua sana,lazima wawe makini na accurate katika kutafuta ufumbuzi,yaani katika watu mil 15 waliopata chanjo then watu 40 wamepata blood clot then ndio unaconfirm kwamba chanjo ndio iliyosababisha? Elimu, Elimu ,Elimu.
 
Mataifa makubwa barani Ulaya yamesema yataanzisha upya matumizi ya chanjo ya
Sijui kama hizo chanjo ni salama maana nimesikia mataifa mengine yanazikataa kwa kusababisha watu 17 kuganda damu.

Naona sisi tutumie tu njia za kujikinga kama kuvaa barakoa ila chanjo imenipa mashaka hata kama rais ajae akiona ije ila mmm naogopa.
 
Mabeberu hawana nia mbaya katika huu ulimwengu,wanaumiza kichwa kutatua tatizo la corona maana hata wao linawasumbua sana,lazima wawe makini na accurate katika kutafuta ufumbuzi,yaani katika watu mil 15 waliopata chanjo then watu 40 wamepata blood clot then ndio unaconfirm kwamba chanjo ndio iliyosababisha? Elimu, Elimu ,Elimu.
Kwani hilo tatizo la CORONA limeletwa na nani?
 
Jibu swali wewe; ni muhenga sana mimi na wewe bado kigoli kabisa. Nauliza tena, kwani CORONA imeletwa na nani?

Swali lako ni la kijinga , halina mantiki yeyote. Labda ungesema malaria imeletwa na mabeberu kidogo ungeeleweka kwasababu kwao haupo(mazingira hayawafevi mbu kwao) ila upo nchi za kitropical.

Mabeberu watengeneze ugonjwa ambao unawatesa hadi wao na hawana dawa ya kuutibu? Kabla ya kutengeneza huwa wanatengeneza na ya kutibu/kukinga kama wangekuwa na nia hiyo.
 
Changa la macho.

wanataka kuwaaminisha Nchi zingine Kama za Kiafrica waendelee kutumia

Wao wameshaziacha usije kuona chupa imeandikwa AstraZeneca ukadhani yenyewe kumbe wamebadilishwa.
 
Mabeberu hawana nia mbaya katika huu ulimwengu,wanaumiza kichwa kutatua tatizo la corona maana hata wao linawasumbua sana,lazima wawe makini na accurate katika kutafuta ufumbuzi,yaani katika watu mil 15 waliopata chanjo then watu 40 wamepata blood clot then ndio unaconfirm kwamba chanjo ndio iliyosababisha? Elimu, Elimu ,Elimu.
Nini kilisababisha? Je ikitokea hii chanjo ikawa na hayo madhara kwa muda wa usoni kwa sababu haijapitia hatua za kawaida hauoni kama kutakuwa na global catastrophe kwa sababu asilimia kubwa wamechanjwa fasta na chanjo ya majaribio?

Anyway usione kama wanaopinga hii chanjo hawana elimu. Hicho ni kibri kisicho na faida wala maana!
 
Sijui kama hizo chanjo ni salama maana nimesikia mataifa mengine yanazikataa kwa kusababisha watu 17 kuganda damu.

Naona sisi tutumie tu njia za kujikinga kama kuvaa barakoa ila chanjo imenipa mashaka hata kama rais ajae akiona ije ila mmm naogopa.
Ukiacha wenye matatizo kama pumu, moyo n.k, Corona ina revovery rate ya 99.9+%

Sasa jiulize kwa ugonjwa wa aina hii kwa nini chanjo isukumwe kwa nguvu hivi?

The disease, the business and the politics!
 
Sijui kama hizo chanjo ni salama maana nimesikia mataifa mengine yanazikataa kwa kusababisha watu 17 kuganda damu.

Naona sisi tutumie tu njia za kujikinga kama kuvaa barakoa ila chanjo imenipa mashaka hata kama rais ajae akiona ije ila mmm naogopa.

Chanjo za AstraZeneca ni majanga matupu, Dunia itakuja kushtuka wakati imekwisha chelewa - mataifa ya kiafrica zisikubali raia wake kuchanjwa chanjo ambazo hatujui short na long term madhara yatakuwaje - majaribio ya chanjo yanapaswa si chini ya miaka minne/mitano - Big Pharma Companies wasilazimishe chanjo zao kuingizwa sokoni kwa madhumuni ya kupiga hela ndefu na kuhatarisha maisha ya watu. Mbona watu wengi wamepona kwa kutumia broad spectrum anti biotic capsules,multvitamins na minerals ku-boost immune systems zao - kuna vile vile wonder drung namely "invermectin" ambayo ineonekana hiko highly effective dhidi ya kovid lakini inapigwa vita na Big Pharma Companies wakishirikiana WHO - hawataki cheap drugs kuharibu biashara zao za chanjo ambayo ni relatively expensive ukilinganisha na ivermectin.

Nasemaje? Chanjo zifanyiwe utafiti na majaribio ya kutosha kabla hazija ingizwa sikoni, wasitake kuhatarisha maisha ya watu kwa upuuzi wao.
 
Back
Top Bottom