Maswali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kichankuli, May 22, 2009.

 1. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 857
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Swali langu linatokana na sehemu ya mchango wa Mwakyembe katika Bunge kama ilivyo hapo chini

  Mheshimiwa Mwakyembe aliwasilisha hoja zake kama hivi:

  "Wakili wa Serikali hana usafiri. Yeye na daladala, daladala na yeye. Mvua inyeshe, jua kali, akiwa na mafaili ya Serikali. Wakili wa Serikali tunamtegemea awe smart; suti nyeusi, kiatu cheusi, soksi nyeusi, shati jeupe na haliwezi kuwa moja tu, litaleta utando wa kutisha, kwa hiyo, mashati ya kutosha meupe, tai nyesi na tai maalum nyeupe. Lakini pesa tunayompa Wakili wa Serikali kununulia vitu hivyo, haitoshi hata kununulia robo ya vitu hivyo. Nafikiri kuna umuhimu sasa hivi kuongeza bajeti ya Wizara hii".

  1) Ni mtumishi yupi wa Serikali ambaye ana sifa za kielimu kama za wakili wa Serikali ambaye hastahili kuwa na usafiri

  2) Ni mtumishi yupi wa Serikali ambaye hastahili kuwa smart? je ni Mhasibu, Daktari, Nesi, Mwalimu, Afisa Mifugo na Kilimo, Afisa Mipango, Mchumi, Mhandisi, au Mhudumu, Katibu Muhtasi, Afisa Mtendaji wa Kijiji, Dereva au Mesenja?

  3) Hao Askari waPolisi, JWTZ ambao wanapiga raia na Askari wenzao wa majeshi mengine kila kukicha ambao kwa mujibu wa taratibu zao wanatakiwa kukaa kwenye makambi na siyo kuchanganyikana na Raia hawajafanyiwa hivyo?

  Wabunge wanatakiwa kujenga hoja ambazo zinalenga kuwapatia maslahi mazuri watumishi wote wa Serikali kulingana na sifa za kielimu na kiutendaji walizonazo bila kuwabagua kuwa hawa ni wa hazina, Ofisi ya Rais au usalama wa Taifa

  http://www.parliament.go.tz/POLIS/PA...12-45-2008.pdf
   
 2. M

  Magezi JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2009
  Joined: Oct 26, 2008
  Messages: 2,827
  Likes Received: 87
  Trophy Points: 145

  Swali lako ni lipi hapa mkuu sijaelewa?
   
 3. Kichankuli

  Kichankuli JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2009
  Joined: Dec 18, 2008
  Messages: 857
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 45
  Maswali yangu ni haya matatu

  Ni mtumishi yupi wa Serikali ambaye ana sifa za kielimu kama za wakili wa Serikali ambaye hastahili kuwa na usafiri

  2) Ni mtumishi yupi wa Serikali ambaye hastahili kuwa smart? je ni Mhasibu, Daktari, Nesi, Mwalimu, Afisa Mifugo na Kilimo, Afisa Mipango, Mchumi, Mhandisi, au Mhudumu, Katibu Muhtasi, Afisa Mtendaji wa Kijiji, Dereva au Mesenja?

  3) Hao Askari waPolisi, JWTZ ambao wanapiga raia na Askari wenzao wa majeshi mengine kila kukicha ambao kwa mujibu wa taratibu zao wanatakiwa kukaa kwenye makambi na siyo kuchanganyikana na Raia hawajafanyiwa hivyo?

  Samahani ile website ilitakiwa ije kabla ya maswali
   
Loading...