Maswali Yangu Live kwa Mgombea wa Urais Kuiptia CCM - JAKAYA KIKWETE MRISHO. KESHO. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Maswali Yangu Live kwa Mgombea wa Urais Kuiptia CCM - JAKAYA KIKWETE MRISHO. KESHO.

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by ELNIN0, Oct 28, 2010.

 1. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #1
  Oct 28, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Maswali yangu kwa Mgombea wa CCM Jakaya Kikwete.

  Ndugu mgombea Jakaya Kikwete utakubaliana na mimi huwezi Kujenga Uchumi imara bila kuwa na MIUNDOMBINU imara - SWALI

  Je CCM ilichukua hatua gani kushughulikia mashirika muhimu yaliyoingia mikataba yenye utata? kwa mfano TRL na ATC? Je CCM ina mikakati gani endelevu kuhakikisha mashirika haya yanafufuka na kuendelea kufanya shughuli za usafirishaji ki ufanisi?


  2. Mweshimiwa utakubaliana na mimi kuwa nchi yeyote ile inayotaka maendeleo kwa wananchi wake lazima nchi iwekeze kwenye ELIMU, sasa Ilani ya Uchaguzi ya chama chako inaema Elimu ya bure haiwezekaniki lazima ichangiwe na wananchi. Juzi juzi waziri wako wa elimu amepingana na Ilani yako ya chama cha mapinduzi kwa kutamka kwamba elimu itakuwa bure mpaka kidato cha nne bila hata wanafunzi kufanyikwa mitihani, huoni kwamba huu sasa ni utata mkubwa? tunaomba ufafanuzi wako maana linatuchanganya sisi wananachi.

  Muheshimiwa Jakaya- ulipoingia madarakani mwaka 2005 uliahidi MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA, Ulikuw an amaana ya MAISHA YAPI? kwa hali halisi utakubalia na mimi kwamba maisha yamezidi kuwa magumu kupndikia, na leo hii upo hapa unataka tukupatie miaka mingine mitano, Tunaomba utupe mikakati yako uliyoiandaa mara tu baada ya kuingia madarakani katika sehemu muhimu zifuatazo
  a) Makazi b) Afya za wananchi wako c) Ajira d) Mfumuko wa bei hasa za vyakula.

  3. Mweshimmwa mgombea wa kitu cha urais kupita CCM wewe ni mpiganaji wa UFISADI numberi ONE wa nchi yetu, sisi wananchi tumekuwa na utata juu ya tuhuma za wizi wa mali za umma ambapo serikali yako na ile ya awamu ya tatu iliingia mikataba feki na wakwekezaji, umelishughuikia hilo ingawa bado hatujaridhika na utendaji kazi wako. sasa tukikupa mingine mitano je una mikakati gani ya kukomesha kabisa ufisadi katika nchi yetu?

  Nyongeza
  Kagoda na Richmood ni baadhi tu ya UFISADI mkubwa ambao umezua utata mkubwa katika nchi yetu, hivi kwa kutumia vyombo vyako vya ulinzi na usalama ukiwa amiri jeshi mkuu umeshindwa kuwajua ni kina nani na wafikishwa katika vyombo vya haki? ? Je unazungumziaje suala la wantanzania kuweka mapesa nje ya nchi?, je una mikakati gani tukikupa mingine mitano kushughulikia haya?

  Kwa ufupi tu mheshimiwa kuokoa muda, tupe mafanikio madogo tu ya kauli mbiu yenu ya KILIMO KWANZA, ingawa tunajua si muda mrefu sana tangu kauli mbiu hii kuanza kutumika, tunaomba ugusie Mafanikio, Challenges na Mikakati uliyonayo kwa miaka mingine mitano.

  ASANTE.

  ROSE MWAKITWANGE YAWEKE VIZURI HAYO. (EDIT)
   
 2. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #2
  Oct 28, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Mi nina maswali mengi mpaka nashindwa nianze na lipi?
  Mtakaopewa special mwaliko mtuwakilishe kama wazalendo wa nchi na si kama wakereketwa wa CHAMA
   
 3. HISIA KALI

  HISIA KALI JF-Expert Member

  #3
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 694
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa watakuwa wameandaa vibaraka wake tu kwenda kuuliza maswali ya siasa nyepesi. Hakuna swali gumu wala lenye utata atakalouzwa. Waandishi na wananchi watakaoende pale watakuwa wamepewa maswali ya kuuliza. Kama kweli anataka kufanya mdahalo wa kweli waruhusu maswali ya wananchi kupitia kwenye simu.
   
 4. Nyambala

  Nyambala JF-Expert Member

  #4
  Oct 28, 2010
  Joined: Oct 10, 2007
  Messages: 4,470
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Mkuu unaonaje ukiyapitishia pia kwa Maggid? It is time to prove him kwamba yuko fair au????????
   
 5. Shalom

  Shalom JF-Expert Member

  #5
  Oct 28, 2010
  Joined: Jun 17, 2007
  Messages: 1,315
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  La kwangu ni fupi, awape hai walinzi wake wanne!
   
Loading...