Mataifa ya Kifaransa yavunja uhusiano na Burundi.

Consigliere

JF-Expert Member
Sep 9, 2010
12,037
24,625
Shirika la mataifa yanayozungumza lugha ya Ufaransa OIF limevunja ushirikiano wake na Burundi, likidai kushindwa kwa taifa hilo kupiga hatua ya mazungumzo ili kumaliza mgogoro unaoendelea.

Katika taarifa, OIF limeshutumu hali mbaya ya usalama nchini humo na kusema kuwa linaondoa mipango yake yote isipokuwa ile inayowasaidia raia wa Burundi na zinaweza kusaidia kuimarisha demokrasia. Mataifa ya OIF ni 57 na serikali.

Zaidi ya watu 400 wamefariki huku takriban 250,000 wakilitoroka taifa hilo tangu ghasia kuzuka kufuatia hatua ya rais Pierre Nkurunziza ya kuwania muhula wa tatu.

Msemaji wa serikali ya Burundi amekuwa na hasira akijibu habari za kupigwa arufuku katika shirika hilo katika mtandao wa Twitter.Licha ya ushauri,alitumia lugha ya shirika hilo kulishtumu kwa kupuuza uwezo wake.

''Wanadhani wao ni mungu na Burundi ni lazima iliabudu shirika hilo''.

Source: BBC
 
Vyuma na interahamwe wenzako wa Bujumbura naona dunia imewashtukia, ila kiama chenu ni siku warundi wakigundua Nkurunziza na serikali yake ni genge la wahuni tuu
 
Vyuma na interahamwe wenzako wa Bujumbura naona dunia imewashtukia, ila kiama chenu ni siku warundi wakigundua Nkurunziza na serikali yake ni genge la wahuni tuu
Burundi ilikuwepo hata kabla ya AU, UNO na mashirika mengine yote unayoyafahamu. Kumbuka pia Burundi ilikuwepo hata kabla ya umoja wa mataifa yanayozungumza kifaransa na itaendelea kuwepo hadi kiama.
 
Burundi ilikuwepo hata kabla ya AU, UNO na mashirika mengine yote unayoyafahamu. Kumbuka pia Burundi ilikuwepo hata kabla ya umoja wa mataifa yanayozungumza kifaransa na itaendelea kuwepo hadi kiama.
Daah wewe ni mwananchi mzalendo kabisa wa Burundi. Hongera kwa uzalendo wako wa kiwango cha juu mkuu.
 
Daah wewe ni mwananchi mzalendo kabisa wa Burundi. Hongera kwa uzalendo wako wa kiwango cha juu mkuu.
Angalia lakini isije ukawa na maslahi binafsi aidha kwa Nkurunzinza au kwa serikal yake

Piganieni uhuru na demokrasia ya kweli msije kama ccm ukienda Zanzibar walewale na ukija bara walewale
 
Angalia lakini isije ukawa na maslahi binafsi aidha kwa Nkurunzinza au kwa serikal yake

Piganieni uhuru na demokrasia ya kweli msije kama ccm ukienda Zanzibar walewale na ukija bara walewale
Hahaha mkuu read between the lines utanielewa vzr mkuu.
 
Back
Top Bottom